Anakorogea uji wa vitumbua na mkono wa mtoto aliyekufa

Anakorogea uji wa vitumbua na mkono wa mtoto aliyekufa

Kuna kona moja ya mtaa mmoja pale Kariakoo enzi hizo akina mama walikuwa wanajipanga kuuza vitafunwa vya kila aina,akaja yule aliyekuwa Mbunge Akiitwa Maji Mafupi,alikuwa amefikia hotel moja karibu na Jangwani, akatangaza wale wamama wengi ni wachawi na pale wote wapo Uchi!.ghafra biashara za wamama zikaanza kudoda, Maji Mafupi alikuwa maarufu sana enzi hizo hotel aliyokuwa anafikia ilikuwa inafurika watu kutibiwa...
 
Kwema wazee.

Yule Mama alikuwa muuza vitumbua, alikuwa maarufu Kwa vitumbua vyake kwani vilikuwa vitamu Sana. Kwa Siku alikuwa anauza ndoo Mbili.
Zikaja Stori kuwa Yule Bi.mkubwa ni mlozi, kikagula, jichawi lililoshindikana.

Bado nakumbuka, wakaitwa Wale watoa Uchawi, Kwa mliokuwepo enzi hizo kulikuwa na vikundi vya watu vilivyojipatia umaarufu Kwa kutoa Watu Uchawi legend wao akiwa Mzee MajiMarefu, kuna wale manyaunyau. Basi Watu wa namna hiyo wakaitwa ati wa mtoa Uchawi Yule Mama. Lile kundi maarufu Kutoka Shambalai liliwatoa Watu Uchawi makumi Kwa manma katika mji wetu.
" Wachawi wanawanga wanga ..wachawi(wanawanga wanga) × 3
Siondoki nangojea pembe siondokixl"
Ilikuwa moja ya nyimbo za kuongoza ibada ya kutoa Uchawi Watu.

Na wengi walitolewa uchawi. Lakini Taikon Baada ya kukua miaka mingi ikiwa imepita, najiuliza je ni kweli Yale matukio yanaukweli wowote?

Baada ya kukua nimegundua ule ulikuwa ni ushenzi mkubwa, na ulikuwa ni Uongo na uzushi unyanyasaji.

Ile hadithi ya kusema Yule Mama wa vitumbua alikuwa anakorogea uji wa vitumbua kwa Kutumia mkono wa mtoto Mdogo aliyekwisha Kufa ulikuwa ni Uongo Mkubwa.
Wivu na husda Kwa mahasimu wake wa kibiashara ndio waliomuundia njama ya kulichafua jina lake na kuiangusha biashara yake.
Hata wale Watu wa manyaunyau watoa Uchawi nao kumbe ilikuwa ni njama na mbinu za Watu wenye Chuki ambao walifanya hila kuwachafua baadhi ya Watu huku wakitumia mazingaombwe ya kitoto ya hila

Hayo mambo ili yakuingie akilini itakupasa uwe mjinga WA kiwango cha mwisho Kabisa au uwe mtoto Mdogo asiyeelewa mambo.

Nimekumbuka Zama za kale.

Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Robert hujawahi oa mwanamke anakulaza na fisi halafu yeye anaenda kuwanga hadi usiku mwingi anarudi!!?

ilimtokea mjomba hii na baby akasanuka siku ya arobaini ya mwizi ilipofika tu kasheshe kitaa Binge la fisi lenye heleni lilitoka ndani wakati mke wake akiwa uchi wa mnyama hadharani saa nne asubuhi!!!

maisha hayo!!
 
Haya mambo yapo kitambo sana. Kuna wauza pombe za kienyeji nao wana mauzauza ya kusadikika kuwa baadhi ya vyombo vyao ni mafuvu ya wafu, kwa mama lishe nako hawaaminiki, inasemwa nao hukaa uchi wakati wanapika ili vyakula vyao viwe vitamu, utamu kama ile kitu iliyotengwa wazi. Ukiwahoji wengi hukiri kwenda kwa waganga kunuwiziwa wafanikiwe kuliteka soko la vyakula vyao. Wapo wanaodai waganga hutaka 'kuwaonjea mpiko' kwanza ndio wawahudumie. Wapo wanaoshindwa masharti na kutoroka kwa waganga, ndio hawa wanaotoa siri za huko walikokwenda kutafuta 'dawa'
 
Ujinga kama huu nchi zenye viongozi wanaojitambua wasingekubali ufanyike.

Fikiria umeikuza biashara kwa jasho na damu anakuja punguani mmoja kavaa kaniki yake na mkononi kashika usinga anakuchafua kwa kuwaambia watu huyu anauza sana kwa sababu anakorogea uji kwa mkono wa mtoto.

Ukitoka hapo ushapoteza wateja ushapoteza heshima na huyo mjinga aliyefanya hivyo anatamba tu mtaani.
Yah,
Sema ubaya, imani kama hizi huwa zinachukua mda kupotea, mpaka sasa bado kuna kundi kubwa la watu linaamini
Hata wazungu kuna karne walikua wanawa choma wenzao moto kwa imani hizi hizi za uchawi, mpaka baadae walipo elimika wakaacha

Huwa ni ujinga na kukosa critical thinking
 
Ujinga kama huu serikali ilikuwa inauruhusu tu.

Waganga wanapita nyumba kwa nyumba watu nyomi wanawafata nyuma eti unakuja kutolewa vitu.

