Anasema anajenga kwa kukopa, Magufuli alitaka tujitegemee kwa kiasi fulani kujenga

Anasema anajenga kwa kukopa, Magufuli alitaka tujitegemee kwa kiasi fulani kujenga

Mama juzi kajisifu kukopa sana ili kukamilisha miradi aliyoanzisha Jpm, na kwamba atahakikisha hakuna hela ya mkopo inaliwa.

Watanzania tujue mabeberu walikua wanachukizwa na ari ya jpm ya kujitegemea na ile kuwafunza watanzania kwamba nchi yao ni tajiri jambo ambalo ni kweli. Aliwaonyesha mabeberu uwezo wa nchi yetu kujenga miradi kwa kujitegemea kwa kuanza na hela za ndani jambo lililowaudhi kwani aliweka mikakati kuhakikisha biashara za ndani na wawekezaji wanalipa kodi kufuatana na sheria na sio vinginevyo.

Nia ya mabeberu ilikua kutawala nchi kuhusu miradi gani tunaweza kufanyab na ipi hatuwezi au haturuhusiwi kufanya kufuatana na maslahi yao na sio maslahi ya nchi yetu. Pia ile jeuri ya kutaka kuruka kizingiti kwamba hatuwezi kujenga bila kukopa kwao kwa masharti yao iliwaudhi.

Nachotaka kusema kwa mama ni kwamba sio tu kwamba ahakikishe miradi inakamilika lakini awe alimuelewa jpm. Kwa hivyo asije ua ile fikra ya kujitegemea kwa kurukia mikopo kwa kila kitu na hasa ile isiyokua na tija bila kutumia kwa kiasi kikubwa nguvu yetu wenyewe. Atambue ubeberu moja ya nyenzo zao ni kuhakikisja tupo daima kwenye madeni makubwa yasiyolipika na hata kama yanalipika. Lazima pia kutambua mikopo ni biashara wala hakuna hisani.

Pia mama atambue vigogo wanaomzunguka wanapenda mikopo kwani ni hela ya kigeni inaingia wangependa kuipiga kwa kufanya dili mbalimbali hatimae mradi kua ghali sana au kupunguka ubora.
Kodi ulikuwa unalipa kiasi gani?
 
..Magufuli alikuwa ni kifaa cha kusaidia mapigo ya moyo kilichotengenezwa na mabeberu.

..Kwa hiyo yeye kudai anachukia Mabeberu ilikuwa ni ulaghai kwani uhai wake ulitegemea hisani ya kifaa chao.

..Na zile pushup na vitimbi vingine majukwaani kuonyesha kuwa yuko imara ilikuwa ni ulaghai.
A/c kwenye hewa Safi
 
Ukiwa zezeta usiyejua chochote ndio utaamini zile propaganda za Magufuli
Kwa makusanyo ya kodi ya nchi hii, kamwe huwezi kujenga bila kukopa
Alikuwa akikusanya bilioni 1400 kwa mwezi (trilioni 1.4)
Katika hizo, bilioni 700 zilikuwa zinatumika kulipa mishahara ya wafanyakazi
Bilioni 600 kulipa riba na madeni ya nje
Bilioni 100 kwenye elimu bure na mengineyo
Halafu utekeleze mradi wa trillioni 7 kwa pesa za ndani? Zipi hizo?
Ukiwa unatoa data jitahidi kuweka data za ukweli...Elimu bure ilikua 18B kwa mwezi not 100...
 
Mjinga tu ndio alishindwa kumuelewa magu. Alichomaanisha kama wanaweza kukuibia mabilioni ya madini ukidanganywa ni mchanga tunahitaji kuamka usingizini tuweze kua nchi tajiri.
Hukusikia Kabudi alivyosema au hujui kama hujui.
 
Dar-Moro alikopa wapi?

..Moro to Dodoma to Makutupora ni fedha za ndani au mkopo?

..Na Isaka to Mwanza ni fedha za ndani au mkopo?

