Anachofanya huyu mchumba wa rafiki yangu ni sahihi?

Anachofanya huyu mchumba wa rafiki yangu ni sahihi?

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Labda mimi ndo nina mtazamo hasi, huyu rafiki yangu Nakaa naye ghetto moja, Ingawa vyumba tofauti, Ana mchumba wake aliemaliza chuo Mwaka huu, huyu kidume ameajiriwa, ni mwalimu wa sekondari.

Kiukweli huyu jamaa anampenda sana huyu mdada, na ana malengo na huyu mdada, na ashamtambulisha huyu mdada hadi kwao..hata nikiwa na huyu mshkaji, msela anasema alitumia miaka miwili hadi kumpata huyu mdada, na anamsifia sana huyu mdada.

KINACHONISHANGAZA:
Mdada amemaliza chuo hajaajiriwa, ila kila mara akija ghetto kwa huyu mwanaume, mwanaume ndo ataosha vyombo, atapika, atafanya usafi, mdada hagusi chochote, hata kumsaidia jamaa kupika, yani mdada akija ghetto analiwa mzigo, hela anapewa, chakula anapikiwa Wanakula, halafu huyoo mdada anasepa.

Yani mwanamke unakuja kwa boyfriend aliekutambulisha kwao, mko kwenye uhusiano wa mda mrefu, tena unaonukia ndoa siku zijazo, unashindwa Walau hata kusaidia kupiga deki ghetto la Mwanaume wako, au kumpikia???? Sasa najiuliza.

1) Huyu mdada ni mvivu?
2)Hapendi kupika? Hajui kupika?
3) Anamchukulia jamaa kama mwanaume wa kupita??

Nauliza hivi kwasababu baadae hata mm yanaweza kunikuta yanayomkuta huyu jamaa hlf nisijue maamuzi ya kufanya.

Wenye uzoefu na hili mnipe mawazo yenu.
 
Seat ya mbele

Sema nini....io stage ya kupenda huwa ipo na huwa haina matokeo mazuri mwishoni

Nlikaribiaga kuwa chizi dem nlomkubali sana alipozinguaaa

Sasa ndo nayoyaona apo
 
Hapo ushaur wangu Ni ufuate ya kwako bro, ya wengne waachie wao wanajuana..Kama unaogopa yatakukuta Ina maana ww Ni kdume bkra had muda huu unapost
 
Hilo halishangazi.

Kuna jamaa yangu alikuwa na mwanamke, alimpenda mpaka akawa ndondocha.

Imagine, mwanamke anaenda kujisaidia. Akishamaliza, anamuambia 'baby njoo nitawaze'.
Jamaa anaenda, anamtawaza alafu anaflash mzigo. 😂😂😂

Kisa nini, demu kaweka mikucha mirefu, hivyo hataki kuchafua kucha zake.

Jamaa aliponiomba ushauri, nikamuambia endelea naye. Ipo siku utaambiwa unyonye nya.

Baada ya jamaa kumkoromea, mwanamke akakata kucha zote. Anafanya usafi, anapika na kufua. Usista duu kule.
 
Back
Top Bottom