Anayefikiria kujiunga na Savanna Fibre kuwa makini sana

Anayefikiria kujiunga na Savanna Fibre kuwa makini sana

Kutokana na uzoefu wangu binafsi, nashauri mtu yeyote anayefikiria kujiunga na Savanna Fibre kuwa makini sana kabla ya kufanya malipo.

Nilifanya malipo kwa matarajio ya kuunganishiwa huduma kwa muda uliotajwa, lakini hadi sasa nimepitisha zaidi ya miezi miwili bila kupata huduma kama nilivyotarajia.

Katika kipindi hicho nimekuwa nikifuatilia mara kwa mara, kupiga simu nyingi na kutuma ujumbe mara kadhaa nikitarajia kupata suluhisho la haraka, lakini hali imeendelea kuwa ya kusuasua.

Jambo la kukatisha tamaa zaidi ni kwamba badala ya kupata majibu ya moja kwa moja, nimekuwa nikipewa ahadi za kusubiri zaidi na zaidi. Baadaye niliambiwa nitarejeshewa fedha ndani ya siku chache, lakini hata muda huo ulipopita sikupata mrejesho wa kuridhisha.

Kama unahitaji huduma ya internet kwa haraka, kwa matumizi ya kazi, biashara au masomo, nakushauri ufikirie kwa makini kabla ya kufanya malipo.

Na kama hupendi usumbufu wa kupiga simu mara kwa mara, kufuatilia kila siku na kusubiri majibu yasiyo na uhakika, basi ni vyema kufanya uchunguzi wa kina na kuangalia mbadala nyingine kabla ya kuamua kujiunga.

Mimi binafsi nimepoteza muda mwingi, nguvu na gharama za kufuatilia huduma niliyokuwa nategemea kuipata baada ya kulipa. Natoa tahadhari hii ili wengine waweze kufanya maamuzi kwa uangalifu na kujiepusha na changamoto nilizokutana nazo.

Fanya uchunguzi wako kwanza, uliza maswali yote muhimu kabla ya kulipa, na usitegemee ahadi pekee.
hiyo kitu ndio nini gentleman kwa faida ya wadau wa Jf?🐒
 
Hizi huduma ZA internet majumbani
Zuku
Savana
Na wengine, kuunganishiwa ni bure ila lazima ulipie kifurushi cha mwezi 45,000 - 55,000 ili wa process account siku wakija wakiunga ianze kutumika onSpot.
Kwa maelezo yako Savanah hawana huduma ya internet maeneo hayo pengine ungeshare details zaidi
Maeneo kama
Mbezi Beach
Mbweni
Makongo Juu
Goba
Kawe
Sinza
Kariakoo
Posta
Upanga
Mikocheni
Ubungo
Mwenge

Ukilipia hua wanakuunga ndani ya siku 3 maximum.
Share details zaidi
Mahali ulipo
No ulizowasiliana nazo
Receipt ya malipo kwa ufatiliaji
Wameconfirm eneo specifc kabisa Goba. Ndio wakaniruhusu kufanya malipo
 
Pole mbona wamenyooka sana? Huenda upo eneo ambalo bado hawajalifikia na ulikuwa umeshaaminishwa imefika ndio maana wanakuzungusha!

Huyu alinisaidia mimi, jaribu kuongea naye! +255 783 351 727
Hili bado ni kosa lao. Kama wanajua eneo hawajafika mbona walichukuwa malipo? Halafu unamshauri apige simu? Watanzania tujaribu kuelewa nguvu aliyonayo mteja na siyo tuendeleze utamaduni wa kubembeza mtoa huduma. Walipoingia kwenye biashara hawakujua kuwa wanatakiwa kujali wateja?
 
Hili bado ni kosa lao. Kama wanajua eneo hawajafika mbona walichukuwa malipo? Halafu unamshauri apige simu? Watanzania tujaribu kuelewa nguvu aliyonayo mteja na siyo tuendeleze utamaduni wa kubembeza mtoa huduma. Walipoingia kwenye biashara hawakujua kuwa wanatakiwa kujali wateja?
Hakuna kampuni inahuduma mbovu kama hiyo yaani ni takataka
 
Nimetoa tu onyo kwa members wa humu . Mtu asije toa pesa yake ikaenda bure.
Yaani utasumbuna na huduma kwa wateja hadi utakoma.
 
Mbaya zaidi kabla huja fanya malipo walikuwa wananipigia simu kibao kila muda baada ya kufanya malipo wamekula kona hadi leo
IMG_8611.jpeg
 
Usijaribu kabisa ni matapeli wakubwa litageuka deni bora utafute alternative nyingine kabisa
Mkuu kama kwako haifanya kazi kabla ya lawama tafuta chanzo cha tatizo Kwa ; Je wamefika eneo lako? Savanna hawana shida hiyo wako very fast hawajamaa
 
Pole mbona wamenyooka sana? Huenda upo eneo ambalo bado hawajalifikia na ulikuwa umeshaaminishwa imefika ndio maana wanakuzungusha!

Huyu alinisaidia mimi, jaribu kuongea naye! +255 783 351 727
Nipe experience mwanike. Bei zao zikoje, na speed pia.
 
Achananao hao takataka labda kama hupendi pesa zako au unapenda kusumbuana na huduma kwa wateja
 
Back
Top Bottom