Anataka kuacha ajira ya kudumu ajikite kwenye kilimo

Masanja ana hela gani?

Unafananisha kilimo Cha Mo mwenye heka zaidi ya mkoa na biggest sisal producer duniani na wewe mwenye hela 2 na kutegemea mvua? Jichanganye ufurahie show.

Ukitaka kuwa fukara nchi hii kuwa mkulima.
Kwa intlijensia yang ndogo nahs huyu anayetangaza ukitaka kuwa maskn kuwa mkulima yeye ni mkulima Tena mwenye mafanikio makubwa! Alshaona neema iliyojfcha ardhin hatak weng tufanikiwe ili tubaki madkin wa kutupwa! Nmefanya biashara mbal mbal ila sjaona iliyonpa kipato km kilimo! Kilimo kinakufanya upge hatua kubwa kubwa na hv naandka nko field navuna mpunga wangu haitatokea mtu ankatishe tamaa, nalima kw kutegemea mvua cmwaglii bado najivunia
 
Me nashauri aende navyo vyote hivyohivyo atafika tu
 
Huyo jamaa yako kama mpaka muda huu atakuwa hajachukua maamuzi magumu ya kuacha hiyo kazi inayo dhrauliwa mpaka na wendawazimu wanao okota makopo barabarani, basi atakuwa ni kilaza wa mwisho kabisa duniani.

Yaani unaingiza mpaka milioni 180 kwa mwaka, halafu bado unakubali kutumikishwa kwa mshahara wa laki 6 kwa mwezi?

Jambo la msingi hapo asiongeze ukubwa wa shamba ndani ya muda mfupi. Badala yake atumie sehemu ya faida aliyopata kununua kiwanja maeneo mazuri na kujenga nyumba za biashara mfano za kupangusha, Lodge, nk. Hizo nyumba ndizo zitakazompa ulinzi pale itakapotokea kilimo kikamyumbisha.
 
Ajira muda mwingine ni umaskini mkuu. Tunakubaliana na mawzo yako. Mm nalipa 300k kama intern Kwa mwezi lakin hii hela ni chini ya kiwango ninachopata kariakoo Kwa siku. Jumamos Moja napata mpaka 45k... Unafrkiria mm nawaza nn Kwa sasa?
 
Weka/kuwa na standards.. sio hela yote iishir kilimoni tu. Mbona unaweza uka"conglomerate" investment zako bila shida kaka?
 
Ajira muda mwingine ni umaskini mkuu. Tunakubaliana na mawzo yako. Mm nalipa 300k kama intern Kwa mwezi lakin hii hela ni chini ya kiwango ninachopata kariakoo Kwa siku. Jumamos Moja napata mpaka 45k... Unafrkiria mm nawaza nn Kwa sasa?
Sio tu muda mwingine, ajira ni umasikini....kama hauna vyanzo vingine vya mapato
 
Ujue moyo unaeza kukuelekeza kumbe pabovu mkuu
Kwa jambo kama hili, ukifuata ushauri wa watu ndiyo mwanzo wa kupotea. Unachotakiwa kufanya ni kutafiti wewe mwenyewe na uje na jibu lako. Mazingira na mipango ya watu inatofautiana kabisa. Kuna ambaye akiicha ualimu atafanikiwa. Kuna ambaye atakwama.
 
Uko sahihi. Nimekumbuka kitabu cha Rich Dad, Poor Dad. Ukitaka maisha yako yawe mazuri ni kujiwekea lengo la kuwa na akiba ambayo unaweza kuitumia kwa kuishi maisha yako ya kila siku angalau kwa miaka miwili na kuendelea bila kufanya kazi. Ukiwa na akiba ya miaka miwili basi una luxury ya kuweza kutumia hiyo miaka miwili ku-maneuver ili upate namna ya kujipatia tena kipato.
 
Muongo huyo story za kusadikika hizo.
Mil 180 kwa mwaka ? Halafu bado uendelee kukomaa na kazi ya mil 6 kwa mwaka? Wakati mpaka unastaafu kazi zaidi ya miaka 30 hupati pension ya mil 180.
 
Sasa kama kwa msimu mmoja anauwezo wa kupata hela sawa au zaidi ya kiinua mgongo baada ya mika 25 serikalini kwanini anapoteza muda hivyo
 
Ndio ndio mkuu nakupata, Hii kanuni imekaa kibiashara ila ni physics tupu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…