Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Ipo siku utajua kuwa Kassim Majaliwa si muislam kama unavyodhani.

Uongozi wa Magufuli uko kiuanaharakatiharakati tu
Leo mpiga debe wa Chadema anaanza kumfagilia Magufuli njia na kumsifu.
Teh teh teh.
Njaa kitu kibaya sana.
Wanamme wasio na msimamo km wewe kuolewa Ni fasta sana.

Halafu we km hujafa mpk sasa basi Ebola na ukimwi ni Uongo mtupu.

Sasa Kina Ben saanane imekula kwao. We nani ataendelea kukulipia kodi ya hicho chumba?
Au umehamia Lumbumba Tayari?
Km nakuona hapo na chupi ya kijani kibichi na mabaka ya njano. Suruali mdebwedo. Makalio hiii haaa!

Teh teh teh.

Cc @Ritz @faby
 
Hili lilitokea kwa Mhe. Majaliwa, jana nimeliona tena likitokea Kwa Magufuli, watu wametumbuliwa very unfairly!.

P
yaani kufanya kazi na serikali hii ni kama upo jobless tu............ muda wowote unatupwa huko hivi wanalipwa kweli stahiki zao ? sheria za kazi zinzsemaje kuhusu mambo haya ya sasa
 
Hili lilitokea kwa Mhe. Majaliwa, jana nimeliona tena likitokea Kwa Magufuli, watu wametumbuliwa very unfairly!.

P
Mwalimu aliwahi kuikemea hii tabia ya mtu kufika kazini asubuhi moja halafu anamkuta nyapara anayemwambia tena kwa ukali kuwa "kuanzia leo huna kazi, hivyo rudi nyumbani", bila kujali kuwa mtu huyo ana mke na watoto wanaomtegemea. Sasa Nyapara wetu anayafanya mbele ya wananchi bila kujali miiko ya utawala bora, halafu wanasema ni mfano wa Nyerere, kweli!!!
 
Hili lilitokea kwa Mhe. Majaliwa, jana nimeliona tena likitokea Kwa Magufuli, watu wametumbuliwa very unfairly!.

P
hivi si alisema hapo hadharani kuwa amewasemehe? Au alitudanganya kuwa amewasamehe?
Mimi niko kwenye kuwasamehe, ni nini kiliendelea baada ya kusema amewasamehe halafu baadae tukaskia wametumbuliwa!
Ni kama amewazuga flani hivi kabla ya kwenda kupewa udhaifu wao.!?
Ok, sory kama sijaeleweka kiaina!
 
Uleandika huu uzi ulikuja kichwa kichwa ,,maana ya kuwa kiongozi mahala na kuwaongoza watu ni kutambua yaliyomo katika eneo lako kwa usahihi ,,,,kama wew ni kiongozi shudu na muongo kwanin usiabishwe ule wakati wa fair ndio umepeleka inchi pabaya acha watu wapambane na hali zao wasifuraie tu kuitwa mkuu katika kitengo ila watendee haki vitengo
 
Pascal kubali yaishe utawala huu ni wamambumbu na washamba. Halafu wewe mwananzengo ujue majuto ni mjuu
 
Sasa wewe ndugu yangu Pascal unataka kiongozi kama anaenda against aitwe kisiri asomewe matatizo yake ,,sasa hapo tutakuwa tunajenga nchi au tunambomoa unajua mtu mnapokutana wawili unaweza ukamsamehe maovu yake
 
Sasa wewe ndugu yangu Pascal unataka kiongozi kama anaenda against aitwe kisiri asomewe matatizo yake ,,sasa hapo tutakuwa tunajenga nchi au tunambomoa unajua mtu mnapokutana wawili unaweza ukamsamehe maovu yake
We hufai hata kwa kutafunwa[emoji90] [emoji196]
 
Sasa wewe ndugu yangu Pascal unataka kiongozi kama anaenda against aitwe kisiri asomewe matatizo yake ,,sasa hapo tutakuwa tunajenga nchi au tunambomoa unajua mtu mnapokutana wawili unaweza ukamsamehe maovu yake
No nataka tufuate principles za good government!, huwezi kuwa reprimand the leaders in front of their subordinates wake, huu ni udhalilishaji wa viongozi!.

Waliobaki wanakuwa demoralized, watatekeleza majukumu yao in fear ya public ridicule, hivyo kujenga nidhamu ya woga!.

Paskali
 
Hili lilitokea kwa Mhe. Majaliwa, jana nimeliona tena likitokea Kwa Magufuli, watu wametumbuliwa very unfairly!.

