Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Watu wamelala sana acha waamshwe ili wafanye kazi zao vzr!
Tuache kufanya kazi kwa mazoea ndicho anachosisitiza
 
Aaah wanyooshwe tu..ni sawa kabisa PM anavofanya
 
Kaka Paschal katika Posts zako zote nzuri hii ya leo umechemsha, tangu kipindi cha mkapa kuna neno linaotwa Transparency tukaja kwa Kikwete kuna kitu kinaitw Open Government Partnetship yaani katika kuendesha serikali ambayo inatokana na wananchi ni vema mambo yote serikalini yawe wazi; haya mambo ya kuficha magonjwa kila dpcument ya serikali na maamizi kugongwa muhuri wa 'Siri' ndio yametufikisha hapa watu wamekuwa wanafanya madudu with impunity! Swala la serikali ya wananchi siyo la mke nyumbani maana yeye anakuhudumia wewe privately ila serikali ni ya umma (public).in light of this ninasupport zaidi ya 100% style ya utendanji wa serikali ya awamu ya 5.Bravo shughulikia haya majitu ambayo yamezoea kufanya kazi kwa mazoea na kufikiri miungu watu.
 
Subconsciously, you are caught up arleady! No wonder you spend a lot of energy being their critique.

Negative!

I don't spend a lot of energy criticizing anybody.

And trust me, I am a very high energy guy.
 
Mkuu Pasco Nasubiri upropose njia ya kistaarabu ya kupambana na uharamia...

Nami ngoja nisubiri toka kwa ndugu Pasco kuhusu proposal yake! Jamaa ni mchangiaji mkubwa sana na kwa kusomaga sredi zake, nafikiri ni kaka/ mjomba/ baba 'anayejitambua' sana! Ila inanisikitisha kuwa siku za hizi karibuni ameongeza kiwango chake cha kuponda mambo ambayo ni mazuri kwa maslahi mapana ya taifa, na amekuwa akiponda bila kuleta 'njia sahihi' ya kuepukana na anachofikiri yeye sio sahihi! Kaka/ mjomba/ baba yetu ndugu Pasco, mimi ni mmoja ya watu wanaosoma sana na mara nyingi siachagi sredi zako zinipite, nakusihi ziboreshe zaidi, unapo criticize uwe pia unaweka njia mbadala ya kuboresha hicho ambacho hauja kikubali! Hii pia iende kwa Nyani Ngabu, The Boss na wengine. Kulalamika bila kutoa suluhisho mbadala haujengi kitu!
 
Last edited by a moderator:
Negative!

I don't spend a lot of energy criticizing anybody.

And trust me, I am a very high energy guy.
I didn't expect you to accept that, but whoever goes through your comments in JF will agree with me, PLUS blowing your own trumpet is also your thing!
 
waache wazalendo wafanye kazi...kuviziana au kutoviziana doesn't matter...cha msingi ni kweli makosa yamefanyika...we unataka awastue ili waandae uwongo wa kumwambia...naikubali serikali ya awamu hii
 
Anavyofanya sawa sawa. Waache Headmaster (Magufuli) na Academic Master (Majaliwa) wetu wachape kazi.

Tena Bado Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Nendeni na huko. Majengo yote yale waliyojenga lazima Kuna Mafisadi wa majengo hatari.

Fanyeni kazi bila kumuangalia mtu usoni, iwe barabarani, ofisini au korokoroni.

Go Magufuli, Go Majaliwa. Tumbueni MAJIPU.

We are behind you, and we pray for you.

Ungekuwa umesomea maswala ya uongozi usingejibu hivi...wanaojua maswala ya good governance,management,leadership wataweza kukosoa kitu kwenye haya.uongozi si kudhalilishana na si busara kumhoji mtu na kumdhalilisha huku anamilikwa na macamera.hata barabara za mwendo kasi dar sasa hivi mvua zikinyesha zinajaa Maji na zina mapungufu mengi.Tukisema tuende na macamera kumhoji wazir husika kwanza atadhalilika sio kwa sababu yeye anahudika direct barabara kuwa vile bali yeye pengine watendaji walioko chini yake walipindisha mambo au katika utekelezaji wa mradi huo alikutana na vipingamizi kama vya kutoruhusiwa kubomoa tanesco (mfano tu).Nadhani kuna namna ya kushughulikia haya mambo na kila mtu akahukimiwa kwa matendo yake na si kwa hivi vinavyofanyika.what if yeye huyo unaemdhalilisha hausiki na sana sana alipata maagizo toka juu na ushahidi anao.tukubali kuwa hii nchi ilikuwa corrupt na ni corrupt mpaka sasa na hamna ambaye hayuko corrupt kwa nafasi aliyoko.
 
sisi hapa ni kazi kuna watu walijiona juu ya sheria wakafanya hii nchi kama mali yao lakini walisahau hizo pesa ni kodi ya watanzania wote lazima nidhamu irudi wamechekewa vya kutosha zile wanazosomewa sio tuhuma bali ni vitu vyenye ushahidi walizoea kudanganya viongozi bila kufanya hivyotutaendelea kulalamika tu
 
