Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Broda leo unageuka unakuwa wakili wa watendaji wabovu wa serikalini kama walituibia gizani wacha waumbuke mwangani
 

Yes their immunities should be waived if there is evidence of their complicity in economic sabotage and financial crimes. In this way we shall honour Baba wa Taifa and also instil discipline in public service.
 
tena majaliwa angetakiwa atembee na bakora awacharaze hao watumishi hadharani

agustino mrema alitumia mfumo wa kuwapelekesha watumishi jeshi la polisi likanyooka alipokuwa mambo ya ndani

MAJALIWA endelea hivyo hivyo na tena wapigishe na warushe hata kichura chura hao mameneja kama Mohamed Buhari 1978 ALIVYOFANYA NIGERIA
 
Sawa kwasababu tumekuwa na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na sio ufanisi wa kazi
 
Target ni JK now naona
naona wanataka ashindwe hata kuitisha vikao vya kamati kuu...
mambo yote sio mapya...nini kifanyike ndo hawaji nacho...ni ku expose na ku expose tu...

Magufuli amewahi kuagiza ubomoaji zaidi ya mara mbili, Rais na PM wakamzuia kufanya hivyo, Magufuli aliwahi kupambana na watu wa mizani, wanaozidisha uzito, PM akaingilia, Magufuli alikuwa anachukia sana lakini kwa sababu hakuwa na madaraka juu yao alikaa kimya.

Leo ana madaraka, ana expose ubovu wa system, ana expose madudu yaliyofanyika kipindi hicho, ili unaposet system nyingine unakuwa unajua wapi pa kubana kwa sababu mbinu na loopholes zote umezifahamu.

Huwezi tu kuweka system haraka kabla hujajua mbinu zote/nyingi ambazo zinaweza kutumika kukuibia.

Hivyo mpeni muda tu, atafanya kitu.
 
Mkuu Pasco hayo ni maonyesho. PM angeweza kumwita mtu ofisini na kumweleza aliyogundua, kumpa muda wa kujieleza akishindwa chukua hatua. Sio lazima uite waandishi wa habari ili uonekane unafanya kazi.

Ukweli ni kuwa JPM anajua kuwa hakuchaguliwa na watanzania, na anajua watanzania waliikataa CCM sasa ili ku win watu ni lazima afanye hivyo, ili hata wale ambao hawakumpigia kura wamuunge mkono.

Jana nilimhurumia sana alipokuwa anaongea na wafanyabiashara, maneno "naomba mniunge mkono" ameyarudia kama mara 20 hivi na akahitimisha kwa maneno "yalitopita si ndwele tugange yajayo." Anajua aliokuwa anazungumza nao hawakumuunga mkono wala hawakumpigia kura, anajua jinsi alivyoupata huo urais ndiyo maana ni lazima a - plead huruma ya watu.

Harakati za PM ni jitihada hizo hizo za kutaka support ya wananchi. Anyway tuwape muda tuone jinsi watakavyotuvusha kutoka hapa tulipo.
 
Wenyewe siyo wastaarabu kwa uzembe, wizi na Ufisadi wa mali za umma ambazo zi zetu sote wewe na mimi. Sasa unataka wafanyiwe ustaarabu gani zaidi ya kuwaumbua ili wajirekebishe na kutoa somo kwa wengine wenye tabia kama za kwao.
 
ameniuzi sana ,ye hajui hii inchi tunakawaida ya kuvumiliana atuvumilie tule tukichoka tutaacha
 
Kuna watu makopo humu ndani ni kama huyu mtoa uzi upo kama mwanamke ambaye hataki kuolewa kila siku anakuja na hiki mara kile!!hivi sasa tulitaka uongozi wa aina gani????aisee mungu tusamehe kwa hawa wachache waliozoea kuturudisha nyuma wewe Pasco ni zaidi ya mnafiki!!good governance zilikuwepo na kuundwa tume ya uchunguzi matokeo yake yalikuwa nn!!si ndio nyie nyie mlipiga kelele tumechoka na kuundiwa tume!!leo unakuja na kuandika huu upopoma aisee umenipa hasira nataman kukutukana dah mungu anisamehe buree!!
 
Watanganyika wanapenda matukio......tunashangilia matukio. Matukio yakiisha tutaanza kulalamika.
 
Nadhani hapa anazungumziwa Kassim Majaliwa ambaye si Rais wa Tanzania.

Leave Makofuli alone!!

Mkuu Kassim Majaliwa anafanya hayo kwa ridhaa ya nani kama sio Rais ??
 
siku mtu msafi atakapokwenda mahakamani na hukumu kutoka ndio tutajifunza-kama makonda alitakiwa kufunguliwa kesi na jamaa wangeshinda
 
anataka amfunike pinda ili yeye apate sifa na umaarufu zaidi


Kwa akili yako Pinda ni mtu? Angekuwa yeye bandarini angeanza kulia na kuongea porojo tu. Kale kajamaa kalikuwa hasara kwa taifa na hata Kikwete alijuwa na ndiyo maana alimkata mapemaaa kwenye jopo la urais. Nani anataka iongozi anayelia bila kujuwa wajibu wake? Majaliwa na JPM ni kiboko na ndiyo tunaowahitaji hapa Tanzania. Hii nchi ililiwa sana.
 
Kweli watanzania nani katuloga?? Hiyo good governance ndio imetufikisha hapa tulipo kama vip hama nchi Pasco. Hapa kazi tu!
 
Wao wameshindwa hiyo good governance, wanaitaka ya nini tena? Majaliwa endelea!
 
Waziri mkuu hawezi kutembelea Ofisi zote za serikali nchini. Hivyo public punishment ni ujumbe tosha kwa ofis nyingine za serikali kufanya kazi bila mzaha.
 
 
Pasco unaijua karma lakini hapa hukupaangalia kwanini?

Kama ulifanya makosa unaijua njia ambayo Mungu atakuhukumu? Kama ulidhulumu wananchi na kusingizia kuwa pesa za serikali hayo ndio majibu yake.

Hawa watu Wanastahili hayo yanayowakuta ni wakati wao wa kuona machungu umefika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…