Anaomba Ushauri: Alisalitiwa na mume wake wakaachana, Mume akaoa na akapata Pesa. Maisha yamekuwa magumu anataka kuwa Mchepuko

Stupid🚮

Sasa wewe ndo ume justify kwanini huwa nawachamba humu.
Deleted01 Vishu Mtata Kisai
Mnabishaga mnasemaga mimi naongeaga negative tu. Mnaona sasa mawazo ya mwanaume mwenzenu yalivyo ya kipumbavu.

Eti mwanaume hata akichepuka napungukiwa nini. Hivi mnadhanigi wanawake hawana mioyo au. Mngekus mna nguvu za kiume basi za
Kuwaridhisha hao wake zenu na michepuko, mkeo nyumbanu hujui ksms karidhika au ls unaenda kuonesha ulemavu wako mitaani huko zipu hufungi kazi kupandisha gia mbovu.

Wake zenu wana wastahi sana na vilema vyenu tungesems hapa wanaume wasimame basi nyie mnaombwata mngejificha
Sawa mwenzenu kafanyia kazi mnayoyaubiri sasa analia njaa. Mpeni ajira
 
Habari wana Jukwaa,

Nataka kushiriki nanyi kisa changu. Mimi na mume wangu tulikuwa tunapendana sana, lakini kulikuwa na tatizo kubwa—hakuwa mwaminifu. Alikuwa akiendekeza wanawake wa nje ya ndoa yetu. Kwa kweli, nilijaribu kuvumilia hali hiyo, lakini mwisho wa siku, niliamua haiwezekani tena na tukatengana.

Niliondoka na watoto wetu, na nikaendelea na maisha yangu. Lakini, tangu nilipoondoka, mambo yamekuwa magumu sana kwangu. Hata hivyo, nimekuwa nikifuatilia maisha ya mume wangu wa zamani na kugundua kwamba anaishi vizuri sana. Alioa tena na sasa ana mtoto mwingine.

Jambo hili linaniumiza sana. Mara kwa mara najikuta nikijiuliza kama niliamua vizuri kuachana naye. Pengine kama ningevumilia, angebadilika na tungeweza kuwa na familia yenye furaha. Kwa upande mwingine, sitaki kurudisha watoto wangu ili walelewe na mama mwingine. Ni jambo gumu sana kwangu kuelewa kama nilifanya uamuzi sahihi au la. Imefika hatua natamani hata kuwa mchepuko kwa mume wangu ili maisha yaende.

Naomba ushauri wenu wana Jukwaa. Asanteni.
Wewe kwanza kabisa haukuwa na mapenzi ya dhati na mumeo. Kushindwa kutengeneza ndoa yako hadi ukaondoka ilikuwa ni upumbavu.
Secondly, sidhani kama unataka kurudi sababu unampenda mumeo wa zamani ila ni kwa sababu dhiki zinakuzidia.
My take, pambana sana ujikomboe hapo ulipo kwa juhudi zako. Kwa sababu kama ungefanikiwa juhudi zako usingemkumbuka mzazi mwenzako na kutamani kuwa mchepuko wake. Kwahyo hakuna namna, ushavuka mstari wa kujirudi, endelea tu na maisha yako. Mungu atakusaidia.
 
Habari wana Jukwaa,

Nataka kushiriki nanyi kisa changu. Mimi na mume wangu tulikuwa tunapendana sana, lakini kulikuwa na tatizo kubwa—hakuwa mwaminifu. Alikuwa akiendekeza wanawake wa nje ya ndoa yetu. Kwa kweli, nilijaribu kuvumilia hali hiyo, lakini mwisho wa siku, niliamua haiwezekani tena na tukatengana.

Niliondoka na watoto wetu, na nikaendelea na maisha yangu. Lakini, tangu nilipoondoka, mambo yamekuwa magumu sana kwangu. Hata hivyo, nimekuwa nikifuatilia maisha ya mume wangu wa zamani na kugundua kwamba anaishi vizuri sana. Alioa tena na sasa ana mtoto mwingine.

Jambo hili linaniumiza sana. Mara kwa mara najikuta nikijiuliza kama niliamua vizuri kuachana naye. Pengine kama ningevumilia, angebadilika na tungeweza kuwa na familia yenye furaha. Kwa upande mwingine, sitaki kurudisha watoto wangu ili walelewe na mama mwingine. Ni jambo gumu sana kwangu kuelewa kama nilifanya uamuzi sahihi au la. Imefika hatua natamani hata kuwa mchepuko kwa mume wangu ili maisha yaende.

Naomba ushauri wenu wana Jukwaa. Asanteni.
Nakuhurumia kwa hizi comment!
Wengine wapuuzee usitilie maana kila comment utakufa bure
 
Stupid🚮

Sasa wewe ndo ume justify kwanini huwa nawachamba humu.
Deleted01 Vishu Mtata Kisai
Mnabishaga mnasemaga mimi naongeaga negative tu. Mnaona sasa mawazo ya mwanaume mwenzenu yalivyo ya kipumbavu.