..Hizo ndizo segments za Sgr ambazo ujenzi wake uliakuwa umekwisha anza wakati Magufuli akiwa hai.
 
Chagua moja hapa:- Uwe mateka wa mtu mwongo ambaye alikuwa anakopa halafu anadanganya kuwa anajenga kwa fedha za ndani.

AU

Utumie akili zako vizuri kwa kumuelewa Samia ambaye anakiri anakopa kumalizia kujenga miradi aliyoanzisha mtangulizi wake.
Fala kazini
 
Dar-Moro alikopa wapi?
The Tanzanian government has signed a facility agreement with Standard Chartered for a US$1.46bn term loan to fund part of the construction of the country's latest mega-project, the Standard Gauge Railway (SGR).Feb 18, 2020

Vijana acheni uvivu someni. Mtaishia kuwa vijana wa kiki tu!

Mkopo wenyewe nikupe data zaidi ni wa 6 years 8% kwa mwaka!! wakati Mama alipata 3% kwa 20 years aliotumia kujenga madarasa!. Hapo Raisi alikuwa Mama au Magu?
 
Awamu ya sita ilikopa katika kuendeleza miradi ingwa awamu ilitumezesha uongo wa mchana kweupe kuwa haikopi . Na wabobevu wa masuala ya kikopo walihoji Sana lakini sauti zao zilizimwa na propaganda za uongo.
Hivyo hayati magu alikopa Sana ingawa alitumia uongo kutuhadaa sisisi tusiojua Mambo.
 
Hii nchi itakuwa vigumu kupata maendeleo ya kweli kwa sababu kila Rais anayeingia madarakani anakuja na maono,mitazamo na misimamo yake ya jinsi gani nchi inatakiwa kwenda na kipindi chake kikiisha anayefuata naye anaanza na yake yani hakuna muendelezo kabisa
 
Mama juzi kajisifu kukopa sana ili kukamilisha miradi aliyoanzisha Jpm, na kwamba atahakikisha hakuna hela ya mkopo inaliwa.

Watanzania tujue mabeberu walikua wanachukizwa na ari ya jpm ya kujitegemea na ile kuwafunza watanzania kwamba nchi yao ni tajiri jambo ambalo ni kweli. Aliwaonyesha mabeberu uwezo wa nchi yetu kujenga miradi kwa kujitegemea kwa kuanza na hela za ndani jambo lililowaudhi kwani aliweka mikakati kuhakikisha biashara za ndani na wawekezaji wanalipa kodi kufuatana na sheria na sio vinginevyo.

Nia ya mabeberu ilikua kutawala nchi kuhusu miradi gani tunaweza kufanyab na ipi hatuwezi au haturuhusiwi kufanya kufuatana na maslahi yao na sio maslahi ya nchi yetu. Pia ile jeuri ya kutaka kuruka kizingiti kwamba hatuwezi kujenga bila kukopa kwao kwa masharti yao iliwaudhi.

Nachotaka kusema kwa mama ni kwamba sio tu kwamba ahakikishe miradi inakamilika lakini awe alimuelewa jpm. Kwa hivyo asije ua ile fikra ya kujitegemea kwa kurukia mikopo kwa kila kitu na hasa ile isiyokua na tija bila kutumia kwa kiasi kikubwa nguvu yetu wenyewe. Atambue ubeberu moja ya nyenzo zao ni kuhakikisja tupo daima kwenye madeni makubwa yasiyolipika na hata kama yanalipika. Lazima pia kutambua mikopo ni biashara wala hakuna hisani.

Pia mama atambue vigogo wanaomzunguka wanapenda mikopo kwani ni hela ya kigeni inaingia wangependa kuipiga kwa kufanya dili mbalimbali hatimae mradi kua ghali sana au kupunguka ubora.
Jamaa yenu alikuwa anakopa na kukwapua kimya kimya, heri Dr. Ni muwazi na anasema ukweli,ukweli ni jambo jema.
 
Back
Top Bottom