Good governance my foot. Maneno meeeengi. Si ungesema tu "tunaonekana vichwamaji tulioahidiwa mabadaliko feki na Lowassa, na sasa aibu inatusuda kwa kushuhudia mabadiliko halisi"? Nani atarajie pongezi kwa ninyi mliokuwa mnamsujudia Lowassa. Na sasa Lowassa halisi anaanza kujulikana kupitia kwa washikrika wake wa karibu akina Awale. Mliimba sana "kama fisadi mpelekeni jela basi" sasa kilio chenu kinasikilizwa na kutekelezwa.
Unataka awataarifu "jamani ee, nakuja kukagua kuhusu upotevu wa makontena. Naomba mniandalie taarifa kamili."?
Ni mtu mwenye matatizo ya akili tu anaweza kuhoji utendaji kazi wa Majaliwa ilhali habari ya msingi ni upotevu wa MAKONTENA ELFU MBILI NA UPUUZI. Nazungumzia makontena as containers za kubebea cargo bandarini sio kontena za take away.
Nendeni zenu huko, hamna hoja, hamha mpya, mnaugulia maumivu tu. Who cares fisadi akiumbuliwa if it helps kupambana na ufisadi? The end justifies the means. Unadhani angeenda kuwachekachekea kama JK tungefahamu kuhusu upotevu huo wa makontena?
Yes, alikuwa na facts lakini alichofanya ni kupata other side of the story kutoka kwa wahusika. La muhimu ni kukamata mhalifu na sio jinsi alivyokamatwa. Msituletee utetezi kama ule wa JK kuhusu HAKI ZA BINADAMU ZA MAFISADI.
Ushauri mwepesi: Lowassa alishindwa urais kabla ya siku ya kura.Tulijaribu sana kuwafumbua macho mkatuona hamnazo. Sasa mnakula jeuri yenu. Choice ni nyepesi, subirini 2020 kama hamwezi kuungana nasi katika operesheni ya kutumbua majipu.
By the way, kelele za chura hazimzuwii ng'ombe kunywa maji.