Huyo jamaa yako kama mpaka muda huu atakuwa hajachukua maamuzi magumu ya kuacha hiyo kazi inayo dhrauliwa mpaka na wendawazimu wanao okota makopo barabarani, basi atakuwa ni kilaza wa mwisho kabisa duniani.
Yaani unaingiza mpaka milioni 180 kwa mwaka, halafu bado unakubali kutumikishwa kwa mshahara wa laki 6 kwa mwezi?
Jambo la msingi hapo asiongeze ukubwa wa shamba ndani ya muda mfupi. Badala yake atumie sehemu ya faida aliyopata kununua kiwanja maeneo mazuri na kujenga nyumba za biashara mfano za kupangusha, Lodge, nk. Hizo nyumba ndizo zitakazompa ulinzi pale itakapotokea kilimo kikamyumbisha.