Anahitajika msichana/mwanamke kwa ajili ya IVF

Anahitajika msichana/mwanamke kwa ajili ya IVF

IVF kirefu chake ni In Vitro Fertilization.
IVF ni jambo la kurutubisha kwa kuunganisha mbegu za uzazi za mwanamme na yai la uzazi la mwanamke maabara, baada ya hapo zoezi linalofatia ni kupandikiza ujauzito kwa mwanamke kwa njia ya sindano kisha ujauzito utaendelea kukua kama kawaida kwa mda wa miezi tisa kisha mwanamke atajifungua kawaida.

IVF haihusishi kukutana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume bali mwanaume anatoa mbegu kwa kujichua au punyeto na mwanamke anatolewa yai lililopevuka maabara na wataalamu baada ya hapo ndio ujauzito unapandikizwa kwa mwanamke,
Ni njia safi na salama na haihusishi operation kubwa na haina hatari yeyote kwa mwanamke.

Sasa anahitajika mwanamke au msichana katika zoezi hilo,

MALIPO
Moja malipo ni milioni 25 ambayo yatasainiwa kisheria mahakamani na ustawi wa jamii.
Pili kila mwezi atalipwa milioni moja kama malipo ya motisha kwa mda wa miezi tisa ya ujauzito, malipo hayo ni nje ya ile milioni 25.
Tatu kila siku atalipwa elfu ishirini kama gharama ya chakula kulea mimba kwa mda wa miezi tisa ya ujauzito.
Nne atalipwa shilingi elfu hamsini kila siku kama gharama ya chakula baada ya kujifungua kwa mda wa mwaka mmoja kipindi ananyonyesha.
Tano gharama zote za hospital kwa mama kipindi cha ujauzito, mama na mtoto baada ya kujifungua zitagharamiwa na baba wa mtoto/watoto

MASHARTI
Moja ujauzito utalelewa sehemu aliyopo baba wa watoto.
Mbili hauruhusiwi kisheria kutangaza kwa mtu yeyote kama una ujauzito labda wazazi wako tu, na wazazi wakiambiwa nao wataelimisha kuhusu hili sharti.
Tatu baada ya kujifungua, mtoto/watoto wakifikisha mwaka mmoja utawakabidhi kwa baba yao.
Nne baada ya kukabidhi mtoto/watoto hautoruhusiwa kisheria na kibinadam wewe ndugu zako au rafiki zako kuwaona mtoto/watoto kwa namna yeyote kipindi chote cha maisha yenu hapa duniani.
Tano hautoruhusiwa kuwa na mahusiano ya aina yoyote na baba wa watoto kabla na baada ya kujifungua mtoto/watoto.
Sita awe tayari kulea ujauzito akiwa jijini dar es salaam.

SIFA ZA MWANAMKE/MSICHANA ANAEHITAJIKA.
Moja awe na afya nzuri, asiwe na magonjwa ya akili, pili asiwe na magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi.
Pili awe mtanzania kutoka kabila na dini yeyote.
Tatu awe mrefu, mrefu sana atapewa upendeleo.
Nne awe mwembamba, akiwa mnene isiwe unene mkubwa sana.
Tano awe na umri wa kati ya miaka 25 hadi 35.
Sita awe mweupe au maji ya kunde asiwe mweusi sana.

Asanteni.
Pia kwa mwana Jamii Forum mwenye ndugu, rafiki au jirani mwenye hizo sifa naomba mnisaidie kusambaza hili tangazo.
Asante tena.

Vigezo na masharti kuzingatiwa
Wee hutakii hela??huna ndugu mpk uje huku
Mamboo ya kutapika mjusi kanisan mmh
 
[emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16][emoji38] we ni robot nini?

Tangazo litabaki kama lilivyo!

I wish nikuone live
Kama una sifa nilizotaja karibu ndugu,
Pia naomba ujue hili jambo ni serious na lipo kisheria, hivyo sitokujibu maswali yako au ya mtu mwingine kwa utashi wake au mawazo yake binafsi.
Nimeandika hivyo sababu nimeona post nyingi una ni quote kwa kushindwa kunielewa au kwa kutojibu kwa utashi wako au kwa jinsi unavyoona wewe ni sahihi.
 
Mfano dada ana vigezo vyote hapo na maisha yamempiga akijitokeza akakubali ilo dili dada anapata mtaji wa kujiinua kimaisha na jamaa anapata hitaji lake la mtoto sasa ubaya uko wapi hapo?
Kajaribu na wewe ujue ni rahisi au ngumu afuu ulete mrejesho hapa
 
Kwa nini utumie galama yote iyo kama shida ni toto si unaoa tu unazaa zaid ata hako kamoja unako kagalamia mamilioni iyo ni ndagu sio bule yaan apo mama anakufa namwanae tumboni.
 
Ukiwa na mipango mizuri milioni 50 inakutoa kimaisha.. hata ukipiga hustlings zingine hainaanishi kwamba pesa utayopata haitaisha na hapo hakuna utu wowote uliotolewa maana mtoto kwa sababu mtoto hajakufa wala hajadhulika unheambiwa ujifungue alafu mtoto umtoe kafara hapo tungesema hauna utu lakini unazaa kwa makubaliano unapewa chako na mtoto unamkabidhi kwenye mikono salama sioni utu wowote uliokiukwa hapo
Utu umekiukwa mkuu kwa kuthaminisha mtu kwa kitu (mtoto kwa pesa)... Ubinafsi pia kwa anaehitaji hivyo ni kwa matakwa binafsi bila kujua mbele watoto watahitaji nini ?(sio utu pia )
 
Utashangaa jf wanakupangia wanavyotakia wao
Hii ni changamoto sana ndugu na nashukuru nawe umeliona hilo jambo , nimeona kuna watu wachache wanataka nijibu maswali wanavyotaka wao, ila nawakumbusha kwamba hili ni jambo serious sana hivyo tangazo lililotolewa limejitosheleza kwa mtu ambaye yupo tayari ingawa ushauri pia nachukua
 
Kama una sifa nilizotaja karibu ndugu,
Pia naomba ujue hili jambo ni serious na lipo kisheria, hivyo sitokujibu maswali yako au ya mtu mwingine kwa utashi wake au mawazo yake binafsi.
Nimeandika hivyo sababu nimeona post nyingi una ni quote kwa kushindwa kunielewa au kwa kutojibu kwa utashi wako au kwa jinsi unavyoona wewe ni sahihi.
Sawa mkuu...[emoji119][emoji119]
 
Utu umekiukwa mkuu kwa kuthaminisha mtu kwa kitu (mtoto kwa pesa)... Ubinafsi pia kwa anaehitaji hivyo ni kwa matakwa binafsi bila kujua mbele watoto watahitaji nini ?(sio utu pia )
Kuna watu wanaishi maisha ya shida mkuu as long as mtu avunji sheria aachwe tu atumie chochote alichonacho kujikwamua.. masuala ya utu yabaki kuwa personal
 
Back
Top Bottom