ANATAFUTWA: Michael Juma anatafutwa na mwanae. Alikuwa askari magereza, mkazi wa Masasi na Mtwara mjini

ANATAFUTWA: Michael Juma anatafutwa na mwanae. Alikuwa askari magereza, mkazi wa Masasi na Mtwara mjini

Mara nyingine tena narudi kwenu kuendelea na zoezi hili maana JF inazalisha watu wapya kila siku wenda wakamfahamu.

Ana ni mtoto wa kwanza wa mzee Michael,na amezaliwa miaka ya 1978/79.Baba yake mzee michael alikuwa ni askari magereza katika gereza la Musoma miaka ya 1980s na alikuwa na mke anajulikana kwa jina la mama Ana(bahati mbaya hatujapata majina yake halisi),Mnyiramba-Singida.

Na inasadikika Ana alizaliwa Mkoani singida ambapo mama yake alikuwa ameenda kwao kwa ajili ya maandalizi ya mazazi,badae alirudi Musoma.

Miaka hiyo ya 1980-82,huyu mama alipata mtoto mwingine wa kiume na badae Mzee juma aliacha kazi na kuwa fundi seremala kwa muda na inavyosadikika alirudi kwao Masasi-Mtwara na baada ya hapo taarifa zake hazikupatikana tena.

Tumejitahidi sana kufatilia hadi kazini kwake hatukufanikisha na pia kupitia hapa jukwaani bado hatujampata na hivyo kupitia binti yake huyu au kijana wake kama wapo au ata (wajukuu) wake kwani kwa sasa wanaweza kuwa ni watu wazima na pengine wakawa watumiaji wa JF.

Naomba wajitokeza kwani kuna ndugu yao anawatafuta muda mrefu.Asanteni
 
Picha ingekuwepo ingekuwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli ila hadi sasa hatumjui na picha yake hatuna kwani hii ni kupitia tu kusimuliwa na mama ambaye ndiye aliyezaa naye miaka ya 80.Kumbuka mazingira ya wakati huo hayakuwa mazuri kwa utunzaji wa kumbukumbu ina maana ata hawakupiga naye picha isipokuwa anakupa tu mwonekano wake
 
Poleni na majukumu wana JF.Kwa mara nyingine narudi kwenu kwa kuamini kuwa JF inazalisha watumiaji wapya kila siku.wengi mtakuwa mumeshasoma mada hii toka mwaka juzi,kwa ambao hawajaupitia ni kuwa huyu mzee Juma Michael alikuwa askari magereza miaka ya 80 ktk gereza la musoma-mara,kwao ni Masasi na pia alikuwa akisema kuwa baade mazazi wake waliamia Mtwara Mjini.

Alikuwa na mke anaitwa mama Ana-kwao Ilikuwa SINGIDA (akijulikana kwa jina la mtoto hila jina lake halisi hatukilipata hii ni kwa mjibu wa mtoa taarifa wetu).Miaka ya 1980 ndo alizaliwa mtoto Ana ambapo kwa sasa ni mtu mzima.Sababu ya kumtafuta ni kwamba kipindi yuko Musoma alizaa mtoto kwa sasa naye ni mtu mzima na anaitaji kuju a tu sehemu ya ukoo wake na pia kama mzee bado anishi aweze kumujua, yeye ni mfanyakazi kwa sasa.

Taarifa ambayo tulipewa ni kuwa kwenye miaka ya 1981 Mzee aliacha kazi na kufanya kazi ya fundi selemara kwenye karakana alioianzisha mwenyewe na badae alirudi kwao masasi.Kwa yeyote mwenye kumjua na ata kama Ana au watoto wake wapo tuwasiliane 0762364740.ASANTENI
 
Lakini mbona kama alimpata? Au nilikuwa naota maana uzi uliletwa hapa hapa
Hakupatikana mheshimiwa,wale walitupa taarifa za kitapeli ili wapate pesa tulifatilia tukaona ni uongo na pia nilitoa mrejesho hapa.ASANTE KWA KUJALI
 
Ngoja basi tuanze.upya..hao matapeli vipi hatima yao mpaka.sasa?
 
Habari Wana Jf?

