Anayejua kuhusu hili la RITA anisaidie tafadhali

Wewe acha kukaza jugula. Sajili mtoto kama mtanzania vinginevyo kama unasimamia ukweli kwanini usiende kumchukulia cheti Cha kuzaliwa Kenya. Utaingia gharama kwa kukaza fuvu, nenda uhamiaji wakupe taratibu maana naona huelewi.
Sawa bwashee
 
Asante
 
Okey,

lakini kwanini asipewe hapa cheti na kiandikwe kuwa amezaliwa kenya na mama mkenya ila baba ni mtanzania?
Na je, nikitaka kumuombea passport book sasa hivi atweza kupewa?
Sijui ana umri gani, hata ukitaka kumuombea passport itakubidi upeleke kwanza cheti cha kuzaliwa cha Kenya.
 
Sijui ana umri gani, hata ukitaka kumuombea passport itakubidi upeleke kwanza cheti cha kuzaliwa cha Kenya.
Ana mwaka mmoja,
Ila hichi ulichosema sasa ndio nilikua nataka kujua, yaani kumbe naweza kumtengezea ppt ya Tanzania na hicho hicho cheti cha kuzaliwa cha kenya?
 
Ana mwaka mmoja,
Ila hichi ulichosema sasa ndio nilikua nataka kujua, yaani kumbe naweza kumtengezea ppt ya Tanzania na hicho hicho cheti cha kuzaliwa cha kenya?
Ndio. Unaweza kupata passport yake kama unasafiri nae kwenda popote, zamani kulikuwa na kurasa za kuandika watoto kwenye passport yako, siku hizi hamna hiyo, ila cheti cha kuzaliwa cha Kenya ndio msingi wa mambo yote kwenye kesi yako hii.
 
Naomba connection za ubwabwa
 
Sio ndio maendeleo unayoyapigania ya huyu mzenji

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
 
Unathani we una utakatifu kuliko ibrahim aliyeamua kusema mkewe ni dada yake....ili asolve tatizo lake muda ule...na Mungu hakuhangaika na Ibrahim akahamgaika na mfalme....! Au elisha aliyesema kuwa wanaemtafuta sio yeye ila ngoja awapeleka kwa wanaemtafuta ilihali alijua wanamtafuta yeye....!!! (2Wafalame 6: 19) amini kuwa kuna vitu vipo nje ya uwezo wako na njia zako haziwezi kuziweka sawa...labda kama unataka kutoa rushwa....au...We endelea kuhangaika la rita baadae utakuta hiyo nchi imeingizwa kwenye list.
 
Mie baba ni mtanzania, mama ni mkenya
Mpaka sasa ana uraia wa inchi mbili mpaka atakapofika 18
Ila wakuu nimeomba kwa anaejua tafadhali anielekeze naona uvivu kurudi tena rita
Kwani si umeshaelekezwa fanya kama kazaliwa mkoani kwako ulipo huwezi nenda katumie mfumo wa usajili uliopo burundi
 
Duh, sio mchezo, Kwahiyo hapo nimewaaibishaje kwa mfano
Ushamba mzgo hivi nani alikwambia uraia ni ukabila ety mtoto afuate uraia wa baba hiyo doesn't make sense man
Ushamba mwingine ety unaitafuta Kenya kwenye Rita ya Tanzania bro are you serious? Na umekazania kwel
Hv unadhania Kenya ni mkoa au ni sehem ya Tanzania
Dat stupidity
 
Sikia, unayo nafasi ya kwenda kuandikisha mtoto kazaliwa nyumbani ukamtafutia cheti cha kuzaliwa cha Tanzania.
Au
Kuwa mkweli kamtafutie cheti cha kuzaliwa cha Kenya aje aombe uraia wa Tanzania baadae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…