Anayefikiria kujiunga na Savanna Fibre kuwa makini sana

Anayefikiria kujiunga na Savanna Fibre kuwa makini sana

jooohs

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
3,908
Reaction score
15,013
Kutokana na uzoefu wangu binafsi, nashauri mtu yeyote anayefikiria kujiunga na Savanna Fibre kuwa makini sana kabla ya kufanya malipo.

Nilifanya malipo kwa matarajio ya kuunganishiwa huduma kwa muda uliotajwa, lakini hadi sasa nimepitisha zaidi ya miezi miwili bila kupata huduma kama nilivyotarajia.

Katika kipindi hicho nimekuwa nikifuatilia mara kwa mara, kupiga simu nyingi na kutuma ujumbe mara kadhaa nikitarajia kupata suluhisho la haraka, lakini hali imeendelea kuwa ya kusuasua.

Jambo la kukatisha tamaa zaidi ni kwamba badala ya kupata majibu ya moja kwa moja, nimekuwa nikipewa ahadi za kusubiri zaidi na zaidi. Baadaye niliambiwa nitarejeshewa fedha ndani ya siku chache, lakini hata muda huo ulipopita sikupata mrejesho wa kuridhisha.

Kama unahitaji huduma ya internet kwa haraka, kwa matumizi ya kazi, biashara au masomo, nakushauri ufikirie kwa makini kabla ya kufanya malipo.

Na kama hupendi usumbufu wa kupiga simu mara kwa mara, kufuatilia kila siku na kusubiri majibu yasiyo na uhakika, basi ni vyema kufanya uchunguzi wa kina na kuangalia mbadala nyingine kabla ya kuamua kujiunga.

Mimi binafsi nimepoteza muda mwingi, nguvu na gharama za kufuatilia huduma niliyokuwa nategemea kuipata baada ya kulipa. Natoa tahadhari hii ili wengine waweze kufanya maamuzi kwa uangalifu na kujiepusha na changamoto nilizokutana nazo.

Fanya uchunguzi wako kwanza, uliza maswali yote muhimu kabla ya kulipa, na usitegemee ahadi pekee.
 
Pole mbona wamenyooka sana? Huenda upo eneo ambalo bado hawajalifikia na ulikuwa umeshaaminishwa imefika ndio maana wanakuzungusha!

Huyu alinisaidia mimi, jaribu kuongea naye! +255 783 351 727
Asante sana . Ila sihitaji tena huduma yao nifukuzia refund yangu
 
Pole mbona wamenyooka sana? Huenda upo eneo ambalo bado hawajalifikia na ulikuwa umeshaaminishwa imefika ndio maana wanakuzungusha!

Huyu alinisaidia mimi, jaribu kuongea naye! +255 783 351 727
Niliwapigia hawa savvana,nimeshangaa wanasema kukuunganishiabni bure,ila nikivyoomba waniunganishie wanasema nilipe kwanza kifurushi.
Nilitegemea waunge,then mimi nichague tu kifurushi na kujiunga
 
Niliwapigia hawa savvana,nimeshangaa wanasema kukuunganishiabni bure,ila nikivyoomba waniunganishie wanasema nilipe kwanza kifurushi.
Nilitegemea waunge,then mimi nichague tu kifurushi na kujiunga
Hmm hapo sasa sielewi, ila ni heri utafute hata 50k wakufungie mazima,
 
Kwangu naona Zuku inafanya vizuri, hapo nao kwenye issue za kiufundi ikitokea shida wana vichangamioto vyao, ila nje ya hapo huduma ni nzuri
 
Niliwapigia hawa savvana,nimeshangaa wanasema kukuunganishiabni bure,ila nikivyoomba waniunganishie wanasema nilipe kwanza kifurushi.
Nilitegemea waunge,then mimi nichague tu kifurushi na kujiunga
Hizi huduma ZA internet majumbani
Zuku
Savana
Na wengine, kuunganishiwa ni bure ila lazima ulipie kifurushi cha mwezi 45,000 - 55,000 ili wa process account siku wakija wakiunga ianze kutumika onSpot.
Kwa maelezo yako Savanah hawana huduma ya internet maeneo hayo pengine ungeshare details zaidi
Maeneo kama
Mbezi Beach
Mbweni
Makongo Juu
Goba
Kawe
Sinza
Kariakoo
Posta
Upanga
Mikocheni
Ubungo
Mwenge

Ukilipia hua wanakuunga ndani ya siku 3 maximum.
Share details zaidi
Mahali ulipo
No ulizowasiliana nazo
Receipt ya malipo kwa ufatiliaji
 
Pole mbona wamenyooka sana? Huenda upo eneo ambalo bado hawajalifikia na ulikuwa umeshaaminishwa imefika ndio maana wanakuzungusha!

Huyu alinisaidia mimi, jaribu kuongea naye! +255 783 351 727
Wako vizur na network yao iko sawa.

Hujakutana na TTCL . Watu walilipia toka mwaka juzi ila hadi leo nguzo zimewekwa ila wire haujafika..

Wakat wenzao Tigo na Savanna ndan ya wiki tu wanaweka nguzo na wire na kukuunganishia na huduma.
 
Mimi nililipia kifurushi service sijatoa hata senti, sasa sielewi unafunga cha nini kama
Hujajipanga kw awakati huo!
Sasa huyu anasema nilipie kifurushi kabla hawajafunga,
Hapa nahofia kupigwa
 
Niliwapigia hawa savvana,nimeshangaa wanasema kukuunganishiabni bure,ila nikivyoomba waniunganishie wanasema nilipe kwanza kifurushi.
Nilitegemea waunge,then mimi nichague tu kifurushi na kujiunga
Usijaribu kabisa ni matapeli wakubwa litageuka deni bora utafute alternative nyingine kabisa
 
Back
Top Bottom