Anaandika Tundu Lissu kuhusu kurudi kwa wabunge 19 waliofukuzwa CHADEMA

Anaandika Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti Chadema kuhusu Covid 19

Kama wanaruhusiwa kurudi itakuwa ni kwa sababu hawakuwa na makosa yoyote, ila sisi ndio tuliowakosea. Kama tukiwaruhusu kurudi maana yake ni kwamba sisi viongozi wa chama wote tulikuwa waongo, ila wao ndio walikuwa wa kweli.

Kumbukeni tuliyoyasema hadharani na kwenye vikao vya chama; na waliyoyasema wao hadharani na mahakamani kwa kiapo:

1. Sisi tulisema Kamati Kuu haikuwateua wao, na wala haikuteua Mgombea yeyote wa viti maalum na Katibu Mkuu wetu hakuwahi kujaza fomu za uteuzi zilizokabidhiwa kwake na Tume ya Uchaguzi kama inavyotakiwa na Sheria za Uchaguzi.

2. Wao walidai mahakamani kwa kiapo kwamba walienda kuapa ubunge kwa baraka za chama na walimtaja Katibu Mkuu kuwa alijaza fomu zao za uteuzi.

3. Tulisema hadharani kwamba walikiuka maagizo ya Kamati Kuu kutoutambua uchafuzi mkuu na matokeo yake, huku wengi wao wakiwa wajumbe wa Kamati Kuu na viongozi waandamizi wa chama. Wao walidai hawakufanya kosa lolote kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama.

4. Dhana ya wao kuomba msamaha ina matatizo makubwa kimantiki. Baada ya kuwafukuza uanachama walikimbilia mahakamani kwa madai kwamba tumewakosea. Na wameendelea kudai hivyo hata baada ya Mahakama Kuu kuamua kwamba Kamati Kuu haikukosea kuwafukuza, na wamekata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu.

5. Wakati wa maridhiano, mojawapo ya madai yetu ilikuwa ni kuondolewa kwao Bungeni na wakati fulani tuliambiwa kwamba Samia amekubali kuwaondoa. Hilo halikutokea. Na halikutokea kwa sababu Samia na CCM haijawahi kukubali kuondolewa kwao Bungeni.

Soma Pia: Halima Mdee kushawishi Covid-19 kurudi CHADEMA, je Wasamehewe na Chama au Wananchi?

6. Kumekuwa na kampeni kubwa ya kichini chini, ndani na nje ya chama, ya kuwarudisha wasaliti hawa kwenye chama. Mimi siamini kwamba kampeni hii ina maslahi yoyote ya chama. Ninaamini kwamba wanataka au wanatakiwa warudi ili waweze au wawezeshwe kugombea Ubunge mwaka ujao. Mark my words.

7. Kama tunataka warudi, haiwezi ikawa ni kwa sababu sio wasaliti na hawakukosea. Itakuwa ni kwa sababu hatuna tena nguvu au ujasiri wa kupambana na watu wa aina hii.
Lisu ndani ya Chadema Hana nguvu kabisa Hana uwezo wenyewe wakuamua warudi
Atabaki tu anapiga miayo tu na watarudi tuTundu Lisu atake au asitake
 
Lissu aache ujinga. Kama anaona Mbowe anakosea ahame chama. Hicho chama ni mali ya mtu binafsi (Mbowe) kwahiyo Lissu aache kuweka pua yake kwenye mali za watu.
 
Tuliwaonya kuwa laana ya kushangilia kifo cha Magufuli ni kubwa.

Baada ya miaka 3 mnayo hiyo amani mliyosema mtapata? Hamtekwi tena? Hamshindwi tena kwenye chaguzi? Watu hawakimbii chama chenu tena?

Na laana iwatafune milele nyumbu nyie
Akili gani hizi, kama walifanya makosa kwa Lowasa kwa hiyo waendelee?
 
Tuliwaonya kuwa laana ya kushangilia kifo cha Magufuli ni kubwa.

Baada ya miaka 3 mnayo hiyo amani mliyosema mtapata? Hamtekwi tena? Hamshindwi tena kwenye chaguzi? Watu hawakimbii chama chenu tena?

Na laana iwatafune milele nyumbu nyie
Jiwe yule alikuwa jambazi na gaidi mkubwa sana! Yuko wapi Ben Saa8 na wengine?
 
Anaandika Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti Chadema kuhusu Covid 19

Kama wanaruhusiwa kurudi itakuwa ni kwa sababu hawakuwa na makosa yoyote, ila sisi ndio tuliowakosea. Kama tukiwaruhusu kurudi maana yake ni kwamba sisi viongozi wa chama wote tulikuwa waongo, ila wao ndio walikuwa wa kweli.

Kumbukeni tuliyoyasema hadharani na kwenye vikao vya chama; na waliyoyasema wao hadharani na mahakamani kwa kiapo:

1. Sisi tulisema Kamati Kuu haikuwateua wao, na wala haikuteua Mgombea yeyote wa viti maalum na Katibu Mkuu wetu hakuwahi kujaza fomu za uteuzi zilizokabidhiwa kwake na Tume ya Uchaguzi kama inavyotakiwa na Sheria za Uchaguzi.

