Anakorogea uji wa vitumbua na mkono wa mtoto aliyekufa

Anakorogea uji wa vitumbua na mkono wa mtoto aliyekufa

Ujinga kama huu nchi zenye viongozi wanaojitambua wasingekubali ufanyike.

Fikiria umeikuza biashara kwa jasho na damu anakuja punguani mmoja kavaa kaniki yake na mkononi kashika usinga anakuchafua kwa kuwaambia watu huyu anauza sana kwa sababu anakorogea uji kwa mkono wa mtoto.

Ukitoka hapo ushapoteza wateja ushapoteza heshima na huyo mjinga aliyefanya hivyo anatamba tu mtaani.
Hawa jamaa mjomba wangu aliwatoa baru. Enzi hizo watu wenye bunduki ni wachache. Kijijini huko.. Eti mvua imekataa kunyesha wanasema yeye ndiye anaizuia isinyeshe kwa uchawi wake. Wakamleta ''manyaunyau'' atoe uchafu. Ikapigwa risasi moja hewani pwaa.. watu wakakimbia kama wale nguruwe walioingiwa na mapepo kwenye biblia.
 
Kama una biashara kubwa lazima uundiwe zengwe na masikini au washindani wako.

Walikuja watu wa kujiita lambalamba mtaani kwetu, wale jamaa walikua wanakula bia bure, wanakula wake za watu hadharani, wanakula madem hovyo.
Kama kawaida wanawake wanavyopenda kutumia hisia, wao ndio waliwafinance sana hao watu.
Zilichangishwa pesa kila duka, kila nyumba eti hao walozi wafanye ulozi.

Wale jamaa walikua waongo wa waziwazi, ajabu watu sijui salipigwa upofu hata hawaoni aisee.

Wajinga Ni vipofu siku zote.
Sasa tuna kina lambalamba Huko makanisani
 
Mengine ni uongo na mengine ni ukweli, waswahili wanasema lisemwalo lipo, nimefanya uchunguzi binafsi nimegundua kweli wapo ambao wanafanya biashara za vyakula, wanatumia uchawi wa kuweka vitu vichafu kwenye chakula, ili kuvuta wateja, hata sokoni nyama za buchani nyingi si halisi Robert Heriel Mtibeli Grahams

Buchani nyama sio halisi?
Hapo ndio patamu,
 
Ilishatokea lilipokuwa duka letu mjini hpa picha linaanza raia wanatutuhumu ushirikina, siwakachangishna wakamleta manyaunyau, raia ka ote.
Picha linaanza manyaunyau ana paka akaomba apewe unga na kisu raia hao dukani tupimie unga nikawajibu tu hatuwezi kutoa unga kwajili ya ushirikina, raia yoweee...... leo huku wanakazia Leo! lzma mnase tu ukaenda kutafutwa unga na kisu wakaleta unaambiwa acha manyaunyau apige mkwara wa hja mwisho akuteletea kiini macho kumng'ta pka shngoni na kuzuga kumnyonya damu mar ooh eti hpa pazito twendeni kwanza

😂😂😂
Wabongo ukiwazidi Akili na Pesa utaitwa mchawi
 
Siamini mambo ya uchawi kabisa, ila Kuna mama alikua anapika chakula Hana mfanyakazi, aisee unakuta mibaba imepanga foleni inagombania chakula, afu sahani zikiisha unaosha mwenyewe unapanga foleni na hela kulipa ni cash, Kuna jamaa zangu wameosha sana sahani pale na ni watu na heshima zao, aisee hii kitu haijawahi kunitoka kichwani
Mkuu ile story ya utapeli ulimalizia kweli???
 
Ndio maana zikaitwa "imani" za kishirikina, maana yake hili ni suala la kuamini na wala siyo lazima iwe ni ukweli(facts). Madhara ya uchawi hayatokani na wachawi wanaodhaniwa kuloga hapana, bali madhara makubwa na hatari kabisa hutokana na wale wanaoamini kuwa kuna uchawi. Kwa mfano utakuta jitu likishaaminishwa kwamba kiungo cha albino kina uwezo wa kumfanya mtu awe tajiri, basi utakuta jitu hilo kwa ujinga wake kweli linakwenda kumtafuta albino wa watu maskini asiyekuwa na hatia yeyote na kumuua au kumkata kiungo.

Halikadhalika kwa vile mganga mpuuzi kamuaminisha mtu eti akiloweka nguo chafu ya ndani katika mchuzi wa ugali wateja watakuja lukuki, basi mtu huyo kwa ujinga wake kweli anakwenda kuwalisha watu uchafu wa ajabu usioelezeka. Waafrika nasisi tuache kushabikia mambo ya kishirikina yasiyokuwa na ushahidi wowote zaidi ya speculations tu sisizokuwa na kichwa wala miguu na mbaya zaidi si waganga tu wanaoshadidia mambo haya bali hata baadhi ya viongozi wa dini nao wamekuwa chanzo kikubwa cha kupandikiza imani hizi ndani ya waumini wenye uelewa mdogo kwa faida zao binafsi hasa za kiuchumi.
 
Wale mabwana walikuwa washenzi sana. Na akili za watanzania zilikuwa finyu katika kuchanganua mambo. Wale walikuwa wakiitwa lambalamba au rambaramba Kila nyumba lazima watoe chupa imefungwa vitambaa vyekundu na vyeupe Yan rangi mixer.

