Anahitajika msichana/mwanamke kwa ajili ya IVF

Anahitajika msichana/mwanamke kwa ajili ya IVF

Unatumia yai langu means mtoto atakuwa part of me, pia anyonyeshe mwaka mzima watengeneze bond kabisa halafu umchukue mtoto asimwone kabisa maisha yote.....heee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mim huwez nielewesha,utanielewesha nini?

Nimekuuliza mtoto akikuuliza mama yuko wapi utamjibu nini?
Asante kwa maoni,
Nimekujibu kwamba sio watoto wote duniani wamepata malezi kwa baba na mama.
Pia hao watoto wameweza kukua kwa furaha na afya pengine kuliko wale waliolelewa na wazazi wote wawili.
 
Huu msemo umenikumbusha mbali.. Mazaa alipenda kutuambia hivi ni baada ya maneno kua mengi kutoka kwa ndugu zake kua anazaa hovyo kwetu tupo 7 tumebaba kwenye kijumba chetu hadi tumekua.

Aunt aliokua anasema hivi yeye alizaa watoto 2 tu (sasa wote wameshaolew) yupo mkiwa na jumba lake hata housegirls hawadumu... anamsumbua maza kila siku ampe mdogo wangu mmoja wa kike akae nae mimi na bro hatutaki sikia hiyo habari TAJIRI NA MALI ZAKE MASIKINI NA WANAE.
Hahaha kwani nyie hamtakua muoe na kuolewa? Hahah kweli kila mtu atumie chake
 
Asante kwa maoni,
Nimekujibu kwamba sio watoto wote duniani wamepata malezi kwa baba na mama.
Pia hao watoto wameweza kukua kwa furaha na afya pengine kuliko wale waliolelewa na wazazi wote wawili.
Huu ni utoto sasa

Endeleeni kujificha ila ukweli tunaujua,mnajua hamwezi kupata watoto sasa mmeibukia kwny ivf ili nanyi muonekane mnawatoto lakini ukweli unafahamika mnakazwa.
 
Huu ni utoto sasa

Endeleeni kujificha ila ukweli tunaujua,mnajua hamwezi kupata watoto sasa mmeibukia kwny ivf ili nanyi muonekane mnawatoto lakini ukweli unafahamia mnakazwa.
Asante kwa maoni ndugu, ila huo ni mtazamo wako.
Kuna vitu vingine viko juu ya uwezo wako, hivyo penda kujifunza vitu usivyofaham.
Pia usipende kushinikiza na kukisema uongo kitu usichokifahamu vizuri.
 
Hahaha kwani nyie hamtakua muoe na kuolewa? Hahah kweli kila mtu atumie chake
Mkuu kwetu hapajawahi kuisha watu nyumba ni ndogo lakn hijawahi kujaa... kuna housgirl maza alimtaftia akakaa miezi miwili akashindwa... lkn alirudi kukaa kwetu pale 2years bila malipo
 
Umekosea kusema akae nae kwa Mwaka mmoja,
Wenzio hua wanawachukua mara baada ya kujifungua yaani wakati mtoto anatoka unatakiwa uwe pembeni unampokea kutoka kwa madaktari na sio yeye ili kuondoa ile bond ya Mama na Mtoto, hiyo ndio maana ya Surrogate Mother.
 
Asante kwa ushauri mzuri ndugu,
Hili jambo bado halijatekelezwa hivyo nitazingatia kila ushauri mzuri ili niweze kufanya jambo lililo bora zaidi.
 
Asante kwa ushauri mzuri ndugu,
Hili jambo bado halijatekelezwa hivyo nitazingatia kila ushauri mzuri ili niweze kufanya jambo lililo bora zaidi.
Naam,
Hapo ni kumwambia Mama awe anakamua maziwa kwa miezi mitatu ili Mtoto apate lishe bora ila hawaonani wala hamnyonyeshi baada ya hapo Mtoto ataendelea na virutubisho vingine,
Lakini kuwakutanisha ni mbaya mnoo haifai.
 
Kuna mwamba anaitwa Dennis kama nsikosee yeye alifanikisha hii njia alitumia around 70M... sabab zake zilikua nyepesi kwa mtazamo wangu.

mkuu mitindo huru hujaweka bayana sababu zako huenda ni usiri kwa mambo binafsi au ni swala la kifamilia ( nikimaanisha makubaliano kati ya wewe na mke wako)

Je umajaribu njia nyingine zote na hii ni chaguo la mwisho kwako ? KAMA NDIO NIKUTAKIE KILA JEMA KUPATA HITAJI LAKO KWANI WATOTO/MTOTO NI SEHEMU YA FURAHA

Kwa ishu ya surrogate yeye pia kua ndo mtoa yai.. ungetafuta mtoa yai mwingine surrogate abebe tu kwani sharti la mama kutengana na mtoto baada ya mwaka ni gumu mno.
 
