Anaomba ushauri: Akubali kuwa mke wa pili au asubiri atapata mume wake?

Anaomba ushauri: Akubali kuwa mke wa pili au asubiri atapata mume wake?

Mimi mstaarabu

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
262
Reaction score
577
Nina rafiki yangu kwasasa ametimiza miaka 25 lakini wadogo zake wameolewa ambao ni watoto wa mjomba ake sasa yeye kwa sasa anafanya kazi hizi za kujitolea katika shirika X kwahiyo kuna muda anakua anatamani kuwa na mume au mchumba ambaye ana nia ya kumuoa sasa the bad thing ni kwamba hana mchumba ambaye yupo serious kwahiyo anajiona yupo singo tu kwasababu hajawahi kutolewa barua, Na umri unaenda watu wanamwambia ukichelewa kuzaa utapata tabu.

Kwahiyo hivi karibu amekua akipata watu kumtongoza ila MUME ZA WATU NA anasema kuna mmoja yupo serious anataka kumuoa ila anaogopa kwao watamshangaa kwasababu umri wake kuingia ndoa ya matala ni kitu kigumu. Na pia huyo mwanaume ana umri wa miaka 41.

Anaomba ushauri je asubiri tu azidi kuomba mungu agampa kijana mwenzie au akubali kuolewa ndoa ya uke wenza??
 
Ndoa zitawapa uchizi zama hizi, kuna ma cousin wawili wapo late 20's walikuwa slay queens miaka hii 3 iliyopita, ila kwa sasa wanahaha na kuolewa mmoja kashaanza na kwenda kwa waganga, mwingine huyo ni anatembelea na kusalimia kila ndugu anaamini huko huenda akapata mume, ni sarakasi tupu
 
Kuwa mke wa pili au watatu au wanne, hakuna neno. Tena wahi haraka sana.


Hata takwimu za Tanzania zinaunga mkono hilo, wanawake wengi kuliko wanaume.

Na wanaume wenyewe ndiyo hao wa arkisusi, supu za pweza na vumbi la kongo. Wengine kibao ni upinde, wanatamani waolewe wao.
 
Nina rafiki yangu kwasasa ametimiza miaka 25 lakini wadogo zake wameolewa ambao ni watoto wa mjomba ake sasa yeye kwa sasa anafanya kazi hizi za kujitolea katika shirika X kwahiyo kuna muda anakua anatamani kuwa na mume au mchumba ambaye ana nia ya kumuoa sasa the bad thing ni kwamba hana mchumba ambaye yupo serious kwahiyo anajiona yupo singo tu kwasababu hajawahi kutolewa barua , Na umri unaenda watu wanamwambia ukichelewa kuzaa utapata tabu.

Kwahiyo hivi karibu amekua akipata watu kumtongoza ila MUME ZA WATU NA anasema kuna mmoja yupo serious anataka kumuoa ila anaogopa kwao watamshangaa kwasababu umri wake kuingia ndoa ya matala ni kitu kigumu. Na pia huyo mwanaume ana umri wa miaka 41.

Anaomba ushauri je asubiri tu azidi kuomba mungu agampa kijana mwenzie au akubali kuolewa ndoa ya uke wenza??
Kiswahili mara nyengine kinashangaza kweli! Sasa unaposema "anafanya kazi za kujitolea katika shirika X kwahiyo kuna muda anakua anatamani kuwa na mume " una maanisha hizo kazi ndizo zinazomsababisha atamani mume? Kazi gani hasa anazofanya?😉
 
Khaa, miaka25 ana udogo gani?


Huu ushauri siyo mwema kabisa, napingana nao.
Asubiri subiri walau afike miaka 32 huku akiongeza kipato chake.

Nje ya mada Mkuu, wewe uliolewa ukiwa na Umri gani?

Wanasema wakati sahihi ni wakati wa Bwana Mungu 🙏
 
Back
Top Bottom