Anayejua kuhusu hili la RITA anisaidie tafadhali

Mie yahe natafta cheti tu cha tanzania
Hayo ya uraia ni wewe unasema
 
Hapa sasa umenisaidia kidogo, ingawa bado hujaniongoza kipi cha kufanya baada ya kushindwa kuipata kenya kwenye form ya maelezo ya mtoto online ya rita website
Ni mkenya kwa kuzaliwa hivyo inabidi awe na cheti cha kuzaliwa kenya maana emezaliwa ardhi ya kenya.There is no way amezaliwa tz/ aandikishwe tz! Rekodi zake za kizazi zipo kenya.
Ila ni mtanzania kwa kurithi kwa wazazi Hivyo akifikisha miaka 18 ndipo kisheria ana uhuru wa kuamua abaki raia wa kenya au aukane uraia wa kenya abaki na utanzania.Hivyo usihangaike na rita kwa sasa.Option 2 ndio hiyo ya kudanganya lkn kwa maelezo yako nimefarijika kuwa huna tabia hiyo
 
Si akaombe cheti cha kuzaliwa Kenya ?Mtoto kazaliwa Kenya jamani,halafu unaomba cheti chake cha kuzaliwa Tanzania.
 
Ila broo we ulioaje Kenya Kuna utaratibu wowote Wa kufata nina manzi wangu yupo kule nataka nimuoe kama vip
 
Okey,

lakini kwanini asipewe hapa cheti na kiandikwe kuwa amezaliwa kenya na mama mkenya ila baba ni mtanzania?
Na je, nikitaka kumuombea passport book sasa hivi atweza kupewa?
Ila mkuu khaa samahani, mbona hutaki kuelewa wakati wadau wanakuelewesha vizuri kabisa kwamba ni kitu kisichowezekana sababu aliyezaliwa kenya atapata cheti huko??

Au unachotaka wewe ni sifa ya kuzaa na mkenya na mtoto aliezaliwa Kenya?? Unahisi ni kitu special sana au?? Sorry kama nimekukwaza ila sijakuelewa unachotaka.
 
Okey,

lakini kwanini asipewe hapa cheti na kiandikwe kuwa amezaliwa kenya na mama mkenya ila baba ni mtanzania?
Na je, nikitaka kumuombea passport book sasa hivi atweza kupewa?
Mbona una kichwa kichwa kigumu sana. Umeambia cheti cha kuzaliwa hutolewa na nchi ulikozaliwa. Yeye alizaliwa Kenya halafu unataka Tanzania wampe cheti cha kuzaliwa. Haiwezekani. Kuhusu passport anapata bila shida. Unaomba kwa kutumia cheti cha kuzaliwa alichopewa Kenya. Passport itaandikwa alizaliwa Kenya. Ila akifikisha miaka 18 atachugua uraia mmoja tu
 
Iko hivi,
Chukua cheti cha kuzaliwa cha Kenya,nenda nayo uhamiaji watakupa barua ya kuwa raia wa Tanzania kwa Kurithi.Hiyo barua ataitumia pamoja na cheti chake cha kuzaliwa.
Huyo ni Mtanzania kwa kurithi na si Mtanzania kwa kuzaliwa.
Rita watakupotezea muda wako.
 
Mungu akupe baraka na neema
 
Asante sana mkuu,
Ni slow learner
 
Asante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…