Anaomba ushauri, tabia za mumewe zinamchanganya

Bi dentamol

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
1,018
Reaction score
2,130
Mdau (ke) yupo ndani ya ndoa kwa mwaka 1 Ila tabia ya mme wake inampa shida sana.

1). Jamaa mkimya sana akiamka asubuhi salamu anaaga anaenda kazini akirudi salamu anakaa kimya anakula ataangalia mpira kimya badae kulala ata bidada akimsemesha anajibu tu short then kimya Ila akija mgeni anaongea tu vizuri na kucheka.

2). Ndani hakuna kukaa kupanga labda maendeleo tufanye hiki ...jamaa anakazi na bidada anakazi,,, jamaa akipanga kufanya lake anafanya bila kumshirikisha bidada. Inampa shida bidada sababu nayeye akipata mshahara anashindwa achangie vp mfano ujenzi au maendeleo ya ndani anaishi kununua vitu let say vya ndani anataman wapange pamoja washirikiane ujenzi na maendeleo kwa pamoja.

3). Sex inaweza pita wiki or wk 2 hawajapeana kwa Sasa bidada mjamzito miez 4 hajaguswa tangu ujauzito una mwezi mmoja.

Bidada inamchanganya japo jamaa anahudumia vizuri familia, hawakukaa mda mrefu sana kwenye uchumba so hakumsoma vizuri.
 
Bidada inamchanganya japo jamaa anahudumia vizuri familia, hawakukaa mda mrefu Sana kwenye uchumba so hakumsoma vizuri
Siri kubwa imejificha hapa

Anyway, kwa kuwa hilo lilisharukwa basi tukubali limepita na tuliache, kwa sasa bidada ajue mumewe ni mtu wa aina gani na ajiandae kuishi nae kwa miaka 100 ijayo katika hali hiyo. Aji adjust fikra zake towards ndoa na asim compare jamaa na ma boiyfrendi wa zamani.

Ajue mume ndio huyo na ndio alivyo. Kwa kuwa jamaa hajalalamika kuomba kuchangiwa matumizi na maendeleo basi bidada atunze hela zake tu. Au kama ni lazima kuchangia maendeleo achangie tu ila asije akafanya siri.

Kama ni kiwanja nae anunue tu kisha amwambie mumewe au gari anunue tu alafu amwambie mumewe asimfiche kitu na mume akilalamika kwa nini hakushirikishwa basi ndio solution itapatikana kuanzia hapo maana watayaongea

Upande wa kukosa mkuyenge nashindwa cha kushauri aisee.
 
Mwambie bidada akaze buti huyo bwana ndio tabia yake na hawezi mgeuza. Aendelee kumheshimu na afanye wajibu wake kama mwanamke. Asiwe mtu wa kulalamika.

Atakacho aombe ... hata unyumba akijisikia aombe atapewa. Ajiwekee akiba na afanye mambo yake ya maendeleo bila kificho. Cha maana ni kuishi kwa amani. ajipe amani. Ogelea maji yanakoelekea, usipingane na mto!
 
Ndio maana mnaambiwaga ndoa sio fasheni ili mradi tu uwaringishie watu kuwa umeolewa.

Jitahidi uolewe na rafiki yako. Huyo mwanaume wala hana tatizo, shida hapo ni kila mtu na hulka tofauti.

Suluhisho hapo; Kama mume haongei wewe muongeleshe, Kama hakugegedi wewe usilale na nguo kisha anzisha wewe miguso mbona kinaeleweka tu. Kama hapangi mikakati ya maendeleo anzisha wewe mada ya nini unapenda kifanyike.

Kumbukeni ndoa ni muunganiko wa watu wawili wa jinsia tofauti na wenye tabia za tofauti.
 
Mwambie achukue ushauri Wa huyu MTU.
 
Vipi bidada akijaribu kumuuliz au kuzungumza nahuyo mumewe, mume hutoa response ipi??
 
Mwanamke nae akisusa ndoa kama vile mwezi kususia kuonekana Tz bc atapoteza ndoa hiyo, ni bora aanze yeye kumuongelesha.
 
Hivi mwanaume unapata vipi ujasiri wa kususa papuchi?!
Hajasusa, Kuna aina hii ya wanaume ambao hawanaga shobo na papuchi, hata wanawake ambao hawajisikii hamu ya mara kwa mara ya kugegedwa.

Hivyo mkiwa kwenye ndoa ni hadi mwenza wako awe anajiongeza kutoa vishawishi vinginevyo inakuwa kero kwa muhitaji.

Watu hatufanani, kuna wengine wana hormone chache, mwingine hana Hobby, mwingine anarizika tu kwakuwa tayari yupo kwenye ndoa.
 
Sure, hapo chemistry ndio changamoto.
 
Kiukwel wanaume tupo wabkariba mbali mbali amuxoee tu hata Mimi nipo hivyo Kuna muda naambiwaga Nina nuna
 
1. Apunguze makelele. Wanaume hawapendi kelele. Ampe space yake huenda ana mawazo na hataki kuongea. Wanaume wengi ndo walivyo na kuongelea mawazo yao wanaonaga ni udhaifu. Isitoshe kama nature ya mwanaume ni kukaa kimya haimaanishi sasa nature ibadilike kisa ndoa.

2. Bi Dada si aweke hela yake benki ama afanyie investment?

3.Huenda pregnancy hormones zinamuathiri wanaume. Kuna wanaume hawawagusi kabisa wanawake zao wakiwa wajawazito. Atulie alee mimba tu mume atakaa Sawa. Anawasiwasi ganii Kuku wake mwenyewe manati ya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…