Hapa umeiweka vyema. Saikolojia ya wachawi, hapa ni kwa wote wanaowatakia wengine mabaya. Ukiwapuuza kwa kuwa na neutral response kwa kile wanachokufanyia huumia sana. Kama ulivyosema, Wenyewe kama waona una huzuni hufurahi sana. Lkn ukiwa na furaha wanaugua sana. Halafu wanaanza kukuogopa kwamba wewe ni mchawi. Na ni kweli unakuwa mchawi wao, hata utakuwa na uwezo wa kuwatambua. Maana watakuwa wanajistukia ukikutana nao.
Lakini ili ufanikiwe, pia Mungu aweke mkono wake, inabidi uwe na maisha tofauti. Epuka kujichanganya kwenye ulevi, uzinzi/uasherati, uzulumaji, ugomvi, uizi, nk. Utauona utukufu wa Bwana