Anachofanya huyu mchumba wa rafiki yangu ni sahihi?


Huyo mwanao yatamtokea puani muda si mrefu. Ila usiingilie mahusiano yao mzee baba, tulia zako ila akija mchumba wako afanye uyapendayo akufanyie na pia umpende tu. Huenda kupitia namna unavyokaa na mpenzi wako anaweza kuona kitu cha tofauti.

La mwisho.
Ni makosa sana kumfukuzia demu kwa miaka mingi sijui miaka miwili unafukuzia mwanamke. Utakuja kubebeshwa zigo la mavi ukijua ni Viazi.
 
Dizaini jamaa ana force mapenzi anatumia nguvu nyingi kumridhisha manzi wake ambae hana nia ya dhati na yeye
 
Wapenda slope hawa....

Wanataka wahudumiwe kama wameoa inawezekanaje!!!
 
Ni makosa sana kumfukuzia demu kwa miaka mingi sijui miaka miwili unafukuzia mwanamke. Utakuja kubebeshwa zigo la mavi ukijua ni Viazi.

Huu ndio ukweli mchungu na ndio tatizo lilipoanzia. Japo wadau humu wamekazania kumwambia mtoa mada afatilie mambo yake wakati sote tupo MMU kufuatilia matukio kama hayo yanayowatokea watu na kuelimishana.

Sawa asiingilie mahusiano ya watu, lakini ajifunze kutokana nayo.
 

Ujue kama mwanamke anakubania anaweza kubana kwa miezi tu ila baadae akaachia mkawa kwenye mahusiano. Lakini mwanamke eti unamfukuzia kwa miaka miwili unafukuziaga tu, seriously?? Mwanamke ukiyemfukuzia miaka miwili anakataa ujue ana mtu anayempenda na ndio anampa Jeuri Kwahiyo inabidi ujiongeze uchape raba. Jkute anakuonea huruma kukuchana ukweli au akisema anaona ataharibu mitego yake aliyonayo.
Huyo huyo demu baadae akarudi akavunga anakutext tu ukajua yumoo, basi nawewe ukajiona hatimaye mtoto kaingia kwenye 18..! Kumbe huko Katendwa karudi kwako baada ya kuvurugwa na msongobereko ya wana na anaweza asije yeye kama yeye. Hawa wanarudigi either wamempiga Mimba au wamemtenda. Wahuni sio watu.
 
Sioni shida yeyote kwa maana hata mkifanyiwa mnatuchukulia sisi ni hivyoo .
Hamna shukurani yule dada anafanya hivyo ili hata wakiachana kisimuume alikuwa anamuhudumia kwa kila kitu
 
Ingilia ya watu yatakutokea puani! Ndugu mapenzi mengine yaache kama yalivyo we ingilia tu uje uone yanavyokuzonga utaonekana Bata..[emoji23]

Yani nsingeona reply yako sijui ingekuaje
 
Pilipili usiyoila inakuwasha vipi?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Kwangu mm naona haiko sawa, japo story haijakuwa na mawanda mapana yakuweza kuona na kuyajua hasa makubaliano kati ya rafiki yako na mpenzi wake,

Kwa picha ya juu juu tu, naweza kusema bi dada yupo kwaajili ya kitu tu (hasa pesa), na bad enough ameshajua kuwa anapendwa sana, so ame take love ya rafiki yako just for granted,

Sasa nn kifanyike, hebu jaribu kuongea na rafiki yako, hasa kujua makubaliano yao wao wawili na kama rafiki yako anaridhika na hiyo hali,

Ukishapata hizo data hebu njoo na andiko lingine lenye kutoa taswira pana ya mahusiano elezwa hapo juu.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…