Anayefikiria kujiunga na Savanna Fibre kuwa makini sana

Anayefikiria kujiunga na Savanna Fibre kuwa makini sana

Mtu ukiambiwa ulipe kwanza usikubali hasi uone mafundi mlangoni
 
Kutokana na uzoefu wangu binafsi, nashauri mtu yeyote anayefikiria kujiunga na Savanna Fibre kuwa makini sana kabla ya kufanya malipo.

Nilifanya malipo kwa matarajio ya kuunganishiwa huduma kwa muda uliotajwa, lakini hadi sasa nimepitisha zaidi ya miezi miwili bila kupata huduma kama nilivyotarajia.

Katika kipindi hicho nimekuwa nikifuatilia mara kwa mara, kupiga simu nyingi na kutuma ujumbe mara kadhaa nikitarajia kupata suluhisho la haraka, lakini hali imeendelea kuwa ya kusuasua.

Jambo la kukatisha tamaa zaidi ni kwamba badala ya kupata majibu ya moja kwa moja, nimekuwa nikipewa ahadi za kusubiri zaidi na zaidi. Baadaye niliambiwa nitarejeshewa fedha ndani ya siku chache, lakini hata muda huo ulipopita sikupata mrejesho wa kuridhisha.

Kama unahitaji huduma ya internet kwa haraka, kwa matumizi ya kazi, biashara au masomo, nakushauri ufikirie kwa makini kabla ya kufanya malipo.

Na kama hupendi usumbufu wa kupiga simu mara kwa mara, kufuatilia kila siku na kusubiri majibu yasiyo na uhakika, basi ni vyema kufanya uchunguzi wa kina na kuangalia mbadala nyingine kabla ya kuamua kujiunga.

Mimi binafsi nimepoteza muda mwingi, nguvu na gharama za kufuatilia huduma niliyokuwa nategemea kuipata baada ya kulipa. Natoa tahadhari hii ili wengine waweze kufanya maamuzi kwa uangalifu na kujiepusha na changamoto nilizokutana nazo.

Fanya uchunguzi wako kwanza, uliza maswali yote muhimu kabla ya kulipa, na usitegemee ahadi pekee.
Hao jamaa wapo connected na serikali? Hakuna kitu chochote kinachofanywa na serikali hii dhalimu ya CCM kikakosa kuwa na kasoro na uduwanzi mwingi.
 
Hao jamaa wapo connected na serikali? Hakuna kitu chochote kinachofanywa na serikali hii dhalimu ya CCM kikakosa kuwa na kasoro na uduwanzi mwingi.
Sina hakika ila ni kikampuni uchwara ambacho soon kitaenda kujifia
 
Mimi nililipia kifurushi service sijatoa hata senti, sasa sielewi unafunga cha nini kama
Hujajipanga kw awakati huo!
Sahihii kabisaa wao unalipia kifurushi tuu. Huduma ni buree kabisaa.

Sasa mtu kama hataki kulipa kifurushi halafu anataka wamfungie hiyo Huduma , ni jambo la kushangazq kidogo
 
Mimi nilivyo lipia kifurushi, baada ya siku moja walikuja kufunga mtambo wao
 
Kwangu naona Zuku inafanya vizuri, hapo nao kwenye issue za kiufundi ikitokea shida wana vichangamioto vyao, ila nje ya hapo huduma ni nzuri
upo mitaa gani chief, maana nimecheki coverage yao kwa Dsm ni Mbezi beachm KKOO na Mjini kati
 
Mkuu kama kwako haifanya kazi kabla ya lawama tafuta chanzo cha tatizo Kwa ; Je wamefika eneo lako? Savanna hawana shida hiyo wako very fast hawajamaa
Kabisa!!!! Mimi walinifungia siku hiyo hiyo niliyofanya malipo.
 
Back
Top Bottom