Anaelekea kupata Mafao nimemshauri awekeze kwenye Bonds kakataa, anataka kufungua Baa

Mwache afungue Baa yake, ila cha muhimu tu kwako usije ukamnunia, maana akija kuangukia pua atakutuhumu kuwa wewe ndiye umemloga.
 
Ameshapotea huyu mzee,ataweza pilika za kuendesha bar?,kwa kumsaidia sana,mwambie achukue 50ml,aweke bonds,na 10ml,inatosha sana kufungua min good bar...(Bar ni counter na choo+ store!)+ Jiko!
 
Tafuta vyako, urithi ni umasikini
 
Tafuta vyako, urithi ni umasikini
Kama ni hivyo basi familia zote za kitajiri ni za kipumbavu ...unaposikia neno tajiri maana yake ni familia ...waafrica tuna akili finyu sana mali ya familia ni kama mali za serikali zilivyo ni mali za wananchi siyo ya rais na viongozi tu ...hivyo kudhani mali za familia ni mali za mzazi ni UANITHI WA AKILI ...kwa nini iwe sawa mtoto kumjengea Nyumba mzazi ila iwe haramu mtoto kutegemea nyumba au mali za familia ?
 
NIC walikuja kazini, wakaanza kunishawishi nijiunge na bima yao, kuna ya miaka mitano,kumi na bima ya maisha, yaani nikaona moyo wangu unakuwa mgumu sana, mwisho wa siku nikawaambia siko tayari kwa sasa
 
Hio 60m atapata kiasi gani kwa mwezi? 600k
 
Ni asilimia ngapi ni familia za kitajiri kwa wana JF? Achanana watanzania wote. Unajua maana ya urithi wewe? Kwa masikini ni kuuza na kugawana. Kwa matajiri ni kutunza mali za familia na kuziendeleza. Unaposema watoto wagawiwe, hapo unadhihirisha kuwa nawe ni kizazi cha kimasikini (baba afe ili mali zake tugawane), badala ya mentalityya kitajiri, ambayo kwanza inasikitika baba kufa maana watoto wanapewa jukumu la kuendeleza utajiri mfano Mo.
 
Muache na hela zake ,,,, Hela za mjomba zinakuwashia nini ???? Yani mtu afanye utumishi wee uje umpangie afanye nini na mafao yake ?

Mwambie aongeze mke mwingine
Lakini mjomba si ndio kamfuata kuomba ushauri? Kulikuwa na ulazima gani wa kuomba ushauri wakati ameshafanya maamuzi yake?
 
NIC walikuja kazini, wakaanza kunishawishi nijiunge na bima yao, kuna ya miaka mitano,kumi na bima ya maisha, yaani nikaona moyo wangu unakuwa mgumu sana, mwisho wa siku nikawaambia siko tayari kwa sasa
Hao jamaa wahuni,hata ukichagua hiyo ya miaka mitano wanaweza kughushi ukajikuta kwenye bima ya maisha.

Hata kusaini tu hilo karatasi lao la mahudhurio wakija kazini kwako kuna watu walijikuta wameungwa juu kwa juu wakaanza kufyekwa.
 
Mwachee....
 
Biashara ya bar ni ngumu sana , mwanzoni utaanza vizuri ila mbeleni wateja wanahama.
 
Shida ya Waafrika wanapenda sana kitu kinaitwa kumiliki.
Yaani akiwa na duka, nyumba, guest house au duka anajisikia rahaaa.
Akiweka kwenye bonds anajiona kama hamiliki kitu na atakosa kuitwa boss.
Mwache atupe pesa
 
Hao watu hua ni wagumu sana kushaurika. Wewe shauri afu kaa pembeni. Sijawahi kuelewa sijui shida hua nini kwa wastaafu wengi. Kabla mafao hayajatoka anawasikilizaana familia yake. Ila akishapata hela anawaona familia kama maadui zake namba moja anaenda kubond na watubaki wa nje kabsaa ya familia. Hela zikiisha anarudisha majeshi kwa familia kihuruma huruma na mtamsaidia tu si ni mzazi wenu, ila inaumiza sana. Hii sio kwa wastaafu wa kike ama wa kiume nina experience na hii kitu aiseeh acha tu, ndani ya miaka miwili hana hata senti moja, hakuna investment yoyote yani anaishi kama vile hajawahi kufanya kazi. But wengi wanatapeliwa sana na watu wa nje ya familia. Akiwa mwelewa mtashukuru Mungu lakini akiwa mbishi hapo jipangeni tu kua mnamchangia kila mwezi maana wale jamaa hua ni kama mchwa wanahakikisha washampukutisha kila kitu ndo wanamwacha sasa mhangaike nae.
 
Wapi nimetaja neno urithi ? Wapi nimesema watoto wagawiwe urithi ? Tumia akili wewe pimbi wa ccm .. kuwapa watoto pesa ya kujipambania na kuwawezesha na kuipambania familia ndiyo akili ya matajiri wote duniani ...huyo mstaafu umri umesha kwenda anaweza kuhalibu mambo na kusababisha matatizo tu kwenye familia ...hivyo ni bora kuweka nguzo nyingi kuliko nguzo moja ..hiyo pesa nusu anafanya aonavyo na nusu anaiwekeza kwa watoto ...hii ndiyo akili.
 
Matusi si mtaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…