Eti mwanaume hata akichepuka napungukiwa nini. Hivi mnadhanigi wanawake hawana mioyo au. Mngekua mna nguvu za kiume basi za
Kuwaridhisha hao wake zenu na michepuko, mkeo nyumbani hujui kama karidhika au la unaenda kuonesha ulemavu wako mitaani huko zipu hufungi kazi kupandisha gia mbovu.

Wake zenu wana wastahi sana na vilema vyenu tungesema hapa wanaume wasimame basi nyie mnaombwata mngejificha

Kuchepuka ni jambo baya kwa wote huyo anae sema hivyo anakosa sifa ya uanaume. Nakuachia umalizane naye.
 
Habari wana Jukwaa,

Nataka kushiriki nanyi kisa changu. Mimi na mume wangu tulikuwa tunapendana sana, lakini kulikuwa na tatizo kubwa—hakuwa mwaminifu. Alikuwa akiendekeza wanawake wa nje ya ndoa yetu. Kwa kweli, nilijaribu kuvumilia hali hiyo, lakini mwisho wa siku, niliamua haiwezekani tena na tukatengana.

Niliondoka na watoto wetu, na nikaendelea na maisha yangu. Lakini, tangu nilipoondoka, mambo yamekuwa magumu sana kwangu. Hata hivyo, nimekuwa nikifuatilia maisha ya mume wangu wa zamani na kugundua kwamba anaishi vizuri sana. Alioa tena na sasa ana mtoto mwingine.

Jambo hili linaniumiza sana. Mara kwa mara najikuta nikijiuliza kama niliamua vizuri kuachana naye. Pengine kama ningevumilia, angebadilika na tungeweza kuwa na familia yenye furaha. Kwa upande mwingine, sitaki kurudisha watoto wangu ili walelewe na mama mwingine. Ni jambo gumu sana kwangu kuelewa kama nilifanya uamuzi sahihi au la. Imefika hatua natamani hata kuwa mchepuko kwa mume wangu ili maisha yaende.

Naomba ushauri wenu wana Jukwaa. Asanteni.
Ni kama hii story inanihusu, japo sikuwa na michepuko ila nilibambikiwa sana hilo jambo.

Any way, it was over and never, no retreat. Tafta maisha mengine, ninachoona hapo unamfikiria kwa kuwa amegrow kifedha, je angekuwa na maisha ya shida ungemfikiria?? Wewe humpendi, unapenda pesa yake tu, jaribu maisha mengine maana utaenda kujiongezea stress kibao
 
Pole sana,
Umeshindwa kuvumilia changamoto zake za kimaisha sasa unataka kurudi kwa mlango wa nyuma!!!
Pole,
 
Nani kakwambia anakutaka bado??? Unajua trauma aliyoipata ulivyo muacha ukaondoka na watoto ??? Kama ulishaamua kuondoka why unamfuatilia maisha yake. so angekuwa ame lost kimaisha sindo ungemsema umalaya ndo maana amefilisika sasa hivi?
 
Inawezekana kabisa wewe ndiye ukiyekuwa nyota ya giza kwake. Na ulipoondoka akapata mke mwenye nyota ya nuru na riziki. Sasa imemng'arisha na mambo yako safi. Ni afadhali sana ulivyoondoka. Ungeendelea kubaki maisha yenu yangeliendelea kuwa magumu zaidi. Na ikiwa utarudi ktk maisha yake kwa njia yoyote ile utasababisha arudi kule mlipotoka na mwishowe ashindwe hata kutoa matunzo ya watoto. Kaa naye mbali. Peleka gundu lako baharini.
Labda nijue hili Uliondika kwa sabau ya bwana ni Fuska na unataka kurudi akiwa bado Fuska mbona kama hujabadili kitu? Hebu waache wenzio iwapo uko na nia ya kuboresha maisha JIFUNZE siyo kurudi kule
 
# ROCA FELLA

POLE SANA HIYO NI CHANGAMOTO LAKINI USIPATE AIBU WALA KUJENGA HOFU TULIA NA WATOTO WAKO ENDELEA KUMWOMBA MWENYEZI MUNGU AKUSAIDIE NA HAKIKA KWA IMANI YAKO DHABITI MUDA MWAFAKA MOLA MLEZI ATAKUBARIKI NA KUKUTENDEA MIUJIZA.
 
Sio kila unachotamani kitakua,akili za wanawake bhana eti natamani kuwa mchepuko km vile jamaa bado anamuwazia,utakua na majuto mangap ewe mwanamke,leave the past where it belongs move on kuna neema yako mbele acha kuwaza ujinga
Km alikua na wanawake wengne kumuacha ulikua ni uamuz sahihi,so we endelea kukaza tu utafanikiwa,hao watoto wakutie nguvu za kutafuta kila inapoanza siku mpya
Mleta mada ishi hapa.

Fata hiki ulichoambiwa hapa, aliyoyasema mkuu yote ni sahihi kwa 100%.
 
Pole sana mkuu.
Its so sad
Yan bora ukamwombe mtaji wa biashara au ukamwombe awe hata anakushika mkono pindi upitiapo magumu maana kuwa mchepuko kuna hatari yake tena kubwa tu
 
Back
Top Bottom