Anaomba Ushauri: Alisalitiwa na mume wake wakaachana, Mume akaoa na akapata Pesa. Maisha yamekuwa magumu anataka kuwa Mchepuko

Umemaliza 🙌
 
Hivi Mwanaume ambae anapitia hali ya kukosa kipato akichepuka wewe mke unapoteza nini?
Si umuombee tu anakochepukia iwe salama?!

Sijui mnatafutaga visingizio, sababu za kuachana sababu anakuwa amefulia?!

Haya sasa Mungu nae si Athumani, amemwinua Tena amempa riziki mantashaal 👌👌
Aibu yako @ bibie 😆😆😆
 
Muulize ujumbe ulifika?
 
Hizi takwimu za wanawake wengi kwenye ndoa kuishi kama wajane umetoka nazo wapi? [emoji848] Me nadhani ni muda muafaka sasa ukaacha kutunga taarifa zako.
 
Hivi wanawake huwa mnatatizo na wanaume kuwa na mwanamke mwingine kwa sababu zipi za msingi?


Hebu nilistie hizo sababu hapa nataka kujua kutoka kwako.

Kwa maana wanawake asilimia kubwa nimegundua mnapenda kuwa na reactions na tabia za kiume. Yaani hampogo serious na kile mnachokisema au kukizungumzia.

Je, wewe kama mwanamke hebu niwekee hapa list ya sababu. Kwasababu nikitazama Dini haijabatilisha mwanaume kuwa na mke zaidi ya m'moja ila imebatilisha mwanamke kuwa na mwanaume zaidi ya m'moja.

Wewe nipe hapa sababu hata 5 za msingi kwann mwanaume ni tatizo na sio ruhusa kuwa na mwanamke au wanawake nje ya mkewe, na mimi nitakupa sababu kwann mwanaume ana uhalali kuwa na mwanamke zaidi ya mkewe kwa mujibu wa wanavyoishi na kwann mwanamke ni kosa hata kuthubutu kumuwazia mwanaume mwingine kuwa anaweza kuwa na msaada sawa au wa kumkaribia mumewe? [emoji848]
 
Maajabu ni nini, Maajabu ni alieachana na jamaa kwasababu ya michepuko yeye sasa ndio anataka kuwa mchepuko, aisee. Anyways watu wa tafiti wanasema moja ya sababu yakuwa na single mothers wengi hapa Tz ni kwamba wanawake wengi wanaachana na jamaa zao ambao hawajaoa na wakiachana nao wanaenda kudate waume za watu…
 
Basi na wanaume wasio na kazi wala uwezo kimaisha waolewe. Kama mkombozi wa kiuchumi ni mwanaume😂 kusingekua na vilaza wa kiume usinichoshe
mwanaume anapotengena na mwanamke wake, m wanaume onaondoka man alone sasa nyie wenzetu mnaachwa na mzigo wa watoto(mara nyingi hiko hivyo) sasa auoni kunatofauti hapo
 
angekuwa hajajipata ungetamani kurudi? kama jibu siyo, endelea kupambania mechi zako utashinda na furaha utaipata?
 
Yaani yeye aliondoka kisa mume alichepu, leo hii anataka amchepushe mume wa mtu ili mkewe naye aondoke?
 
jibu zuri sana
 
Anawasha jeneretaaa..!!!
 
Umeyatimba mwenyewe, chakufanya mbane tu atunze watoto wake wakiwa kwako usijiaribu kumvunjia ndoa yake kwani ni wewe mwenyewe uliondoka kwake.
 
Hapo hakuna ushauri, atafute mwingine aliye vizuri
She is out of Soko 🤣 Maybe she can't

Ukiwa single mom harafu upate mtu makini maybe:
1. Ni mrembo hasaaaaaa
2. Ana michongo na ana mchango wa kifedha
3. Kajifunza lugha ya wanaume na anajua ku blend nao vyema kitabia ,maneno etc.
4. Rohon yuko fresh, either ndumba au Mungu
5.Mwanaume ni Simp man
6. Man ametokea ktk single mom familia na trauma zina msumbua kuona anawiwa kulea mwanamke.

Otherwise Kuishi na single mom , Kipengelee na watu wengi hawavitaki, Yuko hapo sabab imembidi.
 
Haya Sasa ndo madhara ya kufanya maamuzi kwa kukurupuka.

Mwenzio kasha move on wewe pambana tu na hali yako coz uliyataka mwenyewe.
 
Kwangu nitamshauri hivi:
1. Awekeze nguvu zake kwenye kujenga familia yake, wanawake huwa hawasikii mpaka akutane na kitu kizito. Yeye kuwa mchepuko haibadilishi dhana kwamba bado mwanaume ana familia yake.
2. Mwanaume kama anataka mchepuko basi atafute mwingine asipashe kiporo!
 
Hizi takwimu za wanawake wengi kwenye ndoa kuishi kama wajane umetoka nazo wapi? [emoji848] Me nadhani ni muda muafaka sasa ukaacha kutunga taarifa zako.
Unataka kuniambia wanaume wengi wanawapa wake zao ela za kujitunza? Mwanaume akishanunua mchele na maharage amemaliza. Wengine wanakwambia hawana hela, mke ndo anahangaika na familia. Hamuwezi kukubali ila hata wao humu wanasoma
 
Wewe kama unapenda kuwa na wanawake wengi si uoe? Waislam mbona wanaoa wengi tu. Ila mwanaume wa kikristo kama unajiona hujielewi na unatabia za mbwa acha kuoa endelea kusuuza rungu magonjwa yakikukuta tunakuzika unapumzika kwani hasara ya nani
 
mwanaume anapotengena na mwanamke wake, m wanaume onaondoka man alone sasa nyie wenzetu mnaachwa na mzigo wa watoto(mara nyingi hiko hivyo) sasa auoni kunatofauti hapo
Alokwambia watoto kwa mama ni mzigo nani? Si ndo mnakujaga kulalamika mnasema watoto hawanitaki wanamlilia mama yao. Wakifanikiwa wanahangaika kumtunza mama yao mnaishia kutoa laana tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…