Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Pia ili kupunguza fujo, nishauri waandishi wa habari wasiwe wanaingia ndani kufanya LIVE coverage ya mazungumzo kati ya viongozi na waajiri. Litakuwa ni jambo la afya sana kama taarifa tu ya yale yaliyojiri au maamuzi ya yale yaliyoamriwa itatolewa na baadaye.

Marekebisho hayo yakifanyika tutakwenda vizuri.
 

Wewe kiazi kweli... Mijitu haina huruma hata chembe why do you want to spare them... Want on wezi hadharani
 
Tena wana bahati,hapa wanamulikwa na kamera za wapiga picha wa TV ,ingekuwa China hao wasakuwa historia,kwa kiongozi msafi kwanini ushindwe kusema ukweli hadharani hadi utake ukae chemba ,kwa kufnya hivyo wengine wataacha kufanya madhambi,nakumbuka wakati tukikua ukiwa kikojozi ulikuwa unaimbwa hadharani,kikojozii,kikojozii ,baada ya kuimbwa kesho yake hurudii kukojoa,dawa ya wala rushwa ni kuwa-shame hadharani tu baasi.mbona Dr Slaa alifanya hivyo Mwembechai na hatukusikia hizi ngonjera za utawala wa haki na sheria?
 
we need serious people and hardworkers
kama mbabaishaji for sure utatolewa
kama ushawahi kuwa kiongozi hata shuleni na ukawa kweli unafanya kazi huwezi kushangaa usimamizi wao hawa jamaa
UKWELI NI KWAMBA WATANZANIA WENGI WAMEBWETEKA SAANA MPAKA KERO AND KILA SIKU WANATAKA WAKIWA WANAENDA KIJIJINI KWAO WAPITE BARABARA YA LAMI HOW?????????

YOU MUST BE SERIOUS
FANYA KAZI KWA MANUFAA YA UMMA NA SIO TUMBO LAKO
CHEO NI DHAMANA......

#HapaKaziTu
 
Mkuu Pasco hatukuelewi unachosema hawa unaona wanadhalilishwa mbele ya kadamnasi tunajuwa wana haki zao ila Waziri Mkuu kaenda alichukuwa vyombo vya habari kwa sababu alikuwa anajuwa watasema uongo kuficha madudu yao,kwa hiyo ili kupata ushahidi wa walivyo waongo ndiyo maana alienda na kamera,usisahau pia kwa mujibu wa katiba wananchi tuna haki ya kupata habari,huko Uingereza unakosema matukio mengi huwa yanarushwa moja kwa moja na vituo vyao vya televisheni.
kwa sasa utatusamehe tumwache Dr JPM afanye vituvyake tupo vitani na vita havina macho.
 

Kama Waziri Mkuu kakosea, ashitakiwe.

Tuambiwe kavunja sheria ipi, apelekwe mahakamani, walioonewa waje hapa kutoa data zao, kama hawana fedha za kuendesha kesi tutawasaidia.

Sio mtu analaumu "mtindo" bila kuongelea sheria.

Mimi nilivyo m blast rais Magufuli kuingilia tafrija ya bunge, niliongelea "checks and balances" za kutoka katika katiba.

Pasco anapom critique PM, atupe msingi wa kisheria.

Kama hana msingi wa kisheria, asimlaumu PM. Ampigie simu mbunge wake sheria ibadilishwe.
 
Last edited by a moderator:
Hapa naona tipic imepamba moto wezi na wasio wezi wameumana.
 
Tuko pabayo mno my brother. To hell with good governance , let people realize that the govt can act?
 
Labda PASCO atuambie.

Je Tatizo ni PM kuuliza aliyoyauliza hadharani tena mbele ya media au ni kitu gani?, Je amevunja sheria ipi ya Uongozi bora kwa kufanya hivyo?.

Pili je PM kwenda na ushahidi na kutaka kufanya authentication ya taarifa kavunja sheria gani ya utawala bora?, Je PM hana mamlaka ya kuhoji hadharani juu ya mambo ya kila siku ya nchi?.

Hii nchi imeendeshwa kimazoea kwa muda mrefu sana, tunahitaji hii kasi ya PM kuweka mambo sawa.

Nchi kama ya China they dont care wewe ni nani na ulikuwa na cheo gani, Ukizingua unapigwa pingu Laivu mbeleya state TV na Ikibidi kupigwa shaba unapigwa shaba na nchi inasonga. Sembuse hii ya kupigwa maswali mfululukizo ndo mnatafsiri kuwa siyo good governance!, Laiti yule mtu wa TPA angepigwa kibao hapo kidooooogo ungetuconvince ndugu Pasco, lakini kuulizwa maswali tu ndo umetishika hivi!, Calm down brother Hapa Kazi tu!