2. Wao walidai mahakamani kwa kiapo kwamba walienda kuapa ubunge kwa baraka za chama na walimtaja Katibu Mkuu kuwa alijaza fomu zao za uteuzi.

3. Tulisema hadharani kwamba walikiuka maagizo ya Kamati Kuu kutoutambua uchafuzi mkuu na matokeo yake, huku wengi wao wakiwa wajumbe wa Kamati Kuu na viongozi waandamizi wa chama. Wao walidai hawakufanya kosa lolote kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama.

4. Dhana ya wao kuomba msamaha ina matatizo makubwa kimantiki. Baada ya kuwafukuza uanachama walikimbilia mahakamani kwa madai kwamba tumewakosea. Na wameendelea kudai hivyo hata baada ya Mahakama Kuu kuamua kwamba Kamati Kuu haikukosea kuwafukuza, na wamekata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu.

5. Wakati wa maridhiano, mojawapo ya madai yetu ilikuwa ni kuondolewa kwao Bungeni na wakati fulani tuliambiwa kwamba Samia amekubali kuwaondoa. Hilo halikutokea. Na halikutokea kwa sababu Samia na CCM haijawahi kukubali kuondolewa kwao Bungeni.

Soma Pia: Halima Mdee kushawishi Covid-19 kurudi CHADEMA, je Wasamehewe na Chama au Wananchi?

6. Kumekuwa na kampeni kubwa ya kichini chini, ndani na nje ya chama, ya kuwarudisha wasaliti hawa kwenye chama. Mimi siamini kwamba kampeni hii ina maslahi yoyote ya chama. Ninaamini kwamba wanataka au wanatakiwa warudi ili waweze au wawezeshwe kugombea Ubunge mwaka ujao. Mark my words.

7. Kama tunataka warudi, haiwezi ikawa ni kwa sababu sio wasaliti na hawakukosea. Itakuwa ni kwa sababu hatuna tena nguvu au ujasiri wa kupambana na watu wa aina hii.
kwa hiyo anapingana na mwenyekiti wake, mwinyimkuu a.k.a mangi.
 
Mbona Lowasa alikuja chadema na direct akagombea urais bila kujali aliyoyasema Lisu hadharani kuhusu Lowasa?
Lowasa aliisaliti CHADEMA? LAowasa aliipeleka CHADEMA Mahakamani? Lowasa unamfananisha na COVID 19?
 
Tuliwaonya kuwa laana ya kushangilia kifo cha Magufuli ni kubwa.

Baada ya miaka 3 mnayo hiyo amani mliyosema mtapata? Hamtekwi tena? Hamshindwi tena kwenye chaguzi? Watu hawakimbii chama chenu tena?

Na laana iwatafune milele nyumbu nyie
Hata maccm yalikuwa hamtaki

Nina watu nawajua ni maccm yalisherekea kifo Cha magufuli

Punguza chuki kwa cdm

Ináwezekana cdm Wana .mgogoro Wa ndani lakini mgogoro hao hatuwezi kuhalalisha matendo maovu ya magufuri

Magifufuri alikuwa shetani hakufaa kuitwa mtanzania
 
Kama wataomba msamaha kwa mahandishi na kwa mdomo mbele ya wanachama basi wasamenewe

Lakini wapewe mashariki hawatagombeacheo chochote kwa kipindi Cha miaka 5
Hapo tutawajua ni kina nani walitaka kuiitumia cdm kugombea ubunge

Kusamehe kkunaweza ukakwa kwa aina 2

1. Kutoshitakiwa na chama kwa kutenda jinai
2. Kutokutii maelekezo ya chama

Naunga mkono Kusamehe kwa kuwa tumefindishwa kusamehe kwenye dini zetu
 
Kumleta Lowasa CHADEMA kumewaondolea CHADEMA moral authority ya kusimamia mengi sana.

Japo Lissu ana hoja, Lakini Kama alimpokea na kumnadi Lowasa, mtu ambaye Lissu alimuweka kwenye list of shame kwa makosa mengi (Siyo Richmond tu) anapata wapi moral authority ya kukikemea chama kikiwarudisha akina Mdee?

Ukivunja principle jiandae nayo kukulia denge ikuvunje one day!
 
Mbona Lowasa alikuja chadema na direct akagombea urais bila kujali aliyoyasema Lisu hadharani kuhusu Lowasa?
Hata wewe ulishafanya makosa kwenye familia yako ukasamehewa na hatutakiwi kurudia kosa. Kwahiyo kosa la kumpokea Lowasa pamoja na kuipandisha chati Chadema halitakiwi kurudiwa. Ila kitendo cha akina Halima kwenda tu mahakamani na kukata rufaa kimeshavunja nguvu ya msamaha. Swala lingeishia chamani msamaha ungekuwa na nguvu. Na je ni kweli Mnyika akikubali kuwa alisaini waende bungeni kuapishwa? Basi ndiye aondoke chamani na watu wake Kwa kuwa atakuwa ametenda kosa. Na kama hakuna ushahidi wa wao kiruhusiwa kwenda bungeni washtakiwe na warudishe pesa ya walipakodi.
 
Back
Top Bottom