Narudi kwenu Tena nikiwa na nyongeza juu ya huyu mzee wetu ,kwa ambao hawakufatilia hii thread apo nyuma ni kuwa Mzee Michael Juma alikuwa ni Askari magereza katika mkoa wa Mara katika gereza la Musoma-Musoma mjini miaka ya 1980s.Alikuwa ni mtu wa Mtwara, na alikuwa anajipambanua kuwa yeye alizaliwa Masasi na badae baba yake alihamia Mtwara mjini Hii ni kwa mjibu wa mtoa taarifa wetu.

Miaka hiyo alikuwa Ana mke aliyejulikana kwa jina la Mama ANA, kwa bahati mbaya hatukupata jina kamili la huyu mke wake Ila la huyu mtoto wao ANa,ambaye alizaliwa miaka ya 1980 Na kwa taarifa huyu mama ANA alikuwa ni mnyiramba kwao Singida.

Miaka ya 1990S aliacha kazi na kurejea kwao ambapo wenzake walikuwa wanaelezea kuwa aliamia kwao na wengine walimweleza huyu mtoa taarifa wetu kuwa aliacha kazi na kwenda kwao Masasi na kuanzisha kalakana lake binafsi kwani alikuwa upande wa ufundi selemara alipokwa gereza la Musoma,n a pia alikuwa akieleza kuwa ndugu yake mmoja alikuwa akifanya kazi ya uanajeshi katika kambi ya kiabakari lakini pia hatukuweza kupata jina kamili kwani mtoa taarifa hakumbuki kwa kuwa mda umepita(nyengeza).

Kwa Nini tuendelee kumtafuta? Hii ni kwa sababu mwanae anamtafuta na walau Kama mzee hayupo duniani aweze kuonana na ndugu zake. Kama Kuna yeyote Ana ABC Kupitia habari hii au Kama huyu mwanae Ana yupo au ata wajukuu Basi watutafute Kupitia 0789443404
 
Bila shaka familia ya baba na mama Anna taarifa hii itawafikia.
 
Bila shaka utampata
Cha msingi Ndo hiki na kwa maisha ya miaka hiyo Kama yupo hai atakuwa anaitaji msaada wa kuudumiwa Cha msingi akipatikana ni Bora zaidi au ata mtu wa ukoo wake
 
Habari Wana jamvi?

Narudi tena kwenu kumtafuta mtajwa hapo juu maana JF huzaliwa members wapya kila siku. Huyu ni mtoto wa kwanza wa mzee Michael Juma, ambaye mara nyingi nimemtafuta humu bila mafanikio. Mara ya mwisho nilipata habari kuwa alikuwa Mbeya, nilifatilia haikuwa taarifa sahihi.

Kwa wageni na hii storI ni kuwa, Mzee Michael Juma alikuwa Afisa wa Jeshi la Magereza miaka ya 80's katika Gereza la Musoma na alikuwa upande wa karakana & uselemala. Miaka hiyo ya 80 alifika Musoma kutokea Gereza la Singida na alikuwa na mwanamke aliyejulikana kwa jina la mama Ana (hatukuweza kupata jina lake halisi), Mnyiranda - Singida na ndiye mwenye mtoto mlengwa hapo juu.

Kwa mujibu wa msimulizi wetu ni kuwa mzee alikuwa akisema kuwa yeye alizaliwa Masasi na baadaye wazazi wake walihamia Mtwara Mjini, na pia alikuwa na ndugu yake aliyekuwa akifanya kazi kambi ya jeshi ya Kiabakari - Musoma.

Inasemekana kati ya mwaka 1989 hadi 1990 aliacha kazi na kurejea kwao, ambapo mtoa taarifa wetu alielezwa na baadhi ya askari alikuwa akifanya nao kazi. Tatizo pia linakuja hatukupata kijiji au jina la ukoo alikuwa akitokea na pia hata kazini kwake hatukufanikisha kwani ni mda mrefu na pia teknolojia imebadilika ya utunzaji kumbukumbu licha ya kutupa ushirikiano.

Kwa nini atafutwe Ana? Hii itasaidia kama kuna mtoto au mjukuu wake, maana kama yupo ni mtu mzima mweye watoto au wajukuu wanaoweza kuunganisha doti na kuielewa historia ya babu yao na pia kuweza kupata taarifa juu ya mzee ili apatikane na kwa umri atakuwa ni mzee kama yu hai na pia kupata usaidizi.

Kama Ana au yeyote atakayepitia maelezo haya na kupata uelewa wa mtu anayezungumziwa tuwasiliane kupitia 0789443404 au 0762364740.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom