Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Mmmmh yaani mara hii tu mlishaanza kulalamika? Hamtachelewa kusema bora awamu zilizopita maana watanzania hamueleweki, jamaa waliopita mmesema walilegeza sana nchi ikaharibika, amekuja huyu mnaanza kulalamika kakaza sana mtaumia! Mnamtaka nani? Huu ni unafiq.
 
Pasco inaonekana mwili mzima ulikuwa umejaa majipu,Pole sana ndio tiba hiyo
 
Last edited by a moderator:
Namwitaga uncle ruckus. Pangekua na vidonge vya kujigeuza mzungu mjomba angemeza zamani sana.

hahahahahaha mwenyewe anasema Miafrika ndivyo tulivyo... Na hivi wanavyopigwa risasi kila siku jamaa ni kweli angeshajibadilisha rangi..
 

Pasco, leo unajifanya kufahamu good governance? wakati EL anadhalilisha wafanyakazi na wateule wa rais hadharani wewe ulikuwa unshangilia na kusema mtu wa maamuzi magumu. Leo umesahau? hapa nchi ilipofikia tunahitaji viongozi kama hawa JPM na Majaliwa. ngoja watunyoooshe
 
aliyeleta hii mada ni wakala wa mafisadi. anatumia tumbo kufikiri
 
System anayoitumia Mhe. Waziri Mkuu ni nzuri sana.
  1. Inatia matumaini kwa wananchi waliomchagua na ambao hawakumchagua.
  2. Inatoa funzo kwa watendaji wote.
Ni system itakayo leta mabadiliko ya kweli. Mhe. Mwalimu J. K. Nyerere alisema "mfichaficha maradhi kilio kitamuumbua" na wengi tunapenda ukweli na uwazi kwenye mambo nyeti ya kitaifa.
 

Vizuri lakini badala ya kumsamehe mpongeze.
 
Wacha waabishwe hivyo hivyo, nao walizidi kufanya mambo watakavyo.
 

Ni sawa kabisa anavofanya coz jamaa walijiachia sana na wameivuruga sana nchi wapendavyo.Acha wafanyiwe tu,haina tofauti ukilinganisha na adha walizotusababishia sisi wanyonge huku chini.
 
PASCO naona kama umechanganyikiwa nchi inahitaji watu kama MAGUFULI NA MAJALIWA Potelea mbali waache wazalilike
 
Hivi mbadala wa dhaifu ni nini watanzania embu tupunguze unafiki
 
Ukikamata sawasawa bandari ikalipa kodi na ushuru wote inavyotakiwa, serikali itapata hela za elimu na matibabu bure na pengine zaidi ya hapo. Muiache timu ifanye kazi kabla ya kuingiza mawaziri kwenye timu.

Tunasubiri tuambiwe makontena 2000 yameikosesha serekali kiasi gani.
 
Pasco, unachoover look kuwa lile karatasi analokuja nalo limeandaliwa na wafanyakazi wa hapo hapo. Na kwenye karatasi husika kuna notice zinazoenyesha namna anayeulizwa swali alivyoshiriki katika mchakato huo halamu. So ngoja tusubirie tuone mwisho wake.
 

Yaani inasikitisha, trl waakopa kuja kulipa mshahara, serious? watu kama hawa ni kufukuza tuuuu
 
Ndugu Pasco unataka kupotosha kupitia andiko lako. Nadhani ulipaswa kudurusu ili ujikumbushe au uongeze uelewa wako juu ya misingi ya utawala bora. kwa kukusaidia tu miongoni mwa misingi ya utawala bora ni pamoja na UWAJIBIKAJI na UTII WA SHERIA. Mh. Waziri Mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali anachofanya sasa hivi sio tu kwamba anatimiza majukumu ya wadhifa wake lakini pia anatii sheria iliyompa majukumu hayo. Unapopewa majukumu kwenye idara au taasisi yoyote lazima upewe nyenzo/nguvu za kuteleleza majukumu hayo. Nyenzo/nguvu hizo lazima zitokane na sheria. Kwa hiyo usishangae na kuanza kupiga mayowe kupinga anayoyafanya Mh. Waziri Mkuu.

Kwani hao unaosema wanaaibishwa na kudhalilishwa wamevuliwa nguo hadharani na kuachwa utupu au wamekaguliwa kwenye maeneo yao ya kazi ambazo hulipwa mishahara ili wafanye kazi hizo? Wewe kwa mtazamo wako unataka badala ya wao kulipwa mishahara kwa ajili kufanya kazi walizoelekezwa na serikali, wapokee mishahara hiyo ili kupotezea serikali mapato yake ambayo wewe na mimi ndiyo tunayategemea kwa ajili ya kuona serikali inaboresha afya, mabarabara, n.k? Mimi ningependa Mh. Waziri Mkuu atembee na viboko akibaini uovu kwanza muhusika atandikwe viboko 12 hatua nyengine zifuate hadi hapo watendaji wa serikali watakapotambua kutimiza wajibu wao bila kusukumwa.
 

Wao si walisema hata kama wakiweka maiti au jiwe UKAWA wataichagua tu na kuikubali!
Na sisi watuachie Magufuli wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…