Nina rafiki yangu kwasasa ametimiza miaka 25 lakini wadogo zake wameolewa ambao ni watoto wa mjomba ake sasa yeye kwa sasa anafanya kazi hizi za kujitolea katika shirika X kwahiyo kuna muda anakua anatamani kuwa na mume au mchumba ambaye ana nia ya kumuoa sasa the bad thing ni kwamba hana mchumba ambaye yupo serious kwahiyo anajiona yupo singo tu kwasababu hajawahi kutolewa barua, Na umri unaenda watu wanamwambia ukichelewa kuzaa utapata tabu.
Kwahiyo hivi karibu amekua akipata watu kumtongoza ila MUME ZA WATU NA anasema kuna mmoja yupo serious anataka kumuoa ila anaogopa kwao watamshangaa kwasababu umri wake kuingia ndoa ya matala ni kitu kigumu. Na pia huyo mwanaume ana umri wa miaka 41.
Anaomba ushauri je asubiri tu azidi kuomba mungu agampa kijana mwenzie au akubali kuolewa ndoa ya uke wenza??
Mimi sio muislam lakini siwezi kumshauri msichana kuwa mke wa pili wa mtu. Vilevile nashauri asikimbilie kuolewa haraka ajiendeleze kama ni elimu au biashara kwanza akae vizuri. Mwenye wawili kesho atataka watatu kesho kutwa wanne🤔 kuweni makini kufuata mkumbo.
Usikokuwa makini utakuwa umeachika ukifika 30 na watoto halafu kutafuta mume hapo itakuwa ngumu zaidi. Ni bora uwe 30 single na maisha yanaeleweka🤔