Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Ufatilii mambo kazi yako ni kudandia treni kwa mbele tu.

Mara ya kwanza alivyoenda bandarini alikuwa hana tatizo na bandari....bali alikuwa na ishu na TRA na data zilikuwa za mwezi june hadi novemba.

Leo ameenda kutoa data za mwezi june hadi octoba za mwaka 2014 na zinahusu bandari. Ishu ni kwamba data zinaonyesha makontena yamefika bandarini...ila bandari haina rekodi ya kupokea makontena hayo.

Hivyo unaweza kuona hizo ni cases mbili tofauti na kwa taasisi mbili tofauti.

mkuu wanaelewa ila wamejitoa fahamu wazi kabisa.
 
Pasco anatuludisha zama za kuunda Tume.Tuliompa kura Magufuli Tunataka serikali yake iongeze kibano...

Wengi wanaokerwa na speed ya MAGUFULI ..ni wale ambao hawajampa kura Magufuli.. mtuachie Magufuli wetu na majaliwa wetu wapige kazi..tuliwapa kura wenyewe

nakuomba Magufuli utembelee na shirika la Bima la Taifa..huku nako majanga matupu
 
Last edited by a moderator:
Pasco usihofu, hiyo inaitwa "UKIJIFANYA BISHOO MIE NAKUWA BISHOO ZAIDI YAKO", hao watendaji ni wahuni hivyo dawa yao ni kwenda nao kihuni hivyo hivyo kutokana na kula mpaka ukoko
 
Last edited by a moderator:
Gombea basi urais usaidie taifa kwa kutumia hiyo blue print yako. Wewe kalisha tu kalio lako hapo na uache wanaume walio thubutu waongoze nchi. Wewe ambae hata kugombea ujumbe wa nyumba 10 huwezi unakuja kutueleza nini kuhusu taifa!? Bora hata Rungwe alithubutu kugombea urais, anaweza akaongea kitu tukamuelewa. Sio wewe coward.

ha ha ha naona umeamua kuua mende na nyundo mpaka kieleweke
 
Tena utulie kabisa,awamu za unafiki zilishapita sasa kazikazi,si mambo yakifanyika chini ya kapeti mnalalamika kwamba serikali dhaifu haifanyi kazi sasa ndio utulie tena waziri mkuu alikuwa polite sana nadhani huu mwanzo tu
 
Wacha wachachafye, pale bandirini kunahitaji kasi hiyo. Lengo lake ni kutuma ujumbe kwa taasisi nyingine. Watu tuache kufanya kazi kwa mazoea
 
Pasco sikuelewi. Watanzania tumeaibishwa na kudhalilishwa sana kwa kukosa huduma kutokana na tuliowapa dhamana kukusanya kodi kuwa manyang'au.Mama na dada zetu wanateseka wakati wa kujifungua,wagonjwa hawapati huduma,wanapiga mbavu chini,wanavyuo hawapati mkopo,kipindupindu nchi nzima kwa kukosa maji safi na salama,hakuna madawati mashuleni nk. Pasco wewe bado unataka TRA , TPA wabembelezwe,waombwe kistaarabu!! Wacha wsisome namba
 
Last edited by a moderator:
Ngabu iko very clear hawana 'blue print' ya nini wafanye
kubadili hii nchi iondokane na kero
so wanashiriki ku expose kero na kukaripia on tv
lakini 'what to do to change things permanently' ndio hawajui...
'the blue print' ya ku replace hii failed system hawana

Halafu, hao wote si walikuwa kwenye serikali iliyopita?

Manake wanachofanya sasa ni kama kuivua nguo hiyo serikali.

Ina maana walikuwa wanatumikia serikali iliyokuwa imefeli?
 
Mimi naona poa tu kwani haya mambo ya kuoneana haya ndiyo yaliyotufisha hapa.
 
Kwakweli alie andika huu uzi ni wakumlaani kabisa tulipofika sio tu kufukuzana kazi ila piga risasi adharan watu wajuwe kuibia serikali adhabu kifo othewise taifa lita angamia na mwisho wa yote vita. Shime Magufuli na Majaliwa na Mama Samia
 
Si ndiyo sera zenu boss?!!
Nimesikia Magu anatekeleza sera za UKAWA...
 
Tumuache PM akaze buti,mnataka alegeze buti mumuite legelege?wewe ukiweka mambo yako sawa wala huwezi kudhalilishwa,na ukiona huwezi majukumu kwanini ukubali uteuzi?ukikubali uteuzi huku unajua majukumu huyawezi basi kaa mkao wa kutumbuliwa jipu.
 
Halafu, hao wote si walikuwa kwenye serikali iliyopita?

Manake wanachofanya sasa ni kama kuivua nguo hiyo serikali.

Ina maana walikuwa wanatumikia serikali iliyokuwa imefeli?

ulitaka wafanyaje sasa
 
Nakwa kuzingatia mapambano haya niya tamaduni zilozooza lazima nguvu ya ziada itumike. Hii ni tofauti Naya makonda ya kufunga watu rumande bila kuwasikiliza
 
Halafu, hao wote si walikuwa kwenye serikali iliyopita?

Manake wanachofanya sasa ni kama kuivua nguo hiyo serikali.

Ina maana walikuwa wanatumikia serikali iliyokuwa imefeli?


Target ni JK now naona
naona wanataka ashindwe hata kuitisha vikao vya kamati kuu...
mambo yote sio mapya...nini kifanyike ndo hawaji nacho...ni ku expose na ku expose tu...
 
Kama una tuhumiwa kuna umuhimu wa kutoa maelezo mbele ya kadamnasi ili wote wanaohujumu mapato ndani ya serikali wajue kitakachowatokea.
 
watu wafanye kazi kwa weredi na haki, deals sio nzuri tena ; nadhani Mh PM analazimika kufanya ivo ili kuhenga misingi ya uwajibikaji na uaminifu kwa Taifa hili.
 
Mleta uzi nadhani nawewe upo kwenye hizo ofisi za pilato nini? Maana naona umeguswa sana, pole sana, bado sana kuna zaidi ya haya yanakuja. Kuna wazarendo wapo mtaani hanazitaka hizo nafasi, kwa ajili ya kulitumikia taifa lao.
 
Target ni JK now naona
naona wanataka ashindwe hata kuitisha vikao vya kamati kuu...
mambo yote sio mapya...nini kifanyike ndo hawaji nacho...ni ku expose na ku expose tu...

Mtasubiri Milele Kama Wafuasi Wa Kibwetele
 
Back
Top Bottom