Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huo muda wa kwenda kupekua uliposema sina.. Ila walioona wanakushangaa hapa unavyokataa.
Kama vipi nirudishe Ignore List tu ntakuboa..
Pasco ,
Huyo Majaliwa anatumwa tu. Mwenyewe Magufuli.
Na kama hamjaweza kumsema Magufuli alipolipangia bunge jinsi ya kufanya tafrija, kitu ambacho hana mamlaka nacho kikatiba ( checks and balances haziruhusu, I haven't seen an article on this), huyo Waziri Mkuu kuvamia mashirika ya umma, kitu ambacho ana mamlaka nacho, hamtaweza hata pa kuanzia.
Weka hapa niliposema nina apartments Masaki na Msasani.
Sasa na hiyo namba ya simu ndo unataka kusema kuwa ni yangu?
Hahahaaa hebu ipige basi tuone....
Na maisha yangu wala huyajui kabisa.
Usitake kujifanya unayajua. Huyajui, mimi hunijui [wait...yeah naitwa Richard Muguzi:biggrin1:], na hujui chochote juu yangu zaidi ya kunisoma tu humu.
Na kwanza wala siishi Atlanta mimi. Uthibitisho mwingine kuwa hujui kitu.
Inaonekana wewe una upeo mdogo sana
hadi comments zako zingine nashindwa ku reply
Kama wewe mwananchi unapenda kinachoendelea basi ujue wapo wananchi wengine hatupendi pia kinachoendelea
hatupendi kusikia waziri mkuu kagundua makontena yamepotea kila siku
tungependa hilo tatizo liwe fixed for good....wezi wakamatwe wafungwe..system ibadilishwe
biashara ziendelee na tuzungumze mengine yenye umuhimu..
sio kila mtu ana enjoy kutazama tv na kukuta the never ending story ya makontena.....
wengine tungependa story tofauti huko bandarini ...success stories.....
sisi wengine hatumpongezi mtu kwa ku expose tatizo
tunapongeza watu kwa kuli fix tatizo for good....sio kila wiki habari ndo hiyo hiyo...
Hawa sio viongozi nadhani hawajui wanataka kuifanyia nchi hii yaani majaliwa anauliza makontena 2431 ya January to December 2014 kwenye serikali waliyokuwemo kwa kweli nimeamini hawana plan yakutuvusha haya mambo yakupachikwa kwenye uongozi tabu tupu
Huo muda wa kwenda kupekua uliposema sina..
Endelea kula Junk Foods huko wahed wewe...
teh teh teh teh teh hiyo dozi ya leo inakutosha..
Endelea kula Junk Foods huko wahed wewe...
teh teh teh teh teh hiyo dozi ya leo inakutosha..
Mkuu nchi ina matatizo meng huwez kufix siku moja leo kawaambia wafunge mfumo kulipia ki electronics.kikubwa alichofuata bandari kukagua ule mfumo wa kupitishia mizigo na kuona inakuwaje kunatokea ubadhirifu?kingne ni kumuuliza meneja mbona kwenye ripot ya CAG waliochukuliwa hatua ni vidagaa 10 tu,mbona mapapa yameachwa?ubaya uko wap hapo?PM kukagua ofisi ya umma?
Inawezekana tunabishana sana hadi tunashindwa kujua nini tunabishania
watu hatupingi nia nzuri ya Waziri mkuu au Rais
ishu hapa sio nia nzuri ,ishu hapa ni njia nzuri ya ku fix tatizo
kuna ulazima wa waziri mkuu kwenda bandarini ghafla mara mbili in a week?
hawezi toa maagizo yakatekelezwa?
kama hilo haliwezekani basi tatizo lipo kubwa somewhere...
Wanabodi,
Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.
Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.
Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.
Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.
Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.
Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.
Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.
Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco
Huna ujualo.
Umebaki kujitekenya na kucheka tu.
Unaweka namba za simu za ajabu ajabu tu ili uonekane unanijua.
Hahahaaa una hamu kweli ya kutaka kunijua wewe eeh?
Mh, pasco, ni wewe kweli wasema hayo! Hayo yanayoandikwa humu JF na kushangiliwa! Hayo yanayowekwa kwenye magazeti ya udaku! VIOJA vinavyofanywa na viongozi! Ufisadi uliokubuhu! Udanganyifu na uzembe uliotukuka. Enough is enough.
CHEO NI DHAMANA
TAFAKARI CHUKUA HATUA
Hayo Mapigo Uliyotoa Ni Kama Ya Ninja Assasin, Picha Limekwisha
You would think angeweza tu kuwaita wahusika ofisini kwake na kujieleza kuliko kwenda bandarini na makamera lukuki.
Kwenda yeye mwenyewe huko bandarini na kuanza kuhoji watumishi wa hapo kunaweza kukatafsiriwa vibaya kuwa wanatafuta sifa tu.