Anataka kuwa mke bora baada ya kunidharau

Anataka kuwa mke bora baada ya kunidharau

Miaka 10 wakati unamkula tu....Daaa.Kwanza ana moyo sana kurudi kwako....mwambie maisha mazuri ni hayo anayoishi aache kujidhalilisha kuombaomba ndoa Kwa maex😏
Anataka nimtafutie kazi yoyote
 
Tulidumu karibu miaka 10, nia yangu ilikiwa ni kumuoa ila baada ya kukamilisha mipango niliyojiwekea, ilipobaki miezi michache tuoane akanikalisha chini akaniambia kuwa hawezi kuendelea kuwa na mimi.

Ikabidi niheshimu mawazo yake japo roho iliniuma mpaka kufikia hatua nikawa napata maumivu kwenye moyo.

Nakumbuka kuna siku nilikuwa namfuatilia kwenye facebook nikitamani kujua aliyenipiku ananini kunizidi, nikakuta kamposti jamaa fulani mfupi kapiga picha mbele ya rav 4, roho iliniuma sana na ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukosa usingizi mpaka asubuhi, na kiherehere cha kumfuatia kikaishia palepale.

Baada ya kupita miaka mitano, Mwaka jana siku moja napeleka mzigo wa mteja mara simu ikaita kuchek namba ya airtel, kupokea anasema mimi I, nikamuambia mimi siongeagi na wake za watu akasema hajaolewa.

Akasema amenimiss anatamani kuniona tukapanga tukakutana, nilikuwa na hamu ya kuona maisha anayoishi,
Tukaenda anapoishi ni chumba kimoja kidogo kina kitanda tu na jiko la mkaa, amepauka amekonda. Akawa anampa mtoto kipande cha tikiti maji.

Hana kazi anategemea elfu 50 ya malezi ya mtoto anayopata kila mwezi kutoka kwa baba wa mtoto. Yenyewe aliipata kwa mbinde kupitia ustawi wa jamii.

Akanielezea kuwa yule mwanaume alikuwa ameoa ana watoto wa 3 na amezalisha wanawake kibao.

Akaniomba numpe nafasi awe mke bora mi nikawa namcheki tu alivyopauka.

Hivi kweli nipambanie maisha mpaka hapa nilipo alafu nioe mwanamke mwenye mtoto tena aliyenidhau.

Hakikisheni mkiacha mtu mnaenda kwa aliye bora zaidi. Ni hesabu rahisi tu.
Acha ujinga.Muoe.
 
Achana nae hisia zisizidi akili , cjui kipi huelew apo aanh unakera [emoji51][emoji51][emoji51] elewa ... Ubao unasoma 1-0 hutoboi umeshindwa miaka 10 utaweza sasa

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Vipi nayeye kumuweka rehani miaka 10, kama ni mtoto yupo darasa tano kabisa.
Kila mtu analinda interest zake, bibie baada ya kuona amewekwa rehani aliamua kumove on kwa hiyo utatuzi wa kuwekwa kinyumba bila ndoa kwa miaka 10 ulishafanyika.
Hapa tunajadili lililopo mbele yetu mkuu nalo ni la bibie kutaka kurudisha jeshi baada ya malengo yake huko alipokwenda kukwama.
 
Duh...!! Zimwi likujualo halikuli likakwisha.

Mi naona kama moyoni kwako bado ana nafasi mchukue umuoe.. hakikisha unamuhudumia mtoto kama wako, zile elfu 50 zisitishwe na aache mazoea na mzazi mwenzie.

Unaweza kuchukua mke mpya akawa na majanga pia matatizo yakaanza na upyaa.

Mmmh! Lakini mwenye mtoto tayari huwaga mtihani..
Haitokaa itokee aache mawasiliano na baba wa mtoto,,kumbuka wameshea damu hapo na shida ndo inaanzia hapo,ingekua hajazalishwa angalau,lkn yule jamaa mfupi aliekuumiza miaka mitano ilopita ndio huyo huyo atakuja kukuumiza tena kwa kigezo cha kumtembelea mwanae.
 
Waafrika tumepatwa na nini?
Hizo certificate na sherehe ni mbwembwe za ziada tu...
Ndoa ni makubaliano ke na me mengine ya zoada...
So huyo dada ameivunja ndoa yake halali sababu kuchelewa kumtunikiwa certificate.

Time wasted.
Wanataka sherehe na matarumbeta
 
Back
Top Bottom