ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,152
- 33,899
Broda leo unageuka unakuwa wakili wa watendaji wabovu wa serikalini kama walituibia gizani wacha waumbuke mwangani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I find emotions in your post.
Are you and can you be rational?
Open up, I believe you are afraid of loosing your lucrative contracts from the present
corrupt leaders of public corporations.
Let Kassim and his boss JPM salvage whatever is salvageable.
MP's should help this new administration by enacting a law to question Presidents, past and present.
Target ni JK now naona
naona wanataka ashindwe hata kuitisha vikao vya kamati kuu...
mambo yote sio mapya...nini kifanyike ndo hawaji nacho...ni ku expose na ku expose tu...
Nadhani hapa anazungumziwa Kassim Majaliwa ambaye si Rais wa Tanzania.
Leave Makofuli alone!!
anataka amfunike pinda ili yeye apate sifa na umaarufu zaidi
Wao wameshindwa hiyo good governance, wanaitaka ya nini tena? Majaliwa endelea!Hayo ni maoni yako ni kwanini unataka uyalazimishe kwa WatanZania wote? Hayo ya utawala bora ni kulingana na tafsiri yako wewe na jinsi unavyoongoza familia nyumbani kwako usitake kutuletea kwenye nchi yetu, tumeshatoka huko, tumeshayafanya yote hayo ya kuitana faragha, kuundiana tume, kuonyana kwamba ninawajua wala rushwa msipojirekebisha mtakiona cha mtema kuni kote huko tumepita lkn matokeo yake ni kwamba makontena zaidi ya 2500 hayajalipiwa kodi, yaani yamekombolewa Bandarini bila kulipiwa sasa huu ni uhujumu Uchumi na kwa nchi nyingine adhabu yake ni sawa na Uhaini kwani unalinganishwa na uuwaji watu wote waliofia mapokezi kwa kukosa dawa hospitalini wameuliwa na hawa wezi!
Hivyo tuache na Magufuli wetu tumeshamkubali jinsi alivyo na vyovyote anavyofanya ana baraka zetu, na ndio maana ya kushinda Uchaguzi na kuwa Raisi vinginevyo basi kila mtu angejiongoza?
Wanabodi,
Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.
Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.
Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.
Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.
Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.
Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.
Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.
Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco