“Heshima iliyokuzwa ni ya woga
heshima inayotakiwa iwe ya moyoni.
---
Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.
Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
Mkuu
Mmawia , asante kwa hoja hii ya nidhamu ya woga.
Kuna watu humu hili la nidhamu ya woga ndio wamelijua Leo baada ya kusemwa na Mama Samia.
If you have time, angalia tarehe ya bandiko hili na hoja yake muone sisi wengine tulilisema lini.
Wanabodi, Naendelea na zile mada zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", zikijikita kwenye uzalendo Kwa taifa Letu huku nikisisitiza ukweli na uwazi, ( truthfulness and transparency) ukiwa mkweli na muwazi, , ukweli utakuweka huru!. Hili ni swali, "Jee hizi terorizing ziara za kushtukiza, hakutajenga...
Kwa wavivu wa kufollow links, hapo niliuliza
Wanabodi,
Naendelea na zile mada zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", zikijikita kwenye uzalendo Kwa taifa Letu huku nikisisitiza ukweli na uwazi, ( truthfulness and transparency)
ukiwa mkweli na muwazi,
, ukweli utakuweka huru!. Hili ni swali, "Jee hizi terorizing ziara za kushtukiza, hakutajenga nidhamu ya woga?!. Jee, kutasaidia?!.
Paskali
Hatukuishia Kwa Number 1 tuu,
ila pia niliendesha somo humu namna ya kutofautisha kuongea Kwa ukali na kufoka foka
Wanabodi Declaration of Interest. Mimi Paskali Mayalla, au kwa jina maarufu humu, Pasco wa JF ni Musukuma wa Mujini, aliyezaliwa mujini, kukulia mujini, kusomea mujini na kuishi mujini, ila nature ni ili ile ya Wasukuma, roho nzuri, kupenda sana, ukarimu mwingi, kujituma sana, uchapakazi...
hata number 3, yule Kiranja Mkuu wa viranja pia tuliwahi kumshauri
Wanabodi, Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kassim Majaliwa, sio!. Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomng'oa...
Hata baadhi ya Mawaziri walipokosa utu, akina sisi tuliwasema...
Wanabodi, Hili ni bandiko la swali lilioandama na pongezi kwa viongozi wa awamu ya tano ya " Hapa Kazi Tuu" kwa kuchapa kazi kweli. Kiukweli kabisa hiki kikosi kazi cha serikali hii ya awamu ya 5 chini ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kinachapa kazi, kinafanya kazi nzuri, ya kutuletea...
Na hatukuishia viongozi wakuu na Mawaziri pekee, hata ma RC tuliwamulika
Wanabodi, Tangu baada ya Nyerere, na mtindo ule wa vitendo bila kuchelewa na utoaji wa maamuzi magumu, Watanzania walimisi sana maamuzi ya aina hii kwenye utawala wa Mwinyi, Mkapa na Kikwete, hivyo sasa wanashangilia sana kila maamuzi ya utumbuaji wa majipu wa papo kwa papo ya rais wetu, Dr...
Huyu pia
Wanabodi, Siamini ninachokisikia hapa kwa kiongozi Japo wote tunamasikio inawezekana sio wote tunaweza kusikiliza kitu tukasikia, hivyo kwa faida ya wengine naomba kusema kwa kifupi tuu mimi nilichosikia na kilicho nifanya nipandishe bandiko hili. Kiongozi huyu anasema kibaka akiingia kwako...
Hivyo hili la nidhamu ya woga lilikuwepo sana kwa JPM, lakini twende nyuma na kurudi mbele,
Kwa hali hii, mfano Mama naye ni binadamu, anaweza kukosea, jee akikosea kibinaadamu, kuna kiongozi yoyote ndani ya serikali anaweza kum correct, au kuna any main stream media that would dare criticize or correct her, or the epitome of cowardice inaendelea?!.
Nasisitiza Mama naye she is a human being, anahitaji kusapotiwa, kusaidiwa, kushauriwa, na akikosea akosolewe kistaarabu kwa lugha ya heshima na staha huku akishauriwa the right thing to do, ushauri wangu wa kwanza, ni Tanzania tunaweza kabisa kusonga mbele na kufanya mazuri bila kunyoosheana vidole and calling names kama "Simba wa Yuda".
Nashauri tufanye tuu mambo tofauti bila kumtaja taja Kwa ubaya!
Aachwe Apumzike!.
Jumapili Njema
Paskali.