P
Yes hapo ndio amewasamehe, vinginevyo...
fuatilia hii Je inawezekana huu ndio mwisho wa utumbuaji wa papara na ...
Paskali

Pasikali,Mikingamo.....nidhamu na uwajibikaji kazini bila shuruti..............
Asikudanganye mtu..Viongozi wazalendo they all act the same everywhere. ..siasa za kuonehana haya ati suti na Tai nooooo
 
Pasikali,Mikingamo.....nidhamu na uwajibikaji kazini bila shuruti..............
Asikudanganye mtu..Viongozi wazalendo they all act the same everywhere. ..siasa za kuonehana haya ati suti na Tai nooooo
nimetoka kappa
P
 
kwa nini na wao wanashindwa kumuuliza maswali ya kushtukiza? kwa mfano wamuulize ni utaratibu gani uliotumika kumpata anaejenga uwanja wa ndenge wa Chato? au anampango gani na kurudisha nyumba za serikali?
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kassim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomng'oa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huku akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo karatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa Rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makontena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkurugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.

Paskali




My Take:
Tuna tatizo kubwa la uelewa humu, ila pia kufuatia wengi kuchoshwa na kukinaishwa na rushwa na ufisadi, wamekata tamaa na kuhamaniko na mihemuko ya kuchukuliwa hatua kali sana na ikibidi hata wanyongwe!.

Nimenote wengi humu hawakunielewa!, japo nimeanza kwa utangulizi wa kuunga mkono hatua zozote zinazochukuliwa na awamu ya 5 kupiga vita rushwa na ufisadi, siungi mkono the means kwa kutumia populistic approach ya kufanya ili watu waone unafanya!.

Tanzania ni nchi inayofuata mfumo wa haki wa Uingereza, wa presumed innocent until proven guilt beyond reasonable doubt by the court of competant juisdiction!, kinachofanyia ni media trial kumuonyesha mtu ni mkosaji mbele ya camera!.

Sio wengi humu wanaojua kuwa hata mhalifu anahaki!, hata mlaushwa, fisadi, mwizi, pia ana haki!. Hata muuaji aliyehukumiwa kifo kwa kunyongwa naye pia ana haki zake, ananyongwa kwa heshima yake, na kabla hajanyongwa, anaitwa daktari kumpima afya yake, akikutwa na maadhi yoyote, hanyongwi!, bali anatibiwa mpaka apone ndipo adhabu hiyo itekelezwe!.

Japo kisheria hairuhusiwi kamera za waandishi kuingizwa mahakamani, Tanzania tunaingiza kamera mahakamani!, polisi nao wanawaparade wahalifu kwa waandishi wa habari ili hali wako mikononi mwa polisi!, ni kama kuwahukumu kabla!. Kama Kova kila uchao, kwenye screen!, hilo baraza jipya likiishateuliwa, kama kila waziri nae atatembea na media team ili watu waone si itakuwa chaos?!.

Nilichokiona jana anachokifanya PM pia kinakwenda against the principles of Natural Justice
Vita dhidi ya uzembe, rushwa, ufisadi, na ukwepaji kodi yes!, means no!, haki sio tuu itendeke bali pia ionekane kutendeka!.

Paskali
Update.

Mkuu Kiranga, sio kila kitu ni sheria, vingine ni taratibu tuu na kanuni!, ndio maana kwenye ofisi za kizamani kuna vyumba vnawatenganisha ma bosi na wafanyakazi wao!, kuna chumba kinamtenganisha waziri na secretary wake, kuna ofisi ya boss, lengo ya yote hayo ni kuweka heshima na privacy!, nimefanya kazi na wazungu fulani nchini Uswiss, wenzetu wako kwenye full open government initiative, no secrets zozote ofisini, partition zote ni za kioo transparent, computers zote ziko linked kwenye network, desktop zote ni shared, ukipint chochote kuna back copy iko saved, all public communications ni shared.

Huwezi kumrepremand boss infront of his subordinates let alone infront of the media, mtu anaulizwa swali, hajapewa muda wa kujibu, linafuata na lingine na lingine!. Mimi sijasema mafisadi na wala rushwa wasishughulikiwe kikamilifu, nimesisitiza tuu, kuwepo fairness, respect, ustaarabu na sio kutegeana, kuumbuana na kuaibishana!. Wote walioangalia jinsi boss wa TRL alivyokuwa anahojiwa, kiukweli yule bosi amedhaaulika anaonekana ni li bosi lijinga ajabu!, limeshindwa kujibu simple questions kutoka kwa PM, wamekopa kwa idhini ya nani?!, baada ya tukio lile, kweli bosi kama huyu ana any respect left kwa wafanyakazi wake wa chini!, nahisi hata akipita, wananchungulia madirishani na kujisemea kimoyo moyo, angalia lijinga lile linapita!, ni huku tuu Afrika tunafanyiana mambo kama yale ile ni bullying of some kind!.

