Anachokitaka mchawi kutoka kwako sio kingine chochote isipokuwa furaha yako. Sababu hizi hapa

Anachokitaka mchawi kutoka kwako sio kingine chochote isipokuwa furaha yako. Sababu hizi hapa

Kuna wajinga wanapigaga ngoma juu ya bati langu huku wwkimwaga michanga ila kila nikitaka kutoka najikuta napuuza sababu ya usingzi.
Inanishangaza sana sababu usiku huo nayapuuza najiachia kabisa ila ikifika mchana najiuliza huo ujasiri wa kupuuza mambo kama haya nautoa wapi
🤣🤣🤣🤣🤭
 
Na mchawi wewe LIKUD unataka nini unavyowahamasisha wazazi waliopeleka watoto wao EM's kuwahamishia kayumba?
Itakuwa anataka afurahi hao wazazi watakapokuwa wanasononeka kwa watoto wao kutojua kingreza baada ya kuhamishiwa huko kayumba!
 
Kuna wajinga wanapigaga ngoma juu ya bati langu huku wwkimwaga michanga ila kila nikitaka kutoka najikuta napuuza sababu ya usingzi.
Inanishangaza sana sababu usiku huo nayapuuza najiachia kabisa ila ikifika mchana najiuliza huo ujasiri wa kupuuza mambo kama haya nautoa wapi
Fanya hivyo hivyo mkuu usipanic wala. Usiogope hawana lolote wanakutia hofu tu hawataki Uwe na furaha
 
Mchawi hana shida na wewe kuwa tajiri as long as your not happy with your money ( mfano uugue Maradhi ya kukusosesha furaha: E.g kukufanya ushindwe kusimamisha vizuri, usile baadhi ya vyakula mfano vyakula vyenye chumvi, sukari, usinywe pombe etc)

Mchawi hana shida na wewe mtoto wa kike kuolewa na tajiri as long as hautakuwa na furaha kwenye ndoa.

Hana shida na degree wala masters yako as long as hautakuwa na furaha nayo

Hana shida na kazi yako au biashara yako kufanya vizuri as long as havitakuwa vinakupa furaha.

Anacho kitaka kutoka kwako ni furaha yako.

Kwa nini? 👇👇👇👇👇

Kwa sababu the currency in the realm of the spirit is energy. The higher the energy the richer the person. ( The medium of exchange is energy)

Furaha ( happiness) is the most highest and valuable currency in the realm of the spirits.

Katika ulimwengu wa roho, furaha ndio nishati yenye thamani ya juu kuliko kitu chochote kile.

Wachawi hawanaga furaha kwa sababu hawana nafsi yenye uhai. Nafsi zao zimekufa. Ndio maana hazina uwezo wa kupokea taarifa nzuri kuhusu watu wengine.

Mchawi anapokuona hauna furaha hukasirika na hutamani ile furaha uliyo nayo wewe ihamie kwake, so anacho kifanya ni kufanya kitu kitakacho kuondolea furaha yako. Furaha yako ikitoweka na wewe ukawa na huzuni basi yeye ndio hufurahia nafsi yake. ( Hapo anakuwa amefanya energy exchange)

Sasa basi ukitaka kuwakomesha wachawi( watu wote wenye husda na maisha yako whether unawajua au huwajui) basi wewe endelea kuonyesha furaha hata katika kipindi ambacho wana expect utakua na huzuni. . . Hali huwa inakua mbaya sana kwao kwa sababu ile huzuni waliyo itegemea kuja kwako hua inarejea kwao mara saba. ..

Kwa mfano walifurahi binti mzuri wa jirani Yao alipopata mimba shuleni akapata tena mimba nyingine ya pili baba hajulikani.

Then baadae wakasikia anaolewa na tajiri, wakafanya uchawi na fitna ndoa ika hairishwa siku moja kabla Bwana Harusi akaota mbawa. Watategemea binti awe na huzuni ya kwenda.

