Pamoja na kwamba katika mambo mengine hayana ushahidi wa moja kwa moja kuhusu ushiriki wako lakini hili la Rwakatale linakutia hatiani moja kwa moja kuwa ulishiriki pasiposhaka kuwa wewe ndiye uliyekuwa bwana mipango wa mambo yote yaliyompata Rwakatale na uthibitisho wake ni kinywa chako mwenyewe kwa kusema kuwa Rwakatale ni gaidi na ukotayari kwenda kutoa ushahidi kuthibitisha kauli yako mpaka mbinguni.
Mwisho wake ilikuja kubainika kuwa hakuna cha ugaidi wala mama yake ugaidi anaohusika nao Rwakatale, mateso aliyopata pamoja na familia yake yalitokana na mambo ya kutungwa kiongozi ukiwa ni wewe mwenyewe, na sijui ni kitu gani kilichokufanya ujitoe muhanga kumuzulia mwenzako na kuteseka kwa kitu ambacho hakukifanya na ninaamini kuwa hata roho yako inakusuta kwa vitendo vya kizushi ulivyomfanyia mwenzako.
Nahapo ndipo ninapoona kuwa ni vigumu sana kwa mwanasiasa hasa kwa wanasiasa watawala kuja kuuona ufalme wa mbinguni.
Unahitaji kuombewa, unakwenda kanisani kila jumapili unakwenda msikitini kila ijumaa lakini raia wako wanatekwa na kuuawa, raia wako wanapigwa risasi mchana kweupe, na hakuna hatua zozote unazozichukua kama kiongozi, raia wanafunguliwa kesi za kubambikizwa yote hayo kwako unaona ni sawa tu kwa kuwa siyo wafuasi wako.
Pengine hata kiti ulichonacho umepata kwa kudhulumu, umehonga ndo ukapata, umedhulumu haki ya wapiga kura ndo ukapata, umechinja wapinzani wako ndo ukapata, umeiba kura ndo ukapata, umefanya kama kile kilichofanyika kwenye uchaguzi wa serekali za mitaa ndo ukapata, na yote haya unaona uko sawa tu na bila aibu unahitaji kuombewa na unakwenda kanisani na msikitini kumwabudu Mungu.