Anataka kuwa mke bora baada ya kunidharau

Si bora angebeti kwangu kuliko huko alikoenda
Muache aishi maisha yake na wewe ishi yako usimlaumu kama unampenda oa uendelee pale mlipoishia miaka 10 umzeeshe na Bado pengine hukuwa na mpango naye, ungesema labda hata barua ya posa ulimtolea tungeamini alikuwa Kwenye mipango yako.

Ukiona unampenda endelea naye lakini lawama za aliniacha ziweke kando, kwanza wewe ndio umemchakata zaidi kuliko alikoenda kama ni asali umeichimba zaidi kuliko huko alikoenda, kwahiyo usione kama kukumisi anakosea.
 
Wanawake shida huwa maono yao mwisho ni zilipoishia pua zao.
Pole sana, na hongera kwa uamuzi wa kiume, usijiloge ukarudi hapo, utakuja juta sana maisha yako yote.
 
Acha mambo yako mkuu, yaaji manzi mmedumu miaka zaidi ya 10, huo ni uvumilivu wa kiwango gani ambao ulikua unautaka toka kwake.

Miaka 10 bro!?? Unampiga pipe tu na kwao hawajui, na yeye uhakika wa kuolewa na wewe hana.

Tatizo lilianzia kwako, umemharibia binti wa watu maisha yake kwa ubinafsi wako.
 
Mipango ya kuoana ilikuwepo
 
Hicho kipande cha tikiti sasaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Niwakumbushe wanawake kwa mkazo......mwanaume hajawahi kuaibika, akianguka anasimama na anajikung'uta anatafuta chaka mpya bora zaidi....mkuu achana naye aendelee kula ustawi wa jamii
 
Maisha yalivyo ya hovyo watu wameanza kumlaumu jamaa na kumuona mwanamke yupo sawa!!
Wanaume tupambane tu kuishi furaha yetu.
Achana na mwanamke anayetafuta kwa kuponea njaa zake.
Anataka kugeuza ndoa kama ajira ya kumfanya Aishi.
 
Kuna jamaa alisema humu katika suala la ndoa mwanamke huolewa na mwanaume yeyote anayeonyesha nia ya kutaka kumuoa.
Mwanamke hawezi kukaa na MTU kwa miaka 10 Kama hampendi,Sema alihisi muda unamtupa mkono ndio akaona atafute mtu amuoe apate heshima ya ndoa bahati mbaya akaangua pua..ajali kazini
 
Katika kitu sitokuja kufanya ni kulea mtoto wa mwanaume mwenzangu tena ukilinganisha huyo mwanamke aliondoka kwako kwa dharau.

Kitendo cha kuishi naye miaka 10 bila kumsaliti kivyovyote kwa akili ya kawaida tu hakutakiwa kuwa na mashaka yoyote sababu ndoa ni kutamka maneno na vipande vya karatasi tu na hakuna kingine zaidi ya upendo wa kweli.

Huyo anakuona bwege bushoke ndio maana mwanzo alithubutu kuondoka kwako na alijua yakienda kushoto atarudi kwako na wewe bwege lake utampokea na kingine mwanamke mwenye mtoto hata ukioa tayari anakuwa na special connection na yule jamaa kama mzazi mwenzake na hapo lazima kuwe na usumbufu kwenye hiyo ndoa na probability ya yeye kulala tena na huyo jamaa ni kubwa mno.

Mkuu kuna watoto wazuri na wabichi kabisa hapa duniani tafuta mwingine uanzishe familia yako mwenyewe halali hakuna kugeuka nyuma au utakuja kulia zaidi, na next time jifunze kuwa na mamlaka kama mwanaume na sio kuwa mpole na yes man au wanawake watakuendesha sana na kukudharau.

No offense kwa maneno makali lakini huo ndio ukweli mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…