Ukiwa hauna pesa za kuwapa waganga watu wanakuchangia(ili uaibike)

Binafsi nilikuwa nashangaa sana kivipi serikali inaruhusu watu kudhalilishana na kushushiana utu.
Serikali ilikuwa imejaa wajinga wengi sana. Na bado wengine wapo. Na haya mambo huko vijijini bado yapo. Serikali ikizuia "miwananchi" inaandamana eti manyaunyau aachwe afanye kazi yake.
 
Robert hujawahi oa mwanamke anakulaza na fisi halafu yeye anaenda kuwanga hadi usiku mwingi anarudi!!?

ilimtokea mjomba hii na baby akasanuka siku ya arobaini ya mwizi ilipofika tu kasheshe kitaa Binge la fisi lenye heleni lilitoka ndani wakati mke wake akiwa uchi wa mnyama hadharani saa nne asubuhi!!!

maisha hayo!!

99% mambo hayo ni Fix Mkuu.
Ingawaje sijasema hayapo,

Sisi waigizaji na waandaaji WA hayo matukio ndio tunawaambia. Ni matukio ya kutengeneza tuu
 
Hv wazungu na wao Wana Hz mambo , kiukwel haya mambo Kwa Africa yapo Sana , yaani tunapeana huduma katika mazingira ya kisenge Sana , sio Tu mkono wa mtoto wengine wanaloweka chupi kwenye maji ya kupikia au kukandia ngano Kwa kutumia matako ...daah mazingira yetu ni hatarishi Sana haya mambo hapo live live , ukianza kufanya biashara utaona watu wanakufata kabisa wanakueleza Mzee tengeneza kamati ( kuroga )
 
Haya mambo yapo kitambo sana. Kuna wauza pombe za kienyeji nao wana mauzauza ya kusadikika kuwa baadhi ya vyombo vyao ni mafuvu ya wafu, kwa mama lishe nako hawaaminiki, inasemwa nao hukaa uchi wakati wanapika ili vyakula vyao viwe vitamu, utamu kama ile kitu iliyotengwa wazi. Ukiwahoji wengi hukiri kwenda kwa waganga kunuwiziwa wafanikiwe kuliteka soko la vyakula vyao. Wapo wanaodai waganga hutaka 'kuwaonjea mpiko' kwanza ndio wawahudumie. Wapo wanaoshindwa masharti na kutoroka kwa waganga, ndio hawa wanaotoa siri za huko walikokwenda kutafuta 'dawa'

Ni Uongo Mkubwa uliokubalika
 
Bahati mbaya kuna wanaoamini ujinga hivyo wanalisha wenzao uchafu kweli kwamba biashara itakuwa nzuri.

Kuna mjinga mmoja alienda kuchanjwa chale akafungua bucha. Miezi miwili akafunga maana akipata pesa kidogo full showoff.
 
Hv wazungu na wao Wana Hz mambo , kiukwel haya mambo Kwa Africa yapo Sana , yaani tunapeana huduma katika mazingira ya kisenge Sana , sio Tu mkono wa mtoto wengine wanaloweka chupi kwenye maji ya kupikia au kukandia ngano Kwa kutumia matako ...daah mazingira yetu ni hatarishi Sana

Tatizo ni kuwa hvyo vitu ni Stori tuu za kubuni kama zile ninazotungaga
 
Kuna kona moja ya mtaa mmoja pale Kariakoo enzi hizo akina mama walikuwa wanajipanga kuuza vitafunwa vya kila aina,akaja yule aliyekuwa Mbunge Akiitwa Maji Mafupi,alikuwa amefikia hotel moja karibu na Jangwani, akatangaza wale wamama wengi ni wachawi na pale wote wapo Uchi!.ghafra biashara za wamama zikaanza kudoda, Maji Mafupi alikuwa maarufu sana enzi hizo hotel aliyokuwa anafikia ilikuwa inafurika watu kutibiwa...

😂😂😂
 
Tatizo ni kuwa hvyo vitu ni Stori tuu za kubuni kama zile ninazotungaga
Haya mambo yapo Mzee wala sio story mi niliamin hayapo Ila nimeshuhudia yapo , sema Mimi siamini katika huo mlengo , Ila nakubali yapo na watu wanafanya
 
Haya mambo yapo Mzee wala sio story mi niliamin hayapo Ila nimeshuhudia yapo , sema Mimi siamini katika huo mlengo , Ila nakubali yapo na watu wanafanya

Nakuambia hivi hiyo ni Michezo ya kuigiza tuu. Hakuna kitu kama hicho.
Kulikuwa na Mzee mmoja alikuwa Baba WA Rafiki yangu, yeye alikuwa mganga na Gwiji wa Uchawi. Yeye mwenyewe anakiri kuwa hiyo ni Michezo ya kuigiza, mazingaombwe.

Ni Sawa na ishu ya msukule au kuzika mgomba, ni Uongo WA Hali ya juu ambao Watu waliamini kuukubali
 
Maji marefu hakuwa lolote zaidi ya utapeli uliopindukia..alipeleka gari yake anayoipenda kwa fundi fulani maeneo fulani..
Yule fundi alimbadlishia spea zote nzima akamuekea feki na gari haikutembea na maji marefu alikuja na kuanza kupigana ngumi na yule jamaa!!akapigwa akaona aibu akaondoka hata polisi hakwenda.na yule jamaa yupo hadi sasa hivi na gerej yake amezeeka tuu.
 
Back
Top Bottom