Paskali
Huyu mayala nayeye sijui haelewi kitu mbona hata Jana kunawatu wametimuliwa kazi kwa kushindwa kujibu huu ndio mfumo was utawala huu sijuwi unamlaumu vp km anza namkuu umlaumu kwanza sisi wenyewe tunafurahia watukufukuzwa tena tunasema kasi ya awamu hii nikali sana mafanikio nimakubwa bidhaa za mkulima kushuka nazamadukani kupanda hayatunaita maendeleo nikiangalia sana naona tumepiga hatua kwakufukuza watu lakini kubadiliaisha bado tukze buti lakini tusishangilie mtu kufukuzwa tushangilie tija yahuyo mtu kufukuzwa
 
..Angalia jinsi Mbunge wa CCM alivyopewa nafasi ya kuzungumza bila kukatizwa-katizwa kwa maswali yenye lengo la kumchonganisha na wapiga kura.

Halafu angalia jinsi Mbunge wa upande wa pili alivyokuwa akitafutwa. utaona kabisa kwamba alikuwa akitafutwa kwa nia ya kumuumbua kwa maswali magumu.

Bahati nzuri Mbunge huyo hakuwepo, kuliko kushiriki ziara isiyo na tija aliamua kuhudhuria vikao vya bunge Dodoma.

Lakini Mwenyekiti wa Halmashauri aliyeongea kwa niaba ya Mbunge alisimama imara na kujibu maswali yote bila kutetereka kiasi kwamba muuliza maswali akakata tamaa.

Kwa maoni yangu, hiki kinachofanyika, is not right, its not good governance!.
P
 
“Heshima iliyokuzwa ni ya woga
heshima inayotakiwa iwe ya moyoni.
---
Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.

Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
Mkuu Mmawia , asante kwa hoja hii ya nidhamu ya woga.

Kuna watu humu hili la nidhamu ya woga ndio wamelijua Leo baada ya kusemwa na Mama Samia.

If you have time, angalia tarehe ya bandiko hili na hoja yake muone sisi wengine tulilisema lini.


Kwa wavivu wa kufollow links, hapo niliuliza
Wanabodi,

Naendelea na zile mada zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", zikijikita kwenye uzalendo Kwa taifa Letu huku nikisisitiza ukweli na uwazi, ( truthfulness and transparency)
ukiwa mkweli na muwazi,
, ukweli utakuweka huru!. Hili ni swali, "Jee hizi terorizing ziara za kushtukiza, hakutajenga nidhamu ya woga?!. Jee, kutasaidia?!.

Paskali
Hatukuishia Kwa Number 1 tuu,
ila pia niliendesha somo humu namna ya kutofautisha kuongea Kwa ukali na kufoka foka

hata number 3, yule Kiranja Mkuu wa viranja pia tuliwahi kumshauri

Hata baadhi ya Mawaziri walipokosa utu, akina sisi tuliwasema...

Na hatukuishia viongozi wakuu na Mawaziri pekee, hata ma RC tuliwamulika

Huyu pia

Hivyo hili la nidhamu ya woga lilikuwepo sana kwa JPM, lakini twende nyuma na kurudi mbele,
Kwa hali hii, mfano Mama naye ni binadamu, anaweza kukosea, jee akikosea kibinaadamu, kuna kiongozi yoyote ndani ya serikali anaweza kum correct, au kuna any main stream media that would dare criticize or correct her, or the epitome of cowardice inaendelea?!.

Nasisitiza Mama naye she is a human being, anahitaji kusapotiwa, kusaidiwa, kushauriwa, na akikosea akosolewe kistaarabu kwa lugha ya heshima na staha huku akishauriwa the right thing to do, ushauri wangu wa kwanza, ni Tanzania tunaweza kabisa kusonga mbele na kufanya mazuri bila kunyoosheana vidole and calling names kama "Simba wa Yuda".
Nashauri tufanye tuu mambo tofauti bila kumtaja taja Kwa ubaya!
Aachwe Apumzike!.

Jumapili Njema

Paskali.
 
Back
Top Bottom