Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Mmmmh yaani mara hii tu mlishaanza kulalamika? Hamtachelewa kusema bora awamu zilizopita maana watanzania hamueleweki, jamaa waliopita mmesema walilegeza sana nchi ikaharibika, amekuja huyu mnaanza kulalamika kakaza sana mtaumia! Mnamtaka nani? Huu ni unafiq.
 
Pasco inaonekana mwili mzima ulikuwa umejaa majipu,Pole sana ndio tiba hiyo
 
Last edited by a moderator:
Namwitaga uncle ruckus. Pangekua na vidonge vya kujigeuza mzungu mjomba angemeza zamani sana.

hahahahahaha mwenyewe anasema Miafrika ndivyo tulivyo... Na hivi wanavyopigwa risasi kila siku jamaa ni kweli angeshajibadilisha rangi..
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco

Pasco, leo unajifanya kufahamu good governance? wakati EL anadhalilisha wafanyakazi na wateule wa rais hadharani wewe ulikuwa unshangilia na kusema mtu wa maamuzi magumu. Leo umesahau? hapa nchi ilipofikia tunahitaji viongozi kama hawa JPM na Majaliwa. ngoja watunyoooshe
 
aliyeleta hii mada ni wakala wa mafisadi. anatumia tumbo kufikiri
 
System anayoitumia Mhe. Waziri Mkuu ni nzuri sana.
  1. Inatia matumaini kwa wananchi waliomchagua na ambao hawakumchagua.
  2. Inatoa funzo kwa watendaji wote.
Ni system itakayo leta mabadiliko ya kweli. Mhe. Mwalimu J. K. Nyerere alisema "mfichaficha maradhi kilio kitamuumbua" na wengi tunapenda ukweli na uwazi kwenye mambo nyeti ya kitaifa.
 
Kwa kweli kwa hali tuliyonayo, mimi namsamehe Waziri mkuu. ndhani lengo la kufanya hivi ni kutoa ujumbe kwa wakuu wote wa mashirika na idara, kwamba wawe makini. waelewe details za mambo yanavyokwenda katika maeneo yao. tunatoka katika mfumo wa ulegelege, na tunapenda kuwa katika mfumo wa kuchapa kazi. sasa tunakwendaje? kama akifanya "kikao cha management" kama unavyosema, itabidi wapite mashirika yote kufanya hayo hayo. lakini hii wanayofanya ni sawa na kwenye gwaride afande ananyoosha mstari kwa kutumia risasi. atafanya hivyo mara moja tu. mara nyingine risasi haitampata mtu! kila mtu atajipanga usawa kulia na mstari utanyooka nyuzi tisini ndani ya sekunde tu. tuna matatizo mengi sana kwa hiyo tukubali maumivu ya operesheni na kuuguza majeraha ya upasuaji. lengo letu ni kupona

Vizuri lakini badala ya kumsamehe mpongeze.
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco

Ni sawa kabisa anavofanya coz jamaa walijiachia sana na wameivuruga sana nchi wapendavyo.Acha wafanyiwe tu,haina tofauti ukilinganisha na adha walizotusababishia sisi wanyonge huku chini.
 
PASCO naona kama umechanganyikiwa nchi inahitaji watu kama MAGUFULI NA MAJALIWA Potelea mbali waache wazalilike
 
Hivi mbadala wa dhaifu ni nini watanzania embu tupunguze unafiki
 
Ukikamata sawasawa bandari ikalipa kodi na ushuru wote inavyotakiwa, serikali itapata hela za elimu na matibabu bure na pengine zaidi ya hapo. Muiache timu ifanye kazi kabla ya kuingiza mawaziri kwenye timu.

Tunasubiri tuambiwe makontena 2000 yameikosesha serekali kiasi gani.
 
Pasco, unachoover look kuwa lile karatasi analokuja nalo limeandaliwa na wafanyakazi wa hapo hapo. Na kwenye karatasi husika kuna notice zinazoenyesha namna anayeulizwa swali alivyoshiriki katika mchakato huo halamu. So ngoja tusubirie tuone mwisho wake.
 
