Anaelekea kupata Mafao nimemshauri awekeze kwenye Bonds kakataa, anataka kufungua Baa

Kwani ilikuwa lazma akuskilize? Kashapiga hesabu zake mwache ale maisha
 
Siku hizi watu wanakodi fremu wanaweka viti vya mbao sub woofer la sea piano watu wanapokezana kuunganisha Bluetooth tu na yenyewe inakua bar.

Ni kwamba hafanyi biashara yoyote nje ya kuajiriwa na ndiyo anataka aanze biashara? Ambayo anaianza baada ya kustaafu?

Ila ushauri wako wa aweke 60M kwenye bonds ili kila mwisho wa mwezi apate laki tano naona siyo sahihi. Atakufa kwa desperation
 
Kuna anko wangu alipokua anafukuzia mafao anakuja town anafikia home akaomba ushauri, Na kulikua na nyumba inauzwa bei poa tukamshauri ainunue kama kuweka baadhi ya pesa mahali salama

Baada ya kupata pesa tu Anko akapotea na line akabadili akaenda bushinhuko akafungua baa na kuanza ujenzi

Baada ya muda kupita tukasikia anko baa imemshinda na ujenzi aujaisha na pesa imekata kabaki na lumbukumbu ya vikaunda suti alivyoshona
 

Huyu niliyemsimulia hapa ndo anaelekea huko
 
Akimaliza mwaka hajafa sijui..!
 
Biashara ya bar ina stress nyingi na inahitaji team making na mtu mwenye nguvu.. Kuna ushindani na wizi mkubwa kwenye hii biashara na faida ni kiduchu
Inabidi almost muda wote uwepo la sivyo utaambulia mabua
Wateja watataka kukuona nawe unakunywa ili wakuungishe zaidi.. Kwa umri wake hawezi kunywa daily
 
Unapomshauri mtu angalia na namna uelewa na mazingira yake. Mwenzio kazoea give n take, we unataka kumletea biashara za kisomi, mwenzio anataka aendelee kufanya kazi (kuwa productive), wewe unataka akae asubiri gawio hamtaelewana hapo.
Mwachie afanye kitu anachoona ni sahihi. Bar ndio kitu sahihi kwake mwache afanye.

Nje ya mada: kuwa na heshima, huwezi sema mjomba "ana wenge". Ni mama yako huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…