Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

Kanisa aliloacha Kristo ni moja tu! Kanisa Katoliki.Hayo mengine si makanisa bali ni madhehebu tu yaliyoanzishwa na watu.
 
Kusali ni muhimu, lakini baadhi ya tabia na sheria za baadhi ya makanisa yanachangia sana kuvunja moyo watu kuabudu.

Naomba mwenye kujua kanisa lolote lenye sifa zifuatazo ili nijiunge;
  1. Liwe ni kanisa la kikristu
  2. Liwe na mfumo wa kitaasisi (yaani management iwe kimfumo wa kitaasisi)
  3. Liwe linapatikana angalau kila wilaya/mkoa
  4. Misingi ya waumini wake iwe ni ile ya teamwork (umoja bila kubagua masikini au tajiri hususani wakati wa matatizo ya mmoja mmoja)
  5. Liwe ni kanisa lisilotegemea uwepo wa mchungaji/kiongozi mmoja
  6. Liwe ni kanisa lenye ratiba maalum ya kuzingatiwa (standards)
  7. Liwe ni kanisa linalojali malezi ya watoto kiroho
  8. Liwe ni kanisa la watu wenye akili timamu.
  9. Liwe ni kanisa lenye kupenda haki, usawa na uwazi
  10. Liwe ni kanisa linaloponya, kukuza na kujenga imani kwa waumini wachanga n.k
Yoyote anayefahamu kanisa lenye hizo sifa anifahamishe!! Natafuta kanisa la kujiunga!
Hakuna kanisa la namna hii, tafuta kikundi
 
Mt 16:18 SUV

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.


Na hilo ndilo neno la bwana...

Kanisa Takatifu katoliki la Mitume. Na liko duniani kote. Taasisi imara kuliko zote. Kanisa halimilikiwi na mchungaji wala nabii. Unaguzi ni wewe kutozishika na kuziishi kanuni na sheria za kanisa katoliki.

Hakuna ubaguzi kama wanavyodai wengine hapa. Mf. Ruge, nillionea mrema, kingunge hawa ni baadhi ya vigogo ambao waliasi ukatoliki kwa namna yao hivyo kujikuta wakikosa huduma. Hawakua masikini ama wanyonge. Ni vigogo na sheria imetumika ipasavyo. Kanisa ni moja takatifu katoliki. Inada ni moja, inada haiendeshwi kwa utashi wa nabii ama mchungaji. Hivyo inakupa nafasi muumini kujiandaa vyema kwa ibada. Inada ya leo kimara, sinza, mwenge, kkoo, italy, spain, usa, mwanza, rwanda zote zinafanana.


Tumsifu Yesu Kristu[emoji120]
Ameen! Ubarikiwe! I am proudly Catholic & I'll die Catholic
 
ROMAN CTHOLIC (RC} JINA Roman LILISHAONDOLEWA SIKU NYINGI WATU BAADA YA KUENDESHA MGOMO KUWA WAO SIO WAFUASI WA ROMA!!! KAMUULIZE PADRI WAKO

SASA HIVI LINAITWA TU KANISA KATOLIKI SIO ROMAN KATOLIKI!!! nAONA UNAJISALIA KIMAZOEA HATA HUJUI KINACHOENDELEA KANISANI KWAKO
Huyu atakuwa shahidi wa yehova huyu [emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu endelea tu kumsoma nabii wenu Ellen G White huku hautaelewa!
 
Unadhania wote wanajua kitu flan ni dhambi? Uamin kwenye kila wanachoambiwa na padri na kiongozi mkuu wa kanisa pasipo kukichunguza ndio maana leo hii papa anauwezo wa kubadirisha sala ya "baba yetu" na asiojiwe
Viongozi wao wana adhabu kubwa sana kwa kutowaambia ukweli wote waumini.
 
mungu ana mama yake aliyemzaa anaitwa Maria Mama wa MUNGU!!!

Mungu ni roho tupu hakuna binadamu awezaye kuzaa roho .Lakini Maria anaitwa Mama wa MUNGU!!! NA anasemekana alipaa mbinguni!!! Hakuna popote kwenye Biblia KUNAPOONYESHA MARIA ALIPAAA!!!
Kiitikio: Utuombee

Maria Mtakatifu,
Mzazi Mtakatifu wa Mungu,
Bikira Mtakatifu, Mkuu wa mabikira,
Mama wa Kristu,
Mama wa neema ya Mungu,
Mama mtakatifu sana,
Mama mwenye usafi wa moyo,
Mama usiye na doa,
Mama usiye na dhambi,
Mama mpendelevu,
Mama mstaajabivu,
Mama wa shauri jema,
Mama wa Mwumba,
Mama wa Mkombozi,
Bikira mwenye utaratibu,
Bikira mwenye heshima,
Bikira mwenye sifa,
Bikira mwenye enzi,
Bikira mwenye huruma,
Bikira amini,
Kikao cha haki,
Kikao cha hekima,
Sababu ya furaha yetu,
Chombo cha neema,
Chombo cha heshima,
Chombo bora cha ibada,
Waridi lenye fumbo,
Mnara wa Daudi,
Mnara wa pembe,
Nyumba ya dhahabu,
Sanduku la Agano,
Mlango wa mbingu,
Nyota ya asubuhi,
Afya ya wagonjwa,
Makimbilio ya wakosefu,
Mfariji wa wenye uchungu,
Msaada wa Wakristu,
Malkia wa Malaika,
Malkia wa Mababu,
Malkia wa Manabii,
Malkia wa Mitume,
Malkia wa Mashaidi,
Malkia wa Waungama,
Malkia wa Mabikira,
Malkia wa Watakatifu wote,
Malkia uliyeumbwa, pasipo dhambi ya asili,
Malkia uliyepalizwa mbinguni,
Malkia wa Rozari takatifu,
Malkia wa amani.

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utusamehe, Bwana.

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utusikilize, Bwana.

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utuhurumie.

K. Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu.
W. Tujaliwe ahadi za Kristu.

TUMSIFU YESU KRISTU!
 
Thibitisha usemi wako
MT 16:18

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. 20
 
Back
Top Bottom