Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

usizunguke zunguke ndugu.. Njoo tuungame ubatizo mmoja wa maondoleo ya dhambi,tusubirie ufufuko wa wafu na uzima wa milele ijayo.
Mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi za ulimwengu atakuhurumia

Bwana awe nanyi nyote....[emoji7]
Aje wapi?
 
Mimi kwa maoni yangu kanisa ambalo unaweza kuliamini ni biblia ambayo ni muongozo wa roho ya mwnadamu kuingia mbinguni na ukisoma biblia vizuri ukaielewa na ukafuata yale yaliyoagizwa utakuwa mtu mmoja safi sana maana utamuomba Mungu aliyehai na kufuata yeye alichokifundisha.Nasema hivi kwa sababu makanisa mengu hivi leo yanaubinafsi, na kujinufaisha na maigizo mengi amabayo ni hopeless na wala hayakufikishi popote kama lengo lako ni kuwa karibu na mungu
 
Hujaonesha unafiki u wapi pale katika post #262 then nitakujibu
Unafiki ni pale unapothubutu kujiona bora na kuijua Biblia kuliko yeye aliyeandika.Mbaya zaidi inaonekana hauna ufahamu juu ya Roho Mtakatifu bali unaongozwa na hisia.
 
Unafiki ni pale unapothubutu kujiona bora na kuijua Biblia kuliko yeye aliyeandika.Mbaya zaidi inaonekana hauna ufahamu juu ya Roho Mtakatifu bali unaongozwa na hisia.
Waefeso 5:18 kuwa "Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho"

unaielewaje?
 
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
2 Pet 1:20‭-‬21 SUV
Biblia imeandikwa na nani akiongozwa na nani??
 
Mpaka umehitaji kuja kwenye haya makanisa kabla ya hapo upo dhehebu gan
 
Waefeso 5:18 kuwa "Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho"

unaielewaje?
1 Tim 5:23 SUV

Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.


Unaielewaje?
 
Hakunaga
 
Kwa sifa ulizotaja Kati ya hizo naona Kuna kanisa linasifa Kama Tisa nakushauri enenda kwenye kanisa RC( Roman Catholic)
 
😀😀 yaani katika kanisa ambalo sijalielewa ni hilo aise. Mh!😷
na hauwezi kulielewa haliendeshwi kwa mihemko na miujiza inayoonekana kwa macho ya wanadamu. miujiza inaweza kuwepo lakini sio misingi ya imani ya waumini.
linaelewa watu wote si wakamilifu na mabadiliko sio ya siku moja ni process kwa kiasi kikubwa hawaoni hasara kwa ngano kukua na magugu! cha msingi zaidi watu waishi kwa upendo na furaha huku wakijua hapa duniani ni kwa kupita tu.
binadamu anahitaji kuishi kwa uaminifu kimwili na kiroho na ndomaana wanahuduma nyingi za jamii ili kuponya miili ambayo ni hekaru la Roho Mtakatifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…