Tena napendekeza ianzishwe Kampeni katika media ya kudharau tabia za ukwepaji kodi na Ufisadi, yatengenezwe matangazo ya redio na TV ya kuonyesha kuwa Ukwepaji kodi na Ufisadi ni tabia mbaya, za kufedhehesha, za Kutostaarabika, za aibu, za kupigwa vita!. tukifanya hivi umma utakaa ktk msitari
 
Serikali soon itakuwa mhanga wa kwenda kizimbani mara kwa mara jinsi inavyokwenda na zoezi lakutumbua majipu.

Serikali ina nia nzuri na ya dhati kabisa ila ktk kutumbua majpu inabidi iende kulingana na taratibu, sheria, maadili ya utawala bora.

No one is above the law - so tuiunge mkono serikali ktk harakati za maendeleo ila yawapasa wasimamiaji wa sheria kuishauri serikali pale inapobidi.
 
Utawala wa sheria kwa wavunja sheria, lazima kuwe na transparaency; tujuzwe nani kafanya vizuri au vibaya, wapi na wakati gani.

Rule of law bila transparent na kuwa hold wahusika accountable ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
 
Pasco good governance inakwenda na uwajibikaji. Ukitaka uheshimiwe timiza wajibu wako.Rushwa,ufisadi, kutowajibika, utoro kazini na kujiona miungu watu kwenye sehemu za kazi yamekuwa matatizo sugu ambayo yanahitaji mchakamchaka kwenye maamuzi. Rais Magufuli alishatahadharisha huwezi kuendana na kasi hiyo achia ngazi.
 

Ndugu Pasco,

Kinachofanyika kwa sasa ni sawa. Tanzania ilipofika kwa sasa, hatua za waziri mkuu ni sahihi.

Watendaji wa Umma ndio wazalilishaji wakubwa wa mama zetu wajawazito na maskini. Mtu mmoja anamiliki nyumba 73 wakati fedha hizi zingeweza kutatua changamoto za umaskini kwa asilimia kubwa.

Ukitaka maendeleo, suala la haki za binadamu weka pembeni kwanza. Nchini China hii imekua ni moja ya approach yao kuelekea kwenye maendeleo yao. Huwezi ukaiga Umarekani hapa Tanzania halafu ukapiga hatua ya maendeleo.

Go Majaliwa go
 

muhimu mtoa mada ukafahamu hii nchi ilikaribia kupoteza mwelekeo kwa uozo!! hapa tulipifika inabidi watu walio misuse offices and public funds wajitambue kwamba walilikosea taifa hili kabla hata huwajapata muda wakujipanga ili wazidi kuturostisha!! hawa hata mahakamani watakushinda mana wana watu wao kule sababu ya fedha walituibia miaka nenda miaka rudi!! so ndo mana mtoto ikiwa kikojozi alikuwa anapitishwa mtaa huku anaimbiwa ili aone aibu ya alikifanya then hajikojelei tena simply coz of that ambarrassment he went throu!! sheria baadae baada ya kuweka level ground!! nchi imeharibika hii inahitaji major overhaul!!
 
Huyu pasco ana moja ya sifa zifauatazo au zote;
1. Ni mwizi
2. Ana element za ukichaa
3. Sio raia wa Tanzania
4. Kinachowndelea serikalini hakielewi
5. Mamlaka ya serikali hayatambui
6. Alichokiandika hakitambui
7. Upeo wake wa kufikiri ni wa mashaka mashaka
8. Ni mnufaika wa wizi unaoibuliwa
9. Ni mshirikia katika wizi unaoibuliwa
10. Anatumika kusambaza propaganda
 

MKUU KIRANGA
I entire agree with you
 
Last edited by a moderator:
Pasco I support u.. akili ndogo tu ndio haiwez kukuelewa.
 
Last edited by a moderator:
pasco i support u.. Akili ndogo tu ndio haiwez kukuelewa.

wewe na pasco..tunajua tangia mwanzo mko against magufuri.mko tayari kuona majizi yanaiba hamkemei lakini wao wakiulizwa kwa makosa yao mnaona wamevunjiwa heshima.wakati wanaiba pesa za watanzania mbona walikuwa wanatanua na kutudharau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…