Na wewe naye

Umekumbuka maisha ya ndoa leo kumekucha, hii ni kwamba vijibahasha haviji.

Wengi michepuko hawana muda nao pesa hakuna na wanaishia kukumbuka nina mke na nimwekee heshima leo nimtaje ajulukane maana michepuko yote imeyoyoma

Yaani ni shida haswa, pole nimekuwa nikiona nguvu yako ya kumponda muheshimiwa na makamu ila umekuwa kama unapewa pembeni kuja kuchafua.

Pole yenu na hao wawili humu na wale wachache

Sie furaha, hadi huku Tand./Mbaga. tunasherekea

Wakiulizwa wanauma meno, y kuwapa muda. Eeh waunde bodi sijui nini hakuna hiyo wakiona vipi waache kazi.

Yaani inasikitisha, trl waakopa kuja kulipa mshahara, serious? watu kama hawa ni kufukuza tuuuu
 
Ndugu Pasco unataka kupotosha kupitia andiko lako. Nadhani ulipaswa kudurusu ili ujikumbushe au uongeze uelewa wako juu ya misingi ya utawala bora. kwa kukusaidia tu miongoni mwa misingi ya utawala bora ni pamoja na UWAJIBIKAJI na UTII WA SHERIA. Mh. Waziri Mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali anachofanya sasa hivi sio tu kwamba anatimiza majukumu ya wadhifa wake lakini pia anatii sheria iliyompa majukumu hayo. Unapopewa majukumu kwenye idara au taasisi yoyote lazima upewe nyenzo/nguvu za kuteleleza majukumu hayo. Nyenzo/nguvu hizo lazima zitokane na sheria. Kwa hiyo usishangae na kuanza kupiga mayowe kupinga anayoyafanya Mh. Waziri Mkuu.

Kwani hao unaosema wanaaibishwa na kudhalilishwa wamevuliwa nguo hadharani na kuachwa utupu au wamekaguliwa kwenye maeneo yao ya kazi ambazo hulipwa mishahara ili wafanye kazi hizo? Wewe kwa mtazamo wako unataka badala ya wao kulipwa mishahara kwa ajili kufanya kazi walizoelekezwa na serikali, wapokee mishahara hiyo ili kupotezea serikali mapato yake ambayo wewe na mimi ndiyo tunayategemea kwa ajili ya kuona serikali inaboresha afya, mabarabara, n.k? Mimi ningependa Mh. Waziri Mkuu atembee na viboko akibaini uovu kwanza muhusika atandikwe viboko 12 hatua nyengine zifuate hadi hapo watendaji wa serikali watakapotambua kutimiza wajibu wao bila kusukumwa.
 
Hayo ni maoni yako ni kwanini unataka uyalazimishe kwa WatanZania wote? Hayo ya utawala bora ni kulingana na tafsiri yako wewe na jinsi unavyoongoza familia nyumbani kwako usitake kutuletea kwenye nchi yetu, tumeshatoka huko, tumeshayafanya yote hayo ya kuitana faragha, kuundiana tume, kuonyana kwamba ninawajua wala rushwa msipojirekebisha mtakiona cha mtema kuni kote huko tumepita lkn matokeo yake ni kwamba makontena zaidi ya 2500 hayajalipiwa kodi, yaani yamekombolewa Bandarini bila kulipiwa sasa huu ni uhujumu Uchumi na kwa nchi nyingine adhabu yake ni sawa na Uhaini kwani unalinganishwa na uuwaji watu wote waliofia mapokezi kwa kukosa dawa hospitalini wameuliwa na hawa wezi!

Hivyo tuache na Magufuli wetu tumeshamkubali jinsi alivyo na vyovyote anavyofanya ana baraka zetu, na ndio maana ya kushinda Uchaguzi na kuwa Raisi vinginevyo basi kila mtu angejiongoza?

Wao si walisema hata kama wakiweka maiti au jiwe UKAWA wataichagua tu na kuikubali!
Na sisi watuachie Magufuli wetu
 
Back
Top Bottom