Anataka kurudi baada ya kukimbilia kwao

Blaszczykowski

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2022
Posts
310
Reaction score
1,100
Ni miezi 4 sasa tokea mke wangu kukimbia na kuondoka na vitu na kuniacha kama nipo form one. Sasa anataka kurudi ili tuanze maisha mapya kwa sababu tulibahatika kupata mtoto mmoja.

Moyo wangu japo ninampenda ila nikikumbuka dharau, manyanyaso, maneno ya shombo kutoka kwa upande wa kwao nawaza sana. Maana ndoa si watu wawili tu yaani mke na mume, bali ni muunganiko wa familia mbili.

Nina maswali mengi sana ambayo hayana majibu;
~ Anarudi kwangu kwa ugumu wa maisha?
~ Anarudi kwangu kwa ajili ya kulea mtoto?
~ Anarudi kwangu amejifunza kuthamini mume?
~ Au anataka arudi kunimaliza kabisa?

Maana aliondoka kwa kishindo sana.
 
Umeandika hapo juu ndoa ni nini?Miwani yangu imevunjika.Kushnehi ghaega!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…