Asante sana kwa ushauri mzuri ndugu,
Nitazingatia sababu bado sijafanya hitimisho ya hili jambo
 
Naam,
Hapo ni kumwambia Mama awe anakamua maziwa kwa miezi mitatu ili Mtoto apate lishe bora ila hawaonani wala hamnyonyeshi baada ya hapo Mtoto ataendelea na virutubisho vingine,
Lakini kuwakutanisha ni mbaya mnoo haifai.
Asante sana kwa ushauri, nitazingatia pia nikiwashirikisha wataalamu wa afya.
 
IVF kirefu chake ni In Vitro Fertilization.
IVF ni jambo la kurutubisha kwa kuunganisha mbegu za uzazi za mwanamme na yai la uzazi la mwanamke maabara, baada ya hapo zoezi linalofatia ni kupandikiza ujauzito kwa mwanamke kwa njia ya sindano kisha ujauzito utaendelea kukua kama kawaida kwa mda wa miezi tisa kisha mwanamke atajifungua kawaida.

IVF haihusishi kukutana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume bali mwanaume anatoa mbegu kwa kujichua au punyeto na mwanamke anatolewa yai lililopevuka maabara na wataalamu baada ya hapo ndio ujauzito unapandikizwa kwa mwanamke,
Ni njia safi na salama na haihusishi operation kubwa na haina hatari yeyote kwa mwanamke.

Sasa anahitajika mwanamke au msichana katika zoezi hilo,

MALIPO
Moja malipo ni milioni 25 ambayo yatasainiwa kisheria mahakamani na ustawi wa jamii.
Pili kila mwezi atalipwa milioni moja kama malipo ya motisha kwa mda wa miezi tisa ya ujauzito, malipo hayo ni nje ya ile milioni 25.
Tatu kila siku atalipwa elfu ishirini kama gharama ya chakula kulea mimba kwa mda wa miezi tisa ya ujauzito.
Nne atalipwa shilingi elfu hamsini kila siku kama gharama ya chakula baada ya kujifungua kwa mda wa mwaka mmoja kipindi ananyonyesha.
Tano gharama zote za hospital kwa mama kipindi cha ujauzito, mama na mtoto baada ya kujifungua zitagharamiwa na baba wa mtoto/watoto

MASHARTI
Moja ujauzito utalelewa sehemu aliyopo baba wa watoto.
Mbili hauruhusiwi kisheria kutangaza kwa mtu yeyote kama una ujauzito labda wazazi wako tu, na wazazi wakiambiwa nao wataelimisha kuhusu hili sharti.
Tatu baada ya kujifungua, mtoto/watoto wakifikisha mwaka mmoja utawakabidhi kwa baba yao.
Nne baada ya kukabidhi mtoto/watoto hautoruhusiwa kisheria na kibinadam wewe ndugu zako au rafiki zako kuwaona mtoto/watoto kwa namna yeyote kipindi chote cha maisha yenu hapa duniani.
Tano hautoruhusiwa kuwa na mahusiano ya aina yoyote na baba wa watoto kabla na baada ya kujifungua mtoto/watoto.
Sita awe tayari kulea ujauzito akiwa jijini dar es salaam.

SIFA ZA MWANAMKE/MSICHANA ANAEHITAJIKA.
Moja awe na afya nzuri, asiwe na magonjwa ya akili, pili asiwe na magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi.
Pili awe mtanzania kutoka kabila na dini yeyote.
Tatu awe mrefu, mrefu sana atapewa upendeleo.
Nne awe mwembamba, akiwa mnene isiwe unene mkubwa sana.
Tano awe na umri wa kati ya miaka 25 hadi 35.
Sita awe mweupe au maji ya kunde asiwe mweusi sana.

Asanteni.
Pia kwa mwana Jamii Forum mwenye ndugu, rafiki au jirani mwenye hizo sifa naomba mnisaidie kusambaza hili tangazo.
Asante tena.

Vigezo na masharti kuzingatiwa
Aitwaaaa Surrogate!!
 
Back
Top Bottom