Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,891
- 8,448
Anaandika Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti Chadema kuhusu Covid 19
Kama wanaruhusiwa kurudi itakuwa ni kwa sababu hawakuwa na makosa yoyote, ila sisi ndio tuliowakosea. Kama tukiwaruhusu kurudi maana yake ni kwamba sisi viongozi wa chama wote tulikuwa waongo, ila wao ndio walikuwa wa kweli.
Kumbukeni tuliyoyasema hadharani na kwenye vikao vya chama; na waliyoyasema wao hadharani na mahakamani kwa kiapo:
1. Sisi tulisema Kamati Kuu haikuwateua wao, na wala haikuteua Mgombea yeyote wa viti maalum na Katibu Mkuu wetu hakuwahi kujaza fomu za uteuzi zilizokabidhiwa kwake na Tume ya Uchaguzi kama inavyotakiwa na Sheria za Uchaguzi.
2. Wao walidai mahakamani kwa kiapo kwamba walienda kuapa ubunge kwa baraka za chama na walimtaja Katibu Mkuu kuwa alijaza fomu zao za uteuzi.
3. Tulisema hadharani kwamba walikiuka maagizo ya Kamati Kuu kutoutambua uchafuzi mkuu na matokeo yake, huku wengi wao wakiwa wajumbe wa Kamati Kuu na viongozi waandamizi wa chama. Wao walidai hawakufanya kosa lolote kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama.
4. Dhana ya wao kuomba msamaha ina matatizo makubwa kimantiki. Baada ya kuwafukuza uanachama walikimbilia mahakamani kwa madai kwamba tumewakosea. Na wameendelea kudai hivyo hata baada ya Mahakama Kuu kuamua kwamba Kamati Kuu haikukosea kuwafukuza, na wamekata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu.
5. Wakati wa maridhiano, mojawapo ya madai yetu ilikuwa ni kuondolewa kwao Bungeni na wakati fulani tuliambiwa kwamba Samia amekubali kuwaondoa. Hilo halikutokea. Na halikutokea kwa sababu Samia na CCM haijawahi kukubali kuondolewa kwao Bungeni.
Soma Pia: Halima Mdee kushawishi Covid-19 kurudi CHADEMA, je Wasamehewe na Chama au Wananchi?
6. Kumekuwa na kampeni kubwa ya kichini chini, ndani na nje ya chama, ya kuwarudisha wasaliti hawa kwenye chama. Mimi siamini kwamba kampeni hii ina maslahi yoyote ya chama. Ninaamini kwamba wanataka au wanatakiwa warudi ili waweze au wawezeshwe kugombea Ubunge mwaka ujao. Mark my words.
7. Kama tunataka warudi, haiwezi ikawa ni kwa sababu sio wasaliti na hawakukosea. Itakuwa ni kwa sababu hatuna tena nguvu au ujasiri wa kupambana na watu wa aina hii.