Kesho yake akionekana binti yupo na furaha as if nothing has happened na aka maintain kuwa na hiyo furaha basibasi, basi ile huzuni waliyo I anticipate kwa huyo binti itarejea kwao maradufu.

# Hakikisha unakuwa na furaha wakati wote no matter what the circumstances.

Hapa umeiweka vyema. Saikolojia ya wachawi, hapa ni kwa wote wanaowatakia wengine mabaya. Ukiwapuuza kwa kuwa na neutral response kwa kile wanachokufanyia huumia sana. Kama ulivyosema, Wenyewe kama waona una huzuni hufurahi sana. Lkn ukiwa na furaha wanaugua sana. Halafu wanaanza kukuogopa kwamba wewe ni mchawi. Na ni kweli unakuwa mchawi wao, hata utakuwa na uwezo wa kuwatambua. Maana watakuwa wanajistukia ukikutana nao.
Lakini ili ufanikiwe, pia Mungu aweke mkono wake, inabidi uwe na maisha tofauti. Epuka kujichanganya kwenye ulevi, uzinzi/uasherati, uzulumaji, ugomvi, uizi, nk. Utauona utukufu wa Bwana
 
kuna mama mmoja mtaani wanasema ni mwanga nakaurithi uchawi kutoka ka bibi yake, bas ana mtoto wake wa pekee wakike watu pia husema anafundishwa uchawi na mama yake, hii ni kutokana na tabia akipata mwanaume lazma arogwe aoe mwisho wa siku mwanaume hupepea harudi kabisa

sasa kisa changu kinaanza huyu mama alitokea kunichukia from no where tangu nimehamia kwenye mji wangu, yan alianza kwanza ukipika lazima akuulize hujabakisha samaki ukanipa sjui hujabakisha kitu unipe mm mwanzon skua namjua so hata akiwa ananambia hayo mm hua nimemalizasina bas humjibu tu sina wameisha nahisi akaona namnyima but aikua aware naona tu ni jirani nikipita namsalimia naendelea na mishe zangu, akaanza visa tukiwa tupo kwenye shughuli za mtaani kama nipp na mtu anasalimia huyo nutakayekuwanaye kwa majina nikaona huu ufala amenitafuta muda mref sana but i always mantain my silence, yan hua simjibu kitu chochote kile.

siku moja ninelala mchana nikaota kanifwata yeyr na mwanae usingizin wakata kunichangia wanifungie kwenye chumba wanifue, bas sjui nilipata nguvu za wapi nikawakanda vizuri tu, mama mtu akakimbia nikambeba mwanae juu juu nikamtupa chini kama wanavyofanya kwenye wrestling, nikamwambia ukiendelea kunifuatilia nitakuua nikastuka nikajiuliza hiki nn kwa nn hii ndoto kwa nn wao nikamhadithia mama yangu mama akaguna akanambia nanhivo hamuelewani watajua na Mungu wao, nikapuuza hio siku niloota mchana usiku huyo mtoto akakimbizwa hospital analalamika kiuno kinamuuna kalazwa kuja kusikia hiimz habar nilikua kama nimapatwa na bumbuwazi.

najiuliza ni ile ndoto? au nimemkanda kweli?
 
Hapa umeiweka vyema. Saikolojia ya wachawi, hapa ni kwa wote wanaowatakia wengine mabaya. Ukiwapuuza kwa kuwa na neutral response kwa kile wanachokufanyia huumia sana. Kama ulivyosema, Wenyewe kama waona una huzuni hufurahi sana. Lkn ukiwa na furaha wanaugua sana. Halafu wanaanza kukuogopa kwamba wewe ni mchawi. Na ni kweli unakuwa mchawi wao, hata utakuwa na uwezo wa kuwatambua. Maana watakuwa wanajistukia ukikutana nao.
Lakini ili ufanikiwe, pia Mungu aweke mkono wake, inabidi uwe na maisha tofauti. Epuka kujichanganya kwenye ulevi, uzinzi/uasherati, uzulumaji, ugomvi, uizi, nk. Utauona utukufu wa Bwana
100% Fact
 
Back
Top Bottom