Anachosema Lissu ni kwamba, Bunge lisivunjwe mwezi wa sita, Rais na Wabunge waendelee hadi Reforms zikamilishwe, ndio uchaguzi mkuu ufanyike

Anachosema Lissu ni kwamba, Bunge lisivunjwe mwezi wa sita, Rais na Wabunge waendelee hadi Reforms zikamilishwe, ndio uchaguzi mkuu ufanyike

Ushauri wa kipumbavu sana, hawajajiandaa kwa uchaguzi wanataka muda, hatuwapumzishi, ni mchaka mchaka tu
Mara pap, vyombo vya dola vinasema haviko tayari tena kutumika kukibeba chama chochote cha siasa.
 
Ukitafakari sana, bila kuwa na utando wa kishabiki kichwani, Lissu anaongea kitu cha maana na hapa tayari ameonyesha ku-compromise na CCM. Nimesikiliza mahojiano yake kwa makini sana.

Pendekezo lake la "No Reforms na Elections" kwa alivyofafanua na nikamuelewa, anasema kwamba, Chadema wako tayari CCM iendelee kuwa madarakani kwa muda ulioongezwa, yaani Samia na Wabunge waendelee kuwa madarakani, hadi Reforms zikamilishwe.

Zikishakamilishwa basi ndipo sasa ipangwe Bunge livunjwe lini na Uchaguzi Mkuu ufanyike lini, labda October 2026 badala ya October 2025, au hata October 2027. Yaani Wabunge na Raisi waongezewe vipindi vyao vya sasa, labda mwaka mmoja, hadi miwili ikibidi, ili kufanya Reforms.

Sasa mimi nadhani kwa mtu mwenye kufikiri, hili si wazo baya, ni wazo la mtu mwenye akili na alie tayari kutafakari. Amesha-compromise.

Kwa upande wa pili ina make sense. Kwa nini uingie kwenye uchaguzi ambao unajua unafanyika katika misingi mibovu? Ni vema uahirishe uchaguzi ili urekebishe hiyo misingi mibovu kwanza.

Na hii ni lojiki ya kawaida ya maisha ya kila siku. Nikitaka kusafiri kesho, huku nikitambua gari nitakayotumia ni mbovu itanikwamisha njiani, basi ni vema nicheleweshe safari ili gari irekebishwe kuliko kusema ngoja niende tu nitafanya cha kufanya huko mbele. Unaweza ukafia njiani.

Sasa CCM msipoelewa hili nyie ni wakorofi na mnafanya makusudi kwa sababu hamtaki Reforms

Hebu Wasira katika busara za uzee wake atuambie ubaya wa hili wazo ni nini?

Angalia pia: Lissu amjibu Wasira. Asema Uchaguzi Mkuu usogezwe mbele kupata Katiba Mpya, vinginevyo watazuia uchaguzi kwa maandamano

Huyu ndiye Lisu ninayemjua .

Hakuna uchaguzi bila tume huru .

Polisi na jeshi awaambie ukweli CCM kuwa bunge lilivunjwa vyama vyote vinakuwa sana na hata mawaziri wanakua ni batili mana hatuna mawaziri wasio wabunge .

Kwa hiyo hata baraza la mawaziri linakua halipo . Masuala yote ya serikali yanakua chini ya Makatibu wakuu .

Rais anaomba upya ajira kwa watanzania sio kwa vyombo vya ulinzi na usalama .

Haya matatizo yamechangiwa sana na watu wachache wabinafsi ndani ya mifumo kushindwa kujua kuwa Mtu anayegombea urais ni binadamu na ni mtanzania kama wengine ila anawaomba wananchi wampigie kura za kumpa uongozi sio jeshi la polisi linapindua kura na kumpa l
asiyetakiwa na wananchi.

Kwa hali hiyo kama katiba inatoa upendeleo kwa chama tawala ili kuvuruga uchaguzi basi hakuna mn ya uchaguzi kufanyika na kupoteza fedha za umma bila sababu .

Maandano ni nchi nzima mpaka vijijini na vizee vyote marufuku kutoka nje kwenda kuwachagulia vijana viongozi wasiojali maslahi ya vijana kwenye ajira .