Ungekuwa umesomea maswala ya uongozi usingejibu hivi...wanaojua maswala ya good governance,management,leadership wataweza kukosoa kitu kwenye haya.uongozi si kudhalilishana na si busara kumhoji mtu na kumdhalilisha huku anamilikwa na macamera.hata barabara za mwendo kasi dar sasa hivi mvua zikinyesha zinajaa Maji na zina mapungufu mengi.Tukisema tuende na macamera kumhoji wazir husika kwanza atadhalilika sio kwa sababu yeye anahudika direct barabara kuwa vile bali yeye pengine watendaji walioko chini yake walipindisha mambo au katika utekelezaji wa mradi huo alikutana na vipingamizi kama vya kutoruhusiwa kubomoa tanesco (mfano tu).Nadhani kuna namna ya kushughulikia haya mambo na kila mtu akahukimiwa kwa matendo yake na si kwa hivi vinavyofanyika.what if yeye huyo unaemdhalilisha hausiki na sana sana alipata maagizo toka juu na ushahidi anao.tukubali kuwa hii nchi ilikuwa corrupt na ni corrupt mpaka sasa na hamna ambaye hayuko corrupt kwa nafasi aliyoko.
Unataka good governance ila unashindwa tambua hao watu wenyewe wameshindwa kuonyesha kuwa wana uwezo wa kuwa well governed!!
Watu wazima sisi, tuache kukariri jamani. Kufanya vitu kwa mazoea na hiyo 'good governance' ndo kumetufikisha hapa.
Nafikiri hata polisi hutumia strategy moja ya ku-control fujo ya watu wengi, kama umati ni mkubwa na wanaleta fujo, wanabamiza mmoja na risasi ya moto kama onyo kwa wengine! Ndo afanyacho waziri mkuu. Wengine wataona wenzao 'wanavyodhalilishwa' kwa kutokuwa waadilifu, watajifunza jinsi ya kuwa waadilifu kipitia hawa 'mbuzi wa kafara'!
 
Enzi za Nyerere ilikuwa ukiitwa mlanguzi unabaguliwa. Unaonekana hufai ktk jamii. Kwa haya yanayofanyika CEO wengine watatia akili na kukaa sawa kwenye nafasi zao.

Unachosema ni kweli..ila hebu fikiria kama wewe upo ofisi fulani ,halafu kuna ishu ulifanya ya kimemo kutoka juu.na kumbuka ishu ya mkubwa huwa unafanywa tena kwa kutetemeka.yaan halmashaur hata ishu ya mwenyekiti wa halmashaur tu huwa wahasibu wanakimbizana..sasa hebu fikiria kama umewahipitisha kitu kama hicho halafu Leo hii unadhalilika wakati hukula hata mia.kiukweli mi nasema watumishi watadhalilika sana ila na hawa wanasiasa waache Tabia ya kutuma vi memo.maana ndivyo vinavyocost watu sasa.Nina uhakika ukienda TRA kuna vimemo vingi sana vya hawa jamaa.Halafu kingine ukiwa na Tabia ya kumshirikisha mtu kwenye uhalifu lazima na yeye atafika mahali atakuwa mhalifu tu.Vimemo hivi huwa vinafundisha watu mengi.
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco

Paschal mayallah ktk ubora wake
 
Unataka good governance ila unashindwa tambua hao watu wenyewe wameshindwa kuonyesha kuwa wana uwezo wa kuwa well governed!!
Watu wazima sisi, tuache kukariri jamani. Kufanya vitu kwa mazoea na hiyo 'good governance' ndo kumetufikisha hapa.
Nafikiri hata polisi hutumia strategy moja ya ku-control fujo ya watu wengi, kama umati ni mkubwa na wanaleta fujo, wanabamiza mmoja na risasi ya moto kama onyo kwa wengine! Ndo afanyacho waziri mkuu. Wengine wataona wenzao 'wanavyodhalilishwa' kwa kutokuwa waadilifu, watajifunza jinsi ya kuwa waadilifu kipitia hawa 'mbuzi wa kafara'!

Hatujawahi kuwa na good governance,kila mtu anakuja na style yake bt still good governance ni ngumu kuitekeleza hasa kwa tulipofikia.napenda ufuatiliaji wa uongozi wa sasa ila tukubali tu hamna msafi katika haya.yaani hata balozi wa nyumba kumi.tulishashuka shimoni wote na hakuna kinachokera kama vile visimu kutoka juu...yaan vitalazimisha kufanya jambo hata kama hujakusudia.watu wakubali kudhalilika whether walihusika direct or indirect ila n watumishi wajifunze kitu.kitakachookoa ni uadilifu kuanzia huko kwa wanasiasa na huku kwa watumishi.wanasiasa wanaingiliaga sana profession za watu na kujifanyia watakavyo...ila kwa hili watu watajifunza kuwa kura za ndio ni tofauti na taaluma.
 
Back
Top Bottom