Kumbe ilikuwa janja janja tu mmoja anajifanya kapandisha mashetani anasema hapa Kuna kitu anachinjwa kuku au mbuzi ili kutoa hicho kitu.

Ila vile vitu walikuwa wanakuja navyo wanavizika hapo hapo na kuvitoa hapo hapo

Walikuwa wanakula Hela za Bure Kila nyumba 1,500/✓ au 2,000 tsh pamoja na kuku.

Walikuwa ni lazima Kijiji kizima waingie na Kila nyumba.

Na kwa mfano ukikataa nyumba yako wasifike basi pale kijijin wanakuona ww ni mchawi kwann hutaki nyumba yako ikaguliwe.!????


Kuna masheikh walikuwa wanakataa hawa washirikina wasifanye ushenzi wao katika nyumba zao ila wanakijiji wakawa wanaona masheikh ndio wachawi

Basi wale jamaa walinenepa kwa kuku WA dhuluma .ila kumbe ilikuwa ni mpango tu maalumu WA kuwapiga watu Hela .....


Ila jamaa hawakujulikana hata wamepotelea wapi na uzushi wao wale washirikina.

Ujinga mzigo!!!!!
 
Kwema wazee.

Yule Mama alikuwa muuza vitumbua, alikuwa maarufu Kwa vitumbua vyake kwani vilikuwa vitamu Sana. Kwa Siku alikuwa anauza ndoo Mbili.
Zikaja Stori kuwa Yule Bi.mkubwa ni mlozi, kikagula, jichawi lililoshindikana.

Bado nakumbuka, wakaitwa Wale watoa Uchawi, Kwa mliokuwepo enzi hizo kulikuwa na vikundi vya watu vilivyojipatia umaarufu Kwa kutoa Watu Uchawi legend wao akiwa Mzee MajiMarefu, kuna wale manyaunyau. Basi Watu wa namna hiyo wakaitwa ati wa mtoa Uchawi Yule Mama. Lile kundi maarufu Kutoka Shambalai liliwatoa Watu Uchawi makumi Kwa manma katika mji wetu.
" Wachawi wanawanga wanga ..wachawi(wanawanga wanga) × 3
Siondoki nangojea pembe siondokixl"
Ilikuwa moja ya nyimbo za kuongoza ibada ya kutoa Uchawi Watu.

Na wengi walitolewa uchawi. Lakini Taikon Baada ya kukua miaka mingi ikiwa imepita, najiuliza je ni kweli Yale matukio yanaukweli wowote?

Baada ya kukua nimegundua ule ulikuwa ni ushenzi mkubwa, na ulikuwa ni Uongo na uzushi unyanyasaji.

Ile hadithi ya kusema Yule Mama wa vitumbua alikuwa anakorogea uji wa vitumbua kwa Kutumia mkono wa mtoto Mdogo aliyekwisha Kufa ulikuwa ni Uongo Mkubwa.
Wivu na husda Kwa mahasimu wake wa kibiashara ndio waliomuundia njama ya kulichafua jina lake na kuiangusha biashara yake.
Hata wale Watu wa manyaunyau watoa Uchawi nao kumbe ilikuwa ni njama na mbinu za Watu wenye Chuki ambao walifanya hila kuwachafua baadhi ya Watu huku wakitumia mazingaombwe ya kitoto ya hila

Hayo mambo ili yakuingie akilini itakupasa uwe mjinga WA kiwango cha mwisho Kabisa au uwe mtoto Mdogo asiyeelewa mambo.

Nimekumbuka Zama za kale.

Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ila manyaunyau sikuwai muelewa na ile style yake ya kung’ata paka.
 
Wale mabwana walikuwa washenzi sana. Na akili za watanzania zilikuwa finyu katika kuchanganua mambo. Wale walikuwa wakiitwa lambalamba au rambaramba Kila nyumba lazima watoe chupa imefungwa vitambaa vyekundu na vyeupe Yan rangi mixer.

Kumbe ilikuwa janja janja tu mmoja anajifanya kapandisha mashetani anasema hapa Kuna kitu anachinjwa kuku au mbuzi ili kutoa hicho kitu.

Ila vile vitu walikuwa wanakuja navyo wanavizika hapo hapo na kuvitoa hapo hapo

Walikuwa wanakula Hela za Bure Kila nyumba 1,500/✓ au 2,000 tsh pamoja na kuku.

Walikuwa ni lazima Kijiji kizima waingie na Kila nyumba.

Na kwa mfano ukikataa nyumba yako wasifike basi pale kijijin wanakuona ww ni mchawi kwann hutaki nyumba yako ikaguliwe.!????


Kuna masheikh walikuwa wanakataa hawa washirikina wasifanye ushenzi wao katika nyumba zao ila wanakijiji wakawa wanaona masheikh ndio wachawi

Basi wale jamaa walinenepa kwa kuku WA dhuluma .ila kumbe ilikuwa ni mpango tu maalumu WA kuwapiga watu Hela .....


Ila jamaa hawakujulikana hata wamepotelea wapi na uzushi wao wale washirikina.

Ujinga mzigo!!!!!

Hatari Sana.
Kwa sasa lambalamba wapo Kanisani
 
Back
Top Bottom