Kwa sasa Chadema ujipange tu kujenga ofisi za kila eneo mpaka vijijini na kuhakikisha zinakua na TV na dishi la Azam au DSTV. Wananchi wahamasishaji kukijenga na kukipigania chama chao.. Yale mambo ya kuchoma ofisi za Chadema yawe ni mwisho
Ikichomwa ya nyekundu basi zinachomwa za kijani kumi .
Jino kwa meno
 
Nimelisoma. Nachoona Lissu anataka Samia n bunge la CCM waongezewe muda ili tupate katiba mpya. Sielewi kwa nini anataka utawala wa CCM uongezewe muda.
Punguza utoto dogo utakuja kupakatwa. Watu wakiongea mambo yaliyonje ya upeo wake uache kiherehere. Subiri zile post zako zenye mambo ya kipuuzi ndio uweke huu utoto wako.
 
Mara pap, vyombo vya dola vinasema haviko tayari tena kutumika kukibeba chama chochote cha siasa.
I say, ikitokea tutazika wengi sana kwa pressure, na utashangaa wote ni wa chama kilekile!
 
Panic disorder
Kweli kabisa, safari hii TAL atawapigisha ngoma CCM wacheze hadi viuno viwakatike

Naona hapa chini kina wazee na kina mama wa CCM wakinengua kwa ngoma ya Tundu Lisu. Huyo aliebinuka sio Makamu mwenyekiti kweli? Kwa mbele namwona mwenyekiti akitingisha taarabu, na pembeni yake waziri wa fedha katika bright green top anazungusha kiuno, na kwa mbali pale namuona mkwe wa mtu akicheza kwa bidii zote! Mambo ni bum bam, kaza mikono Tundu, ngoma inogile!

1737744554438.png
 
Anatoa mawazo yasiyowezekana kufanikika anadhani CCM ni wajinga kiasi hicho yy kama hawez uchaguzi 2925 aususie wengine wale
Hayawezekani kwa nini? Tukipigwa Corona October uchaguzi utafanyika? Tukipatwa na janga la Tsunami Octoba Dar yote ikamezwa na maji na watu wakafa kwa wingi uchaguzi utafanyika?
 
Ccm wanatakiwa waondoke mapema kabla watu hawajaingiwa na mioyo ya kuanza kupambania nchi yao kwa vitendo, hawa polisi wanao walinda tunakaa nao mitaani wasijisahau wakahisi kama tuko mbali nao. Tunawaangalia tu
 
Anatoa mawazo yasiyowezekana kufanikika anadhani CCM ni wajinga kiasi hicho yy kama hawez uchaguzi 2925 aususie wengine wale

Hiyo biashara haipo kabisa .

Hata mkiazima majeshi kutoka Mongolia bado hakuna upumbavu wa kupoteza pesa za umma . Tutashawishi hizo pesa za uchaguzi wapewe polisi na wanajeshi waboreshe maisha yao . Walipwe viinua mgongo vya polisi na wanajeshi hizo pesa za uchaguzi badala ya kuwawekea vikokotoo halafu pesa nyingi zinakwenda kuwanufaisha wanasiasa wasiofanya siasa .

CCM hawafanyi siasa za kuomba kura kwa hoja . Sasa kwa nini tuwaite kuwa ni wanasiasa wakati wanahujumu siasa . Kazi ya majeshi sio kupigana na wananchi wao . Chama chenye wapiga kura zaidi ya mili. 6 huwezi ukakichezea kijinga kijinga eti kwa sababu una mabomu . Ni ujinga mkubwa . Tena wana bahati sana wanawekwa ndani bila kufanya kosa lolote halafu wanaambiwa waridhiane na watesi wao . Ilikua akivunjwa mguu wa nyekundu wanavunja watatu kama Israel na palestina ili wakiridhiana iwe ni pande zote zinakilio. Hii nchi sio ya Familia ya Samia na Kikwete . Hapana .
Wamejiona ni miungu watoa riziki kwa sababu ya madaraka makubwa waliyopewa na katiba . Wamejisahau kwa sababu ya utajiri walioupata kwenye madaraka . Wamesahau kuwa wao ndio wenye deni la kulipa fadhila kwa watanzania waliowapa kura na sio wao kufanywa Mungu kwa sababu ya vyombo vya dola vilivyojaa watoto wa maskini
 
Back
Top Bottom