Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

Pole sana na sio Tanzania dhehebu langu linaitwa Roman Catholic (RC) umevamia dini unataka kufundisha ata usivyovijua si ndio unaniattack utafikiri apo umekaa na yesu pembeni khaaa uliza gugo wakwambie
ROMAN CTHOLIC (RC} JINA Roman LILISHAONDOLEWA SIKU NYINGI WATU BAADA YA KUENDESHA MGOMO KUWA WAO SIO WAFUASI WA ROMA!!! KAMUULIZE PADRI WAKO

SASA HIVI LINAITWA TU KANISA KATOLIKI SIO ROMAN KATOLIKI!!! nAONA UNAJISALIA KIMAZOEA HATA HUJUI KINACHOENDELEA KANISANI KWAKO
 
Kusali ni muhimu, lakini baadhi ya tabia na sheria za baadhi ya makanisa yanachangia sana kuvunja moyo watu kuabudu.

Naomba mwenye kujua kanisa lolote lenye sifa zifuatazo ili nijiunge;
  1. Liwe ni kanisa la kikristu
  2. Liwe na mfumo wa kitaasisi (yaani management iwe kimfumo wa kitaasisi)
  3. Liwe linapatikana angalau kila wilaya/mkoa
  4. Misingi ya waumini wake iwe ni ile ya teamwork (umoja bila kubagua masikini au tajiri hususani wakati wa matatizo ya mmoja mmoja)
  5. Liwe ni kanisa lisilotegemea uwepo wa mchungaji/kiongozi mmoja
  6. Liwe ni kanisa lenye ratiba maalum ya kuzingatiwa (standards)
  7. Liwe ni kanisa linalojali malezi ya watoto kiroho
  8. Liwe ni kanisa la watu wenye akili timamu.
  9. Liwe ni kanisa lenye kupenda haki, usawa na uwazi
  10. Liwe ni kanisa linaloponya, kukuza na kujenga imani kwa waumini wachanga n.k
Yoyote anayefahamu kanisa lenye hizo sifa anifahamishe!! Natafuta kanisa la kujiunga!
Uko mkoa gan mkuu?

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna Kanisa ambalo lina misingi bora ya kiimani na yenye kumpendeza Mungu kama Kanisa takatifu Katoriki la mitume. (Roman Carothic).
Kwanza lina misingi ya kiuongozi kuanzia chini mpaka juu… pia lina muabudu Mungu wa kweli…
mungu ana mama yake aliyemzaa anaitwa Maria Mama wa MUNGU!!!

Mungu ni roho tupu hakuna binadamu awezaye kuzaa roho .Lakini Maria anaitwa Mama wa MUNGU!!! NA anasemekana alipaa mbinguni!!! Hakuna popote kwenye Biblia KUNAPOONYESHA MARIA ALIPAAA!!!
 
Kwa Sifa hizo zipo kwenye Kanisa la SEVENTH DAY ADVENTIST CHURCH (S.D.A) Hili linapatikana Kila mkoa, wilaya, tarafa, Kata na karibia Kila kijiji Tanzania..

Halitegemei maamuzi ya mtu mmoja, linazingatia malezi ya watoto, kuanzia mjamzito anakuwa na darasa lake katika siku za Ibada kujifunza, watoto umri wa Mwaka 1 Hadi 3 wana Darasa lao., 4--6, Darasa lao, 7--9 Darasa lao, 10--12 Darasa lao, 13--16 Darasa lao n.k, kwa malezi ya watoto Hilo ndo ninalofahamu lipo vizuri.

Kuhusu ubaguzi hakuna Ubaguzi, mtu aweza kuwa mzee wa Kanisa au mkuu wa Kitengo flan, hata kama siyo Tajiri ilimradi tu awe na mwenendo mzuri Kiroho na ana kipawa na uelewa wa kusimamia Kitengo hicho, Mwanzoni kulikuwa na Changamoto ya wanawake kuhubiri Ila kwa Sasa wanahubiri na kuongoza vitengo kanisani, maamuzi mengi ni Shirikishi na watu wanakaa katika Vikao na kuleta Kila maamuzi kujadiliwa na kupitishwa na mkutano wa washiriki wote..
 
Kanisa katoliki, niko hapa na baba paroko na waumini wenzangu tunapiga safari lager bariiiidi na kutafakari masomo ya dominika ya leo
Katoliki kwa mbege hamjambo..naishi karibu nalo aisee father akiteremka madhabahuni tu yupo grocery Ni balaa
 
Jiunge Pentecost international worship center lipo ursino street plot no 28 unaweza kuwatembelea Juma pili moja
Ursino street ni mtaa wa Kikwete maarufu mikocheni karibu na morroco

Kanisa liko na sita tajwa
Kanisa halipo kila wilaya wala mkoa lipo hapo hapo..haya makanisa ya wapigaji hakuna taasisi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sifa hizo anglican linakufaa.

Sifa zake.

1. Ni kanisa la kitaasisi ambalo mfumo wake unaanzia juu, halimiliki na mtu yoyote. Kila mwezi wa 6 linakuwa na ihamisho wa wachunguaji kutoka eneo moja kwenda lingine.

2. Mchungaji kama hamumuelewi wazee wa,kanisa mna haki ya kwenda kwa mkuu wake askofu au jimboni na mkasikilizwa na akahama.

3. Halina michango isiyoeleweka, hata ukitokea mchango uko wazi, mfano

kununua viti.
kujenga kanisa au kuboresha

nyumba ya mchungaji au mwinjilisti.

Mchungaji au mwinjilisti akihama mali zote zilizonunulia na kanisa ni zinabakia kuwa mali ya kanisa si mali zake,,hivyo zitatumia na mwingine aliyefuata.

4. Linajali waumini wote na halina ubaguzi.

5. Linapatikana maeneo mengi, na ni kanisa la pili kuanzishwa karne ya 16 likitanguliwa na roman catholic.

6. sheria zake ziko wazi na mchungaji hupangiwa mshahara na wazee wa kanisa kulingana na pato la kanisa.

Kama una swali uliza.
 
Back
Top Bottom