Hayo magari kama yaliingizwa bila kodi jiandae pia kulipia kodi,nadhani table ya kodi imewekwa hapo juu.Labda kama watakulipia kodi wenyewe,kitu ambacho najua hawawezi maana kodi itazidi hizo usd 6k unazowadai
Ila kama walishalipia kodi basi poa ,wakusaidie kubadilisha ownership maana TRA kwa sasa hawaeleweki sana wanaweza kuku charge capital gain tax,kwa kutafuta tofauti ya bei ya soko kwa hizo gari na kiasi ambacho wewe umewalipa ambacho ni hizo unazowadai.
otherwise wakuachie gari yao pamoja na docs ,wewe uendelee kutumia bila kubadili umiliki.Ila siku ukipata ajali malipo ya Bima itabidi yaingie kwenye akaunti inayosoma jina la mmiliki