Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema wazee.
Yule Mama alikuwa muuza vitumbua, alikuwa maarufu Kwa vitumbua vyake kwani vilikuwa vitamu sana. Kwa siku alikuwa anauza ndoo Mbili.
Zikaja Stori kuwa Yule Bi.mkubwa ni mlozi, kikagula, jichawi lililoshindikana.
Bado nakumbuka, wakaitwa Wale watoa Uchawi, Kwa mliokuwepo enzi hizo kulikuwa na vikundi vya watu vilivyojipatia umaarufu Kwa kutoa Watu Uchawi legend wao akiwa Mzee MajiMarefu, kuna wale manyaunyau. Basi Watu wa namna hiyo wakaitwa ati wa mtoa Uchawi Yule Mama. Lile kundi maarufu Kutoka Shambalai liliwatoa Watu Uchawi makumi Kwa manma katika mji wetu.
" Wachawi wanawanga wanga ..wachawi(wanawanga wanga) × 3
Siondoki nangojea pembe siondokixl"
Ilikuwa moja ya nyimbo za kuongoza ibada ya kutoa Uchawi Watu.
Na wengi walitolewa uchawi. Lakini Taikon Baada ya kukua miaka mingi ikiwa imepita, najiuliza je ni kweli Yale matukio yanaukweli wowote?
Baada ya kukua nimegundua ule ulikuwa ni ushenzi mkubwa, na ulikuwa ni Uongo na uzushi unyanyasaji.
Ile hadithi ya kusema Yule Mama wa vitumbua alikuwa anakorogea uji wa vitumbua kwa Kutumia mkono wa mtoto Mdogo aliyekwisha Kufa ulikuwa ni Uongo Mkubwa.
Wivu na husda Kwa mahasimu wake wa kibiashara ndio waliomuundia njama ya kulichafua jina lake na kuiangusha biashara yake.
Hata wale Watu wa manyaunyau watoa Uchawi nao kumbe ilikuwa ni njama na mbinu za Watu wenye Chuki ambao walifanya hila kuwachafua baadhi ya Watu huku wakitumia mazingaombwe ya kitoto ya hila
Hayo mambo ili yakuingie akilini itakupasa uwe mjinga WA kiwango cha mwisho Kabisa au uwe mtoto Mdogo asiyeelewa mambo.
Nimekumbuka Zama za kale.
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam