Anaomba Ushauri: Alisalitiwa na mume wake wakaachana, Mume akaoa na akapata Pesa. Maisha yamekuwa magumu anataka kuwa Mchepuko

Sawa mwenzenu kafanyia kazi mnayoyaubiri sasa analia njaa. Mpeni ajira
 
Wewe kwanza kabisa haukuwa na mapenzi ya dhati na mumeo. Kushindwa kutengeneza ndoa yako hadi ukaondoka ilikuwa ni upumbavu.
Secondly, sidhani kama unataka kurudi sababu unampenda mumeo wa zamani ila ni kwa sababu dhiki zinakuzidia.
My take, pambana sana ujikomboe hapo ulipo kwa juhudi zako. Kwa sababu kama ungefanikiwa juhudi zako usingemkumbuka mzazi mwenzako na kutamani kuwa mchepuko wake. Kwahyo hakuna namna, ushavuka mstari wa kujirudi, endelea tu na maisha yako. Mungu atakusaidia.
 
Nakuhurumia kwa hizi comment!
Wengine wapuuzee usitilie maana kila comment utakufa bure
 

Kuchepuka ni jambo baya kwa wote huyo anae sema hivyo anakosa sifa ya uanaume. Nakuachia umalizane naye.
 
Ni kama hii story inanihusu, japo sikuwa na michepuko ila nilibambikiwa sana hilo jambo.

Any way, it was over and never, no retreat. Tafta maisha mengine, ninachoona hapo unamfikiria kwa kuwa amegrow kifedha, je angekuwa na maisha ya shida ungemfikiria?? Wewe humpendi, unapenda pesa yake tu, jaribu maisha mengine maana utaenda kujiongezea stress kibao
 
Nachelea kusema kwamba unashida wewe
 
Pole sana,
Umeshindwa kuvumilia changamoto zake za kimaisha sasa unataka kurudi kwa mlango wa nyuma!!!
Pole,
 
Nani kakwambia anakutaka bado??? Unajua trauma aliyoipata ulivyo muacha ukaondoka na watoto ??? Kama ulishaamua kuondoka why unamfuatilia maisha yake. so angekuwa ame lost kimaisha sindo ungemsema umalaya ndo maana amefilisika sasa hivi?
 
Labda nijue hili Uliondika kwa sabau ya bwana ni Fuska na unataka kurudi akiwa bado Fuska mbona kama hujabadili kitu? Hebu waache wenzio iwapo uko na nia ya kuboresha maisha JIFUNZE siyo kurudi kule
 
# ROCA FELLA

POLE SANA HIYO NI CHANGAMOTO LAKINI USIPATE AIBU WALA KUJENGA HOFU TULIA NA WATOTO WAKO ENDELEA KUMWOMBA MWENYEZI MUNGU AKUSAIDIE NA HAKIKA KWA IMANI YAKO DHABITI MUDA MWAFAKA MOLA MLEZI ATAKUBARIKI NA KUKUTENDEA MIUJIZA.
 
Mleta mada ishi hapa.

Fata hiki ulichoambiwa hapa, aliyoyasema mkuu yote ni sahihi kwa 100%.
 
Pole sana mkuu.
Its so sad
Yan bora ukamwombe mtaji wa biashara au ukamwombe awe hata anakushika mkono pindi upitiapo magumu maana kuwa mchepuko kuna hatari yake tena kubwa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…