House4Sale Anayehitaji kununua apartment Upanga

House4Sale Anayehitaji kununua apartment Upanga

Matangazo ya hivi huwa nayaita matangazo ya kikuda. kwa hivo namimi nilyeko milima ya andes na tolabora na nataka ninunue mjengo maskani yanipasa kufunga safari kuja upanga ili tu kujua bei??? Hata tu aliyepo chato itabidi aje dar kujua tu bei? Byashara gani hiyo mkuu mbona hatubadiliki na mbadiliko ya tabia maendeleo. kwanini usingepiga baragumu hapo upanga posta na kariakoo kuwa watu waje waulize bei na kuona? Weka atleast hata price ranges.
 
Kwani si aseme floor ya chini ina square metres ngapi na bei ni ngapi kwa sq mt? Au anaweka cha juu? Mwambieni akiuza lazima atoe risiti ya elektroniki. Mbona NHC wanaweka bei wazi?
 
Weka bei acha kutuzingua...Jengo tunalijua liko pale karibu na Sido. Ni jengo zuri na limejengwa na Mchina wa group six. Ila bila bei tangazo lako ni kazi bure.
Mods anzeni kung'oa mabango yote ya biashara ambayo hayana bei humu JF...
National Housing na NSSF nyumba zao wanatangaza bei kila siku
huyu sijui dalali anataka cha juu na ndio wanaoharibu biashara za watu
 
Hizi Ndio biashara za watanzania wengi. Mambo yanafanyika kama wachawi vile mtu anafanya biashara lakini kusema bei marufuku. Tuna safari ndefu sana
 
IVORY TOWER ltd. inauza apartment iko mjini kabisa , ni mwendo wa kutembe kwenda kariakoo, karibu na supermarkets, kuna chekechea mbili karibu na jengo za lugha ya kiingereza , pia ni karibu na mzumbe university,mtaa wa mfaume, na unaweza kutumia mwendo kasi kwa usafiri wa haraka, mauzo hayo ni kwa bei nafuu kabisa karibu piga namba 0766627538

KARIBU MILIKI APARTMENT YAKO. UNAKARIBISHWA HATA KUFIKA KUANGALIA TU.

hiyo sio RICHMUNDI tower kweli ?
 
Duniani kote bei za nyumba uweka hadharani sijui why Watanzania atuna tabia hii. please weka bei
Hii kitu huwa siipendi ila basi tu..Mara bei njoo pm...Mara karibu kwa mazungumzo...weka hadharani bei tafadhali
 
TUNA

ASANTE KWA USHAURI WAKO ILA KWA MASWALA YA BEI TUNASHAURI MNUNUAJI AFIKE OFISINI KABISA ILI TUYAJADILI ASANTE.

Kaka acha biashara za mkoloni, hivi Watanzania tuna shida gani?, kwa nini tunashindwa kujua biashara za mitandaoni?, hakuna biashara ya Mtandaoni inayoficha bei, iwe Alibaba, au Qatar Air, Be foward nk kote uko unakuta bei, wewe unaficha nini?
Kwani hamna vipeperushi vyenye kuonyesha kila Apartment na bei zake?, ki scan hicho kipeperushi na ukiweke hapa

Biashara ya mitandaoni watu wanavutiwa na Picha na kisha bei
 
bei zinatoofautiana kulingana na floor ivyo ingekuwa vizur ufike ili uone bei ambayo unaweza kuiafford, na ss hv tuna promosion karibu
Wengine toka mbali, ukiweka bei kulingana na apartment, itasaidia mtu kujua kama anaweza nunua au atafte kiwanja majohe ajenge mwenyewe.

Tuwekee kwa kuzijgatia floor zake ili mtu ajitathmini
 
bei zinatoofautiana kulingana na floor ivyo ingekuwa vizur ufike ili uone bei ambayo unaweza kuiafford, na ss hv tuna promosion karibu
Sasa kama mimi nipo nchi jirani nitafikaje? Naweza kumtuma mtu aje aangalie anitumie na picha anipe na bei nukipigwa atakuwa amenipiga wewe au rafiki yangu? Weka bei kuanzia shiling kadhaa mpaka kadhaa ili nikimtuma mtu niwe najua bei asinipige cha juu.
 
Back
Top Bottom