Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

Kanisa aliloacha Kristo ni moja tu! Kanisa Katoliki.Hayo mengine si makanisa bali ni madhehebu tu yaliyoanzishwa na watu.
 
Hakuna kanisa la namna hii, tafuta kikundi
 
Ameen! Ubarikiwe! I am proudly Catholic & I'll die Catholic
 
Huyu atakuwa shahidi wa yehova huyu [emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu endelea tu kumsoma nabii wenu Ellen G White huku hautaelewa!
 
Unadhania wote wanajua kitu flan ni dhambi? Uamin kwenye kila wanachoambiwa na padri na kiongozi mkuu wa kanisa pasipo kukichunguza ndio maana leo hii papa anauwezo wa kubadirisha sala ya "baba yetu" na asiojiwe
Viongozi wao wana adhabu kubwa sana kwa kutowaambia ukweli wote waumini.
 
mungu ana mama yake aliyemzaa anaitwa Maria Mama wa MUNGU!!!

Mungu ni roho tupu hakuna binadamu awezaye kuzaa roho .Lakini Maria anaitwa Mama wa MUNGU!!! NA anasemekana alipaa mbinguni!!! Hakuna popote kwenye Biblia KUNAPOONYESHA MARIA ALIPAAA!!!
Kiitikio: Utuombee

Maria Mtakatifu,
Mzazi Mtakatifu wa Mungu,
Bikira Mtakatifu, Mkuu wa mabikira,
Mama wa Kristu,
Mama wa neema ya Mungu,
Mama mtakatifu sana,
Mama mwenye usafi wa moyo,
Mama usiye na doa,
Mama usiye na dhambi,
Mama mpendelevu,
Mama mstaajabivu,
Mama wa shauri jema,
Mama wa Mwumba,
Mama wa Mkombozi,
Bikira mwenye utaratibu,
Bikira mwenye heshima,
Bikira mwenye sifa,
Bikira mwenye enzi,
Bikira mwenye huruma,
Bikira amini,
Kikao cha haki,
Kikao cha hekima,
Sababu ya furaha yetu,
Chombo cha neema,
Chombo cha heshima,
Chombo bora cha ibada,
Waridi lenye fumbo,
Mnara wa Daudi,
Mnara wa pembe,
Nyumba ya dhahabu,
Sanduku la Agano,
Mlango wa mbingu,
Nyota ya asubuhi,
Afya ya wagonjwa,
Makimbilio ya wakosefu,
Mfariji wa wenye uchungu,
Msaada wa Wakristu,
Malkia wa Malaika,
Malkia wa Mababu,
Malkia wa Manabii,
Malkia wa Mitume,
Malkia wa Mashaidi,
Malkia wa Waungama,
Malkia wa Mabikira,
Malkia wa Watakatifu wote,
Malkia uliyeumbwa, pasipo dhambi ya asili,
Malkia uliyepalizwa mbinguni,
Malkia wa Rozari takatifu,
Malkia wa amani.

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utusamehe, Bwana.

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utusikilize, Bwana.

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utuhurumie.

K. Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu.
W. Tujaliwe ahadi za Kristu.

TUMSIFU YESU KRISTU!
 
Thibitisha usemi wako
MT 